



NA MAGRETH KINABO NA MARY KWEKA- MAELEZO
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Lawrence Masha amelitaka jeshi la polisi lisivunjike moyo kwa kuongezeka kwa taarifa za uhalifu katika vituo vya polisi bali wachukulie kama changamoto na kujidhatiti kukamirisha mikakati ya kukabiliana na matukio hayo.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri Masha wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya wakaguzi wasaidizi wa jeshi hilo, iliyofanyika katika Chuo cha Polisi Dar es Salaam. “Mnao wajibu wa kuwa mstari wa mbele katika kupanga mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto hizi,” alisema Waziri Masha.Alizitaja sababau za kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kuwa ni maendeleo ya Sayansi na teknolojia, ukosefu wa ajira, utandawazi, umasikini, ukuaji wa miji, ongezeko la makazi holela, kuzagaa kwa silaha, imani za kishirikina,ongezeko la pengo baina ya matajiri na masikini pamoja na utumiaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Waziri Masha alisema kuongezeka kwa taarifa za uhalifu katika vituo vya polisi ni miongoni mwa mafanikio ya jitihada zinazofanywa na jeshi hilo, kuwahamasisha wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao. Hata hivyo Waziri Masha aliongeza kuwa makosa yanayowakera wananchi kama unyanga’nyi na uvunjaji wa majumba na wizi yamepungua.
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2008 makosa ya uvunjaji yalikuwa 27,491 na mwaka 2009 yalipungua hadi 26,561 hivyo kupungua kwa asilimia 3.4, wakati makosa ya wizi mwaka 2008 yalikuwa 31,130 na mwaka 2009 yalipungua hadi kufikia 28,427, hivyo yamepungua kwa asilimia 8.7.
Waziri Masha alilipongeza jeshi hilo, kwa kuendelea na mpango wa kuratibu na kusimamia mafunzo ya walinzi wa amani kimataifa ikiwa ni pamoja na kushiriki kwa vitendo shughuli za kulinda amani sehemu mbalimbali duniani.“Serikali inaendelea kuvijengea mazingira mazuri vyombo vya ulinzi na usalama na kutatua matatizo ya makazi na maslahi ya watumishi wake.
Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) katika mwaka huu wa fedha inaendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za askari kwa kujenga maghorofa 30 kambi ya polisi barabara ya Kilwa, sita kambi ya Mabatini Mwanza, sita Musoma , Mara, Tatu Byekera ,Bukoba, 12 Ludewa Iringa, nane Kiwanja cha ndege Arusha, mbili Unguja Kuu Unguja na mbili Finya Kaskazini, Pemba.
Naye Mkuu wa chuo hicho, Elice Mapunda alisema kitaanza kutoa diploma ya sayansi ya polisi kuanzia mwaka 2010/2011 ikiwa ni jitihada za kukipandisha hadhi.Alisema jumla ya wanafuzi walioripoti katika mafunzo hayo walikuwa 356 na wote wamefaulu, lakini wawili kati yao walishindwa kushiriki kikamilifu baada ya kuumia wakiwa chuoni.
KCB Tanzania yajitolea kulea watoto yatima
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya KCB Tanzania imeamua kubeba jukumu la kuwalea watoto 11 wa kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kwa kukikisaidia na kukihudumia kwa mahitaji ya vifaa muhimu vya shule kwa watoto hao kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali wenye thamani ya zaidi milioni 2/- kwa ajili ya takribani watoto 45 wa shule hiyo,Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Christina Manyenye alisema kwa kuanzia wametoa vifaa hivyo ili viwasaidie kwanza yatima.
Akifafanua alisema kutokana na kuguswa na watoto wa kituo hicho kilicho chini ya Shirika la Empowering Children and Community Organization kilichoanzishwa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wameona wakisaidie kutokana na kuona kwamba ndoto za watoto hao ni sawa na za wanaotoka katika familia zinazojimudu kimaisha.
“Hivyo basi hatuna budi kuwasaidia watoto hawa na tunaahidi kuendelea kuwasaidia ili kukipunguzia mzigo kituo cha Amani jukumu la kuwalea watoto kituo hiki cha Amani ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kusoma. Ni wachache sana wanaoweza kufanya ubinadamu huu,” alisema Manyeye.
Hata hivyo aliongeza kwamba msaada huo umefuatia KCB Tanzania kutambua umuhimu wa jamii na kufahamu ukweli kuwa maendeleo ya jamii ni maendeleo ya taifa zima. Aidha alisema bila jamii yenye maendeleo uwepo wao kama benki utakuwa na mashaka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Margareth Mwegalawa alisema kuwa licha kuhudumia watoto yatima 11 wanaoishi bweni, pia wanahudumia watoto wengine wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia vifaa vya shule na mahitaji mengine.
Hata hivyo wanakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kulala watoto, vitanda, uchakavu milango na madirisha ya jengo la kituo hicho jambo linalochangia kituo kuchukua watoto wachache wanaoendelea kuishi kwenye mazingira magumu.
Kutokana na hilo waliiomba KCB Tanzania na taasisi zingine kujitokeza kukisaidia kituo hicho kwa kukipa misaada mingine ikiwemo magodoro, vitanda, vifaa vya kusomea watoto, vyakula, madawati ya kukalia na vifaa vya kufundishia.
Nae Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Bunju, Syzgo Alexander aliiopongeza benki hiyo kwa kuwa na moyo huo wa kujitolea na kusema kutokana na mahali kilipo kituo imeonesha imejitoa kuihudumia jamii kwa hali na mali jambo alilotaka liiungwe mkon o na Watanzania.
KCB Tanzania ni benki kubwa Afrika Mashariki ikiwa na rasilimali nyingi ikiwemo matawi zaidi ya 200 na mashine zaidi ya 400 za kutolea fedha (ATM) zilizotawanywa kote Afrika Mashariki na mtandao unaofikia nchi za Rwanda na Sudan Kusini.

WATOTO MKOANI KIGOMA NA RUKWA KUPATIWA CHANJO YA POLIO.
Na. Aron Msigwa - MAELEZO.
Serikali imewataka wananchi wa mikoa ya Kigoma na Rukwa kushiriki kikamilifu katika awamu ya pili ya zoezi la utoaji wa chanjo ya ugonjwa wa kupooza (polio) kwa watoto walio chini ya miaka mitano litakolofanyika tarehe 4 hadi tarehe 7 mwezi Oktoba, 2010.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni amesema kuwa hatua ya kufanyika kwa zoezi la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto katika mikoa hiyo, inafuatia taarifa ya kutokea kwa mlipuko wa Ugonjwa huo katika wilaya ya Kalemie nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mwezi Agosti mwaka huu.
Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilichukua hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini kutokana na jiografia kati ya Tanzania na DRC ,pamoja na muingiliano wa watu katika maeneo hayo kwa kuihamasisha jamii na viongozi wa ngazi zote mkoani Kigoma na Rukwa na wadau wengine kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo .
Mbali na hatua hiyo amesema, serikali iliendesha zoezi la kutoa chanjo ya polio kwa watoto wote walio na umri chini ya mika mitano kwa njia ya Kampeni , Kuimarisha utoaji wa taarifa za wagonjwa waliopata ulemavu wa ghafla na uimarishaji wa utoaji wa chanjo za kawaida ambapo matokeo ya zoezi la awali yanaonyesha mafanikio kwa kufikia kiwango cha asilimia 90 ya chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano.
Amesema mwongozo wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) unabainisha kuwa ili kudhibiti mzunguko wa virusi pori vya ugonjwa wa polio ni muhimu kutoa chanjo za ziada kwa njia ya kampeni kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka angalau kwa awamu mbili.
Hata hivyo amefafanua kuwa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo watahakikisha kuwa vitendea kazi kwa ajili ya Kampeni hiyo zikiwemo chanjo na vifaa vingine vinaapatikana katika muda muafaka .
“Kampeni na zoezi la utoaji wa chanjo hii katika mikoa ya Rukwa na Kigoma litafanyika kwa mafanikio makubwa kutokana na kuwepo kwa vifaa muhimu kwa shughuli hiyo ambavyo tayari vimeanza kusambazwa” amefafanua Bi.Nyoni.
Amesitsitiza kuwa chanjo hii ya Polio itakayotolewa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wapatao 703,389 katika mikoa yote miwili ni salama na itatolewa na wataalam wa afya kwa njia ya matone kinywani kwa watoto wote bila kujali kama walipata chanjo hiyo hapo awali au hawakupata.
Ametoa wito kwa wazazi na wananchi wote kushiriki kikamilifu katika zoezi hili kwa kushirikiana na wataalam wa afya watakaopita nyumba hadi nyumba na kuongeza kuwa watoto wote watakaopata chanjo hiyo watawekewa alama maalum katika kidole kidogo cha mkono wa kushoto ili kusaidia ufuatiliaji na uhakiki pamoja na kuweka alama kwenye nyumba zitakazofikiwa kulingana na hali ya chanjo ya watoto waliopo katika nyumba hizo.
Jopo la majaji lakutana kuchagua walifanikiwa kuingia nusu fainali shindano la mbunifu wa mavazi wanaochipukia
16 waingia katika nusu fainali ya wabunifu wanaochipukia na majina yao yatajwa
“Contemporary Swahili” ni kauli mbiu ya shindano 2010
Majina ya wabunifu 16 wenye vipaji ambao wataingia katika nusu fainali na kushindania zawadi ya mwaka katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week 2010 wapatikana.
Uchaguzi wa wabunifu wa mavazi wanaochipukia umefanyika Septemba 29 katika hotel ya Southern Sun jijini Dar es salaam, ambapo majina 16 yalichaguliwa na jopo la majaji watatu ambao ni Manju Msitta kutoka Smart Afrika Design Label, Charles Washoma, CEO of African Life assurance and One of Dar es Salaams Fashionable man na Director of arts Nsao Shalua of Baraza la Sanaa la Taifa (National arts Council).
Wabunifu hao 16 waliochaguliwa katika nusu fainali, kwa mara nyingine tena watachuana katika mchujo wa kuwapata wabunifu wa mavazi wanaochipukia wanane (8) ambao watashindana katika kuonyesha kazi zao katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week litakayofanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.
Mratibu wa Swahili Fashion Week, Ndugu Washington Benbella amesema kuwa “Muitikio umekuwa ni mzuri, ari na hamu imeonyesha vipaji vya hali ya juu vya ubunifu wa mavazi ambavyo vipo hapa nchini, lakini kwa wale ambao hawakupahatika kupata nafasi ya kuchaguliwa wasiishie hapa na wasikate tamaa bali waendelee na kuhakikisha kwamba wanafanikiwa na kufikia malengo yao”
Wabunifu wa mavazi wanaochipukia waliofanikiwa kuingia nusu fainali ni pamoja na Zarina Suleiman, Pooja Narendrakumar Jeshang, Abduel Urasa, ShaibMfaume, Annette Ngogi, Mwajabu Sadiki, Diana Malenge, Mgece Makory, Omary Bundalah, Kelvin Boniface, Subira Rahma Wahure, Nadia. A. Ahmed, Angelina Muna, Jacqueline Chipeta, Bami Musese na Grace Kijo.
Majaji walikuwa na kazi ya ziada, kwani walikuwa makini katika kuangalia mambo mbalimbali ili kuweza kupitisha majina ya wabunifu wa mavazi wanaochipukia, kwani walilazimika kualiangalia uwezo katika ubunifu na kuchora, kwa kiasi gani mchoro unavitia, rangi iliyotumika katika mchoro na mambo mbalimbali yanayohusiana na ubunifu kwa ujumla.
Sahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.
Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika November 2010, Dar Es Salaam, Tanzania.
Shindano hili linafanyika kwa mwaka wa tatu sasa, halina kikwazo cha umri, na linatoa fursa kwa watu wote wanaoamini kwamba wana kipaji cha ubunifu, na wanataka kuwa wabunifu. “Swahili Fashion Week ni jukwaa bora kwa wabunifu kuonyesha uwezo wao wa ubunifu na kuibua sindano la wabunifu wapya, ni jukwaa linalowawezesha watu kufikia malengo yao ”, aliongeza Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week.

Baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamesurika na ajali iliyotokea jana maeneo ya Kibaha -Tanita wakati wakielekea mjini morogoro kwenye mpambano wa timu ya Simba na Mtibwa,mara baada ya basi lao kupinduka na kupelekea mtu mmoja kupoteza maisha.Picha kwa hisani ya Shafii Dauda wa Sports Bar ya Clouds TV.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimvisha kofia yake Katibu wa Shina la Wakereketwa la Wajasiliamali la wauza Samaki na Dagaa, baada ya kuzindua shina hilo lililopo mtaa wa Karume Sumbawanga mjini leo.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi Tawi la Shina la Wakereketwa la Wajasiliamali la wauza Samaki na Dagaa, baada ya kuzindua shina hilo lililopo mtaa wa Karume Sumbawanga mjini leo .
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Zakia Bilal, wakiinua mikono kuwasalimia wananchi wa Kijiji cha Ilembo Wilaya ya Mbeya Vijijini, wakati walipowasili kijijini hapo juzi Sept 28 kufanya mkutano wa kampeni.
Mmiliki wa bendi ya Mashujaa ajulikanae kwa jina la Mama Sakina,akiwaomba radhi baadhi ya waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa kimataifa wa Mwl JK Nyerere,Kufuatia kutukanwa kwao na baadhi ya Mabaunsa waliofika uwanjani hapo huku wakiwa wamelewa,Mama Sakina pia alitoa ufafanuzi wa vurugu zilizotokea uwanjani hapo wakati wa kumpokea Ferre Gola,akieleza kuwa watu hao walikuwa wametumwa kwa ajili ya kuja kumuharibia mapokezi hayo wakiwemo na baadhi ya Mabaunsa ambao walikuwa wamelewa kupita kiasi huku wakitukana matusi mazito mazito kwa Waandishi wa habari waliokuja uwanjani hapo kufanya kazi yao.
Mwimbaji na rapa wa Mwanamuziki Ferre Gola kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo anayejulikana kama (Shikitu) akihojiwa na wanahabari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K,Nyerere, hata hivyo Kiongozi wao mwanamuziki Ferre Gola anatarajiwa kuwasili leo mnamo saa 12 jioni na anatarajia kufanya onyesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho Ijumaa akishirikiana na bendi ya Mashujaa inayoongozwa na Mwanamuziki Jado Field Force.
Mwimbaji na rapa mahiri wa mwanamuziki Ferre Gola kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo anayejulikana kama (Shikitu) akipewa escot na Baunsa mara baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K,Nyerere.(Kwa Wahusika naomba nidhamu ya Baunsa huyu ambaye kwa bahati mbaya sikuweza kulibaini jina lake mapema,naomba ichunguzwe kwa makini awapo kazini) .!
Mwanamuziki mpiga gitaa la Sollo kutoka kundi la Ferre Gola anayejulikana kama Chally Sollo akihojiwa na vyombo vya habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere mara baada ya kuwasili kwa ajili ya onyesho lao linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kesho Ijumaa.
Baadhi ya Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakiongozwa na kiongozi wa bendi hiyo Jado Field Force (haonekani pichani) katika kutia nakshi nakshi ujio wa mwanamuziki Ferre Gola (Shetani) mbele ya Camera ya Clouds Tv wakati walipokuwa wakimsubiri mwanamuziki huyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K.Nrerere usiku wa kuamkia leo, pamoja na shamra shamra hizo Mwanamuziki huyo hakuweza kuwasili usiku wa jana,badala yale anatua leo jioni jijini Dar mnamo majira ya saa 12 na ushehe hivi,waliotangulia ni wanamuziki wake.
Mama Asia Idarous Hamsini ambaye pia ni mkongwe katika fani ya ubunifu wa mavazi amenaswa na kamera Jiachie usiku huu ndani ya Uwnja wa ndege wa kimataifa wa Mwl JK Nyerere alipokuwa akimpokea mumewe Mzee Hamsini kutoka huko Ughaibuni ,ambaye ametua rasmi kwa ajili ya onyesho la usiku wa Kanga za Kale litakalofanyika ijumaa usiku katika ukumbi wa Diamond VIP.
Vodacom Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel akiwa amepozi kwa picha huku akiwa ameishikilia bendera ya Taifa kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha katika mashindano ya Miss World yatakayofanyika hapo baadae mwaka huu nchini China.
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akimkabidhi kinyago Miss Tanzania 2010 Geneviev Emmanuel kama sehemu ya kwenda kuitangaza nchi yetu,Mlimbwende huyo anatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea Beijing,China ambako mashindano hayo yatafanyika.
Kushoto ni Mama mzazi wa Miss Tanzania Genevieve wakiwa na aliyekuwa mgeni rasmi Mkuu wa Sekta Binafsi nchini Ester Mkwizu na baba yake Emmanuel Mpangala katika picha ya pamoja na Miss Tanzania 2010.
Kutoka kushoto ni mlezi wa Miss Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji nchini (TIC),Emmanuel Ole Naiko,Mkuu wa Sekta Binafsi nchini Bi. Ester Mkwizu, Genevieve,
Pichani kati ni mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania,Martina Nkurlu na wadau wengine wakifuatilia kwa makini hafla hiyo ya kukabidhiwa bendera ya Taifa,Vodacom Miss Tanzania 2010 Geneviev mapema leo asubuhi jijini Dar.
Na Mwandishi wetuProgrammed virus:
Watu wengi sana kwa sasa wanalalamika virus wamekula mafaili (Files and folder) kwenye flash drive.
Solution ipo kama unataka kuwa safe: KURUDISHA FILE ZILIZOPOTEA
maelezo machache:
There are some virus that will cause destruction such as encrypting recently used files so you are forced to buy the decryption key from the virus programmer.(from eastern Europe(..) and others country)
Then there’s another type of virus such as BDS.Mirc.Backdoor that will hide your documents files by setting the hidden and system attributes to the file. You can still see the files if you set to show hidden files and folders plus disabling hide operating system files. If the virus is capable of restricting Folder Options, chances are you think that your files has been wiped out by the virus but in fact it is hidden in your system.
Contact: DON COMPUTER CARE SERVICES
0787-291773 begin_of_the_skype_highlighting 0787-291773 end_of_the_skype_highlighting OR O716-291773
LOCATION: BHESCO BUILDING 1ST FLOOR, NEAR TO CHEF'S PRIDE RESTAURANT (DAR ES SALAAM)
KAMA UNAHITAJI KURUDISHA FILE ZAKO MUHIMU,
HABARI YAKAZI, KAKA MIMI NIKIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 26, NINA ELIMU YA FORM FOUR DARAJA LA TATU .
KAKA KAMA ILVYO KAWAIDA WIMBIKUBWA LA VIJANA WANA MAIZA KIDATO CHA NNE ILA NAMNA YA KUJIENDELEZA INA KUA NGUM KUTOKANA
NA HALI ZA KIUCHUMI.
NIWAZI NIMEJARIBU KUJIKUSANYA KWAKUFANYA KIBARUWA NA MPAKA SASA NINA $2000. JE NICHUO KIPI NINAWEZA KUPATA ELIMU YA I.T. INFORMATION technology katika ngazi za shahada nje ya nchi. Please naomba mchango wako wa mawazo.
Regards,
Mahuba H. Hilaly
Vodashop Consultant- Kigoma
Mob:(+255) 752 855 116 begin_of_the_skype_highlighting (+255) 752 855 116 end_of_the_skype_highlighting
MSAADA TUTANI
Nina msaada ninaotaka kusaidiwa na watanzania wenzangu hasa walio Tanzania japokuwa hata wanje ya Tanzania nao waweza changia. Mim nipo huku ughaibuni kwa mda mrefu kidogo ila kwa sasa nataka nirudi nyumbani na kuanzisha biashara zangu binafsi ambazo zitakuwa zinahusika na uingizaji wa bidhaa ndani ya Tanzania kutoka USA, Je ni aina gani ya bishara ninayoweza kufanya yenye manufaa kwangu na watanzania?, ambayo itahusu mambo makuu matatu MAVAZI, CHAKULA NA MALAZI
Nitashukuru kwa mawazo na michango yenu!!!!!
Mgombea Mwenza wa urais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Jeras Fungo, ambaye ni mlemavu wa miguu Mkazi wa Kijiji cha Ihai, Kata mpya ya Ihai, aliyefika katika mkutano wa kampeni kijiji cha Chimala, baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika katika eneo la Stendi ya zamani ya Mabasi Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya leo.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilala, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbalali, Modestus Kilufi, wakati alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni kwenye eneo la Stendi ya zamani ya Mabasi Wilaya ya MbalaIali leo.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa CCM wa Kijiji cha Chimala Isitu, wakati alipowasili kwenye eneo la Stendi ya zamani ya mabasi ya Chimala, Wilaya ya Mbalali Mkoa wa Mbeya kufanya mkutano wa kampeni leo.
Mbunifu mkongwe wa mavazi hapa nchini,Mama Asia Idarous Hamsini wa Fabak Fashions akizungumza leo asubuhi na waandishi wa habari kuhusiana na onyesho lake la usiku wa kanga za kale 2010.
Pichani kulia ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bw. Iman Lwinga akizungumza machache mbele wa waandishi wa habari leo asubuhi ndani ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regency,jijini Dar kuhusiana na udhamini wao kupitia bia yao ya Tusker ndani ya onesho hilo la Usiku wa kanga za kale 2010.