KALAle MAHALI PEMA PEPONI ELVIS MUSIBA

Sunday, October 31, 2010
Lukwangule:Mguu ndio uliomuua Musiba
Elvis Musiba enzi za Uhai Wake.
----
Kwa taarifa zilizopatikana,zinaeleza kuwa marehemu Elvis Musiba alifariki katika hospitali ya TMJ leo saa nne asubuhi.Taarifa zinazidi kueleza kuwa Musiba alilazwa jana katika hospitali hiyo akisumbuliwa na mguu ambao ulifanyiwa operesheni hivi karibuni nchini India.

Mipango ya maziko inafanywa nyumbani kwake Mikocheni na wanafamilia wanajadiliana kuhusu mazishi na maziko ya mpendwa wao.

Mungu ailaze roho ya mahali pema peponi-AMIN.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, October 31, 2010 | | Permalink | Maoni 7

Dk slaa akipiga kura leo

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa akipiga kura katika kituo cha Gongali kilichopo katika kata ya Qurus wilayani Karatu mkoani Arusha mapema leo asubuhi.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa akipata maelezo kutoka kwa wasimamizi wa kituo cha kupigia kura cha Gongali wilayani Karatu leo.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Wilbroad Slaa akiwa na Mkewe Josephine,wakati wakisalimiana na wanachi wa eneo hilo mara baada ya kumaliza kupiga kura leo asubuhi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, October 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

jk apiga kura kijijini kwake msoga

JK akionesha kidole chake kuashiria tayari amekwisha piga kura
Mgombea Urasi kwa chama cha CCM.Dk Jaka Kikwete akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Msoga, kata ya Msoga leo asubuhi.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi Msoga leo asubuhi(picha na Freddy Maro).

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, October 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Dk shein apiga kura oysterbay jijini dar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura kuchaguwa Rais, Mbunge na Diwani katika kituo cha kupiga kura Oysterbay jijini Dar es salaam leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa kwenye chumba cha siri kwa ajili ya kupiga kura ya kuchaguwa Rais, Mbunge na Diwani katika kituo cha kupiga kura Oysterbay jijini Dar es salaam leo.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Mama Mwanamwema Shein, akipiga kura ya kuchaguwa Rais Mbunge na Diwani katika kituo cha kupiga kura Oysterbay jijini Dar es salaam leo. Picha na Amour Nassor VPO.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, October 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Mbatia azuiliwa kupiga kura zaidi ya masaa matano..!

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, October 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

waziri mkuu pinda apiga kura kijijini kwake.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga kura kwenye kituo cha uchaguzi kijijini kwake, Kibaoni, Katavi mapema leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mke wa Waziri Mkuu. MamaTunu Pinda akipiga kura kwenye kituo cha Uchaguzi kijijini Kibaoni, Katavi, mapema leo. (Picha na Ofisi ya WAziri Mkuu).
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, October 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

DK. Gharib Bilal APIGA KURA KIEMBE SAMAKI

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akionyesha vidole vyake vikiwa na wino baada ya kutoka katika chumba cha kupigia kura kwenye Kituo cha Kiembe Samaki leo.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika chumba cha kupigia kura katika kituo cha Kiembe Samaki mjini Zanzibar leo.
Mohamed Said Abdul, mkazi wa Kiembe Samaki Zanzibar, akielekezwa kutumbukiza karatasi yake ya kura katika boksi katika Kituo cha Uchaguzi cha Kiembe Samaki leo.
Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na mwananchi mkazi wa Kiembe Samaki, Mohamed Said Abdul, ambaye ni mlemavu wa macho aliyesindikiza katika kituo hicho cha Uchaguzi cha Kiembe Samaki kutimiza haki yake ya msingi ya kupiga kura leo
Mgombe mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitumbukiza karatasi ya kupigia kura wakati alipofika katika kituo cha uchaguzi cha Kiembe Samaki mjini Zanzibar mapema leo asubuhi.Picha na Muhidin Sufiani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, October 31, 2010 | | Permalink | Maoni 1
Idadi ya watu