mambo ya jiving mnusoni

Wednesday, March 31, 2010

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 6

tid ajitoa tuzo za kili music awards ?!


Wanajamvini nimeshitushwa kidoogo na taarifa hii ya msanii Khalid Mohamed a.k.a Top in Dar a.k.a T.I.D,kwamba amejitoa kwenye tuzo kubwa kabisa za muziki hapa Tanzania za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010,kwa mujibu wake na maandishi yake,ametoa sababu zake hizo hapo chini.

======= ======= ========== ==========


Naomba radhi kwa mashabiki wangu wote kutoka pande zote za sayari hii najua mlikua mnasubiria kunipigia kura kwenye hiki kinyanganyiro cha award hizi za kilimanjaro,najua imekua uamuzi muafaka kwangu kujitoa kwene awards hizi basi naomba muelewe sababu zangu hizi za msingi:


1.Kwanza nahisi mimi kama TID na mziki ninao perfom kwa kipindi chote hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo hizi sina umuhimu wa kuwa shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao unakubalika sana na wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki hiyo naona sioni sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.


2.Pia nilidhani labda ni upungufu wa mawazo ya majaji ama waandaaji ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi fulani nilipokuwa nafanya nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine ambao uko nao kwene same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili kutokana na juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini nisiwe mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za viwango vya juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!


3.Kwa sababu hizi ambazo mimi naona kwangu hazinijengi sioni sababu ya kuwepo kwenye TUNZO hizi tena kwani sidhani kama ni wakati wa kuwaangusha mashabiki wangu ambao natumia muda mwingi na effort binafsi bila ya mdhamini kuwaunganisha na muziki wangu basi nisameheni kama nimewakosea lakini hainisaidii chochote endeleeni na hao mnaowapa kila category i will never stop making good music for my country surely i wont,i was born to do


THIS,.. THANKS.


NB:Taarifa hii iko HAPA

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 9

tamasha la pasaka maandalizi yake yazidi kunoga

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

tigo waibuka na promosheni mpya


Kushoto ni meneja Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando na kulia ni meneja matangazo na promosheni Redemtus masaja akizindua Rasmi viwango nafuu vipya vya mawasiliano kwa wateja wa Tigo kuanzia kesho. Ukiwa Tigo Thumni inathamani kama zamani!Ongea utakavyo, sasa ni nusu shilingi kila sekunde baada ya dakika ya kwanza,saa20 kwa siku, kasoro saa12jioni-4usiku.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Rais Kikwete na Balozi wa China waweka jiwe la msingi ujenzi wa Taasisi ya Moyo Muhimbili!!


Rais Jakaya Mrisho Kikwete(wanne kushoto) na Balozi wa China nchini Bwana Liu Xinsheng(watatu kushoto) wakiweka udongo katika jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa Taasisi ya tiba ya moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MNH leo asubuhi.Wengine katika picha ni Waziri wa Afya Profesa David Mwakyusa(watano kushoto) na kuli ni Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bwana Adolar Mapunda, wapili kushoto ni kiongozi wa ujumbe wa Jamhuri ya watu wa China Bwana Sun Liang (picha kwa hisani ya Freddy Maro).
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

flora salon ashusha mzigo mpya wa pasaka,wahi sasa

Hair do mbalimbali mbalimbali zinapatikana ndani ya Flora Salon
Baadhi ya mavasi ya harusi yaliyoingia hivi karibuni dukani kwa kwa Flora Salon



Mambo ya hair Do hayo


Ukiwa jijini Mwanza, kwa mahitaji yako mbalimbali ya Salon,Vipodozi vya aina mbalimbali,wigiz, bila kusahau mambo ya Bridal Shop ambapo unaweza kukodisha ama kununua vitu vyote vya harusi,Hasa kwa msimu huu wa sikukuu ya PASAKA,hakuna kwingine zaidi ya maduka ya FlORA PROMOTIONS yaliyopo mtaa wa Uhuru (Uhurus Street) jirani na hoteli ya Deluxe,nenda ukajionee sasa,uonekane mtu unaekwenda na wakati.

Kwa mawasiliano zaidi bofya namba hizi hapa chini na utajibiwa mara moja


o764 602676


0786 665555



Karibu FlORA PROMOTIONS,Karibu jijini Mwanza.


Pia ukitaka kujua zaidi ingia hapa FLORASALON


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

rais karume azindua Madarasa mapya skuli mbali mbali Pemba

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid karume,akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Madarasa mapya ya skuli ya Kengeja Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DkAmani Abeid Karume akisalimiana na wazee wa Kengeja wakati alipofika katika viwanja vya skuli ya kijiji hicho kwa madhumuni ya uwekaji wa jiwe la msngi pamoja na uzinduzi wa madarasa mapya leo
Wanafunzi wa skuli ya kengeja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume alipokuwa akizungumza nao huko katika viwanja vya skuli ya kengeja mapema leo.Picha kwa hisani ya Ramadhan Othman Pemba.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali akabidhi Ripoti za ukaguzi wa Matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake Kwa Rais Kikwete Ikulu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Ludovick Utouh akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ripoti za ukaguzi wa matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Kushoto ni Msaidizi wa mkaguzi mkuu Bwana Atanas Tarimo(Picha kwa hisani ya Freddy Maro)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

TANGAZO LA MSIBA

BOSCO SAFARI MOSHA WA GLASGOW,SCOTLAND.ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAKE MDOGO ABOUD NDESAMOKE MSOKE.KILICHOTOKEA HUKO DAR-ES-SALAAM TANZANIA.JANA MCHANA, MIPANGO YA MAZISHI YA NAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU TABATA.HABARI HIZI ZIWAFIKIE UKOO WA MSHA WA MAREKANI, FAMILIA YA DR MOSHA WA SAVANA-LA-MAR,UKOO WA MOSHA POPOTE PALE WALIPO .NAOMBA UNITUNDIKIE KWENYE BLOG YETU INAYOSOMWA POPOTE ULIMWENGUNI.NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU.
AKSANTE.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Mashujaa Musica kula pasaka ukonga- Magereza



Bendi mpya ya muziki wa dansi nchini MASHUJAA BAND, imewaandalia Burudani ya aina yake siku ya Sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa Bwalo la Magereza ambapo pia kutakuwa na Bonanza la aina yake litakaloshirikisha timu mbalimbali za maveterani kutoka mikoani.






Kwa mujibu wa Shaaban Mpalule msemaji wa bendi hiyo burudani itaanza saa tisa mchana ambapo nyimbo mbalimbali zitatumbuizwa ikiwa ni pamoja na kutambuylishwa nyimbo mpya inayotazamiwa kurekodiwa mara tu baada ya Sikukuu ya Pasaka ya Safari yenye Vikwazo mtunzi Jadol Fidifosi (FFU).


Aidha bendi hiyo siku ya leo ipo Woodland kwa jimmy Yombo, kesho itakuwa katika ukumbi wake wa nyumbani wa Mashujaa Pub, ijumaa itatelemka katika ukumbin wa Equatol Grill Temeke Mtoni, jumamosi itafanya onyesho tena katika ukumbi wa Woodland, jumapili itashuka kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Magereza Ukonga.




Katika Maonyesho hayo wanamuziki na Wacheza shoo wote nyota wa kundi hilo watakuwapo, ikiwa ni pamoja na Kiongozi wa bendi Aliston Angai, Despino Malaika, Geran Kissa, Masooud USB, Ngosha Mwanamasanja, Jado Fidifosi, Pasia Budansi, Raja Rado, na wengine wengi.Kwa upande wa Burudani ya Shoo bendi hiyo imezidi kung’ara zaidi kutokana na juhudi za Sharony Mapozi, Frida Mwanasuka, Sarafina Shotii,Pendo Bonzo, Merisa Maga, pamoja na Etoo TisaWengine ni mpiga gitaa, Amosi Ras, Baba , Flora Bambucha, Sarafina Shotii, Sharoni Mapozi, Neema Mkama, Pendo Boza, Frida Etoo Tisa, huku waimbaji wakiwemo Ibrahimu Milinda Nyeusi, Pasia Budansi Bakiza Mambo(Raja), Desipino Malaika, Masoud USB, Edward Anthony MaliKidogo(jadol Feed Force FFU)




Wengineo ni Mwanamuziki na rapper wa bendi SIMONG NGOSHA(ngosha masanja) Nyimbo zinazovuma kwa sasa ni ule wa Mwanike ulioimbwa kwa mchanganyiko wa makabila ya Kisukuma na Kihaya, ukiwa umetungwa na Ngosha Mwanamasanja na Moshi wa Sigara uliotungwa na mwanamuziki Pasia Budansi.Viingilio katika maonyesho yote ni vya kuridhisha ili kuwapa mwanya wote kwenda kushuhudia bendi hiyo mpya ya nyumbani inavyokuja kwa kasi katika medani ya muziki wa dansi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 1

sitoichukia nchi yangu tanzania,lakini kwa haya ntasema tu

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mateves iliyopo wilayani Arusha mkoani Arusha wakifanya mtihani wa majaribio wa nusu ya mwaka wakati wengine wakiwa wameketi chini kutokana na upungufu wa madarasa . Shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 910 ambao wanatumia madawati 320 tuuu katika madarasa hayo sasa hebu nambie upungufu uliopo. Piga picha hapo unambie wanasomaje hawa watoto wa A Town. Photo by Fredy Azzah
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 9

mnuso wa Easter Eve Bash in New England


Easter Eve Bash in New England

The African Nite is inviting you to join us on Saturday the 3rd for an Easter Eve Bash.
That African groove and best African mix vibes will be on all night long...
Enjoy the Bolingo, Bongo Flava, Taarab, Kwaito, Mapouka, Reggae, hip-hop and many more…
..
Location: Charlie’s Pub, 14 Cabot St, Lowell, MA, 01854
Door s Open: 8pm till 2am
Cover: $10
Cash BAR
Party will be hosted by DJ Paff, DJ Sam and as always many guest DJ’s
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, March 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

tbl yaimwagia mashindano ya kili taifa cup mili 850

Tuesday, March 30, 2010

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Tanzania Breweriers Limited (TBL)David Minja akiongea mbele ya wanahabari leo wakati kampuni hiyo ilipotangaza udhamini wa jumla ya milioni 850 kwa ajili ya mashindano ya Kili Taifa Cup yanayotarajiwa kuanza mei 8 aprili mwaka huu.


Davidi Minja amesema vituo sita vitatumika katika mashindano hayo ambavyo ni Arusha, Mtwara, Tanga, Iringa, Mwanza na Dodoma, robo fainali za mashindano hayo zitafanyika kuanzania aprili 22 na fainali zitafanyika aprili 30 mwaka 2010.


Wengine wanaoonekana katika picha kushoto ni Ferdrick Mwakalebela Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF na kulia ni George Kavishe Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambayo ndiyo inadhamini mashindano hayo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

karibu libenekeni Da'Jane


NAITWA JANE JOHN MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI NCHINI TBC .NIMEFUNGUA BLOG AMBAYO ni janejohn5.blogspot.com hivyo nawakaribisha watanzania wote kuangalia ili mjionee mambo mbalimbali ya michezo,burudani na mengine mengi ambayo yatakuelimisha. pia unawezea kutuma maoni.

KARIBU
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 2

maadhimisho ya upandaji miti kitaifa kufanyika shinyanga


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. EzekielMaige akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Town iliyoko mjiniShinyanga,wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Taifa ya kupanda Miti nchini ambayo kitaifa inafanyika mkoani Shinyanga, aliyeshika koleo ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Felician Kilahama na anaeangalia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo bw. Fabian Stanslaus .Siku hiyo huadhimishwa nchini Aprili Mosi ya Kila mwaka.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

taarifa kwa umma


Tarehe 17 Machi, 2010, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na hivyo Muswada huo kuwa Sheria Kamili. Muswada huo ulipitishwa tarehe 11 Machi 2010 katika Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hivi karibuni, Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alitoa madai kwamba kuna kifungu kidogo cha (3) ambacho kimeingizwa katika kifungu cha 7 cha Sheria hiyo isivyo halali au “kinyemela”. Kifungu kidogo cha 7(3) kinaweka masharti yanayohitaji uthibitisho wa wajumbe wanaounda Timu za Kampeni za Wagombea wa Kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani.



Mheshimiwa Dk. Slaa anadai kwamba kifungu cha 7(3) hakikuwepo kabisa kwenye Muswada wa Sheria uliojadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.Kwa kuzingatia madai ya Mheshimiwa Dk. Slaa, Vyombo vya Habari vimekuwa vikitoa maelezo mbalimbali kuhusu suala hili. Katika mazingira haya, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa Taarifa kwa Umma yenye lengo la kufafanua kile kilichotokea Bungeni hususan uandishi wa kifungu cha 7(3) katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi.



Kutokana na marekebisho yaliyopendekezwa na Wadau na Wabunge, Bunge liliagiza Muswada uchapishwe kwa mara ya pili. Baada ya Muswada huo kuchapishwa kwa mara ya pili, kifungu cha 7 hakikuwa na vifungu vya (1), (2) na (3). Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja zaidi zilizotolewa na Wabunge kuhusu makundi ya Sanaa na Viongozi wa Vyama wanaoweza kumsaidia Mgombea wakati wa Kampeni za Uchaguzi, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge) Mhe. Philip S.Marmo, iliandaa Jedwali la Marekebisho ambalo lilifanya marekebisho katika kifungu cha 7.



Marekebisho hayo ni:(a) kukitaja kifungu cha 7 kilichokuwepo kuwa kifungu kidogo cha (1) katika kifungu hicho hicho cha 7.(b) kuongeza kifungu kidogo cha (2) ili kuongeza makundi ya sanaa na kundi la watu wanaoweza kufadhiliwa na Mgombea kwa chakula, vinywaji, malazi na usafiri wakati wa Kampeni za Uchaguzi.



Kwa kuwa uamuzi huu ulifanyika wakati wa Kamati ya Bunge Zima, Mwenyekiti aliagiza kwamba suala hilo la kuweka marekebisho hayo, lizingatiwe wakati wa kutoa tafsiri ya maneno “timu ya kampeni”. Kwa kuzingatia mapendekezo ya Mhe. William H. Shellukindo kwamba idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu. Katika kutekeleza hayo, kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati “Timu ya Kampeni” iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika.



Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya “Timu ya Kampeni” ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika “Timu ya Kampeni”.



Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa, kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge.Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. Katika hatua hii, Wabunge wanaweza, kupitia Kanuni ya 86(II) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, kupendekeza mabadiliko katika Muswada.



Endapo Waziri ataafiki mapendekezo ya Mbunge yeyote,atamjulisha Mwenyekiti na Mwenyekiti akiridhia atamuelekeza Mbunge aliyetoa mapendekezo asome maelezo anayotaka yaingizwe kwenye Muswada. Ikiwa Mbunge aliyependekeza marekebisho hayo hana maelezo mahsusi, Mwenyekiti atamuagiza Katibu wa Bunge ashirikiane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka maneno au Kifungu kinachoweka masharti yenye maudhui aliyopendekeza Mbunge.
Mwenyekiti atawahoji Wabunge kama mapendekezo yakubaliwe au la, wakikubali basi waandishi watakwenda kuandika kifungu kwa namna ambayo inatafsiri nia na uamuzi wa Bunge.Kwa kuzingatia maelezo haya kuhusu hoja za Wabunge ninaridhika kuwa kifungu cha 7(3) cha Sheria ya Uchaguzi kimezingatia matakwa na maagizo ya Bunge sawa sawa.



Kifungu hicho hakikuingizwa kwenye Sheria “kinyemela” au kwa hila. Aidha, mtiririko wa mamlaka za kuthibitisha Timu ya kampeni una mantiki sahihi yenye lengo zuri la kufanikisha shughuli za uchaguzi kwa ufanisi.


Imetolewa na

OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

29 Machi, 2010
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 1

wafanyakazi wanawake tbc 1 waanzisha chama chao

Mwenyekiti wa UWAMA Angela Msangi akimuandaa mgemi rasmi Mhariri Mkuu wa TBC 1 ASUMPTA MASOI
Mc WA SHEREHE YA UZINDUZI WA CHAMA CHA WANWAKE TBC UWAMA- RAHELI MHANDO akitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa uwama ANGELA MSANGI akiwa sambamba na mgeni rasmi ASUMPTA MASOI Mharriri Mkuu wa TBC 1
Mgeni rasmi akiwa na mdau wa Jambo Tanzania MAGRETH CHAMBIRI
WANACHAMA WA CHAMA CHA KUSAIDIANA WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASMI MHARIRI MKUU ASUMPTA MASOI kwenye uzinduzi wa chama hicho
Hapo ni wadau wengine wa TBC 1 ESHE MWIDINI na ZUENA MSUYA
wadau wa tbc one ambao ni wanachama wa chama cha kusaidiana UWAMA kutoka kushoto ni AGNES MBAPU,ETI KUSILUKA na LOUISA MTOPWA Wadau wengine Martina na Levina
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 2

stooopppppp.!

Askari wa usalama barabarani kituo cha Migori Mtera katika wilaya ya Iringa vijijini aliyefahamika kwa jina moja ya Peter akiwa amekamata piki piki ambayo ilikuwa imevunja sheria za usalama barabarani kwa kupakizana zaidi ya abiria wawili huku wakiwa hawajavaa kofia ya kuzuia michubuko iwapo watapata ajali , madereva wengi wa piki piki katika eneo hilo wamekuwa wakiendesha bila leseni wala kuvaa kofia kwa madai kuwa chombo hicho ni mali yao haina haja na kuwa na leseni na kuwa wanaweza kupakizana idadi yoyote.Picha hii kwa hisani ya Francis Godwin
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 2

mama salma kikwete ziarani mkoani mara

Mkurugenzi Mkuu wa Singita Grumeti Reserves Bwana Graham Ledger,kulia, akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kazi za taasisi ya WAMA. Makabidhiano hayo yalifanyika katika hoteli ya Grumeti iliyoko katika hifadhi ya Serengeti .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia mamia ya wananchi wa kijiji cha Nyamuswa, wilayani Bunda mkoani Mara, wakati akielekea mjini Bunda kukagua shughuli mbalimbali za akinamama wajasiriamali wilayani humo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 4

waziri mkuu pinda ziarani vietnam

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride la heshima
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea maua kutoka kwa mtoto wa Vietnam wakati alipopokelewa rasmi kwenye viwanja vya Ikulu ya Hanoi , Machi 29, 2010 kuanza ziara yake ya kikazi nchini Vietnam. Kulia ni mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Vietnam, Nguyen Tan Dung.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

TANGAZO LA SHEREHE ZA PASAKA UINGEREZA, MILTON KEYNES


FLEX ENTERTAINMENT


in conjunction with


IBRA HAKUNA MATATA


Proudly Presents:

EASTER BASH PARTY WITH T.I.D LIVE ON STAGE on Saturday 3rd April
@The Beacon,Mount Farm, Bond Avenue, Bletchley, Milton Keynes, MK1 1PA.
From 9pm-6am, Dress Code: Smart, Casual, No hats or hoods, Trainers ok (ROER Right of entry reserved). Entry £15 ALL NIGHT

With Djz Leeboy Flex, Dj Yusuf & Guests.

Music Policy: R&B, Hiphop, Reggae, Dancehall, Old Skool (Soul & New Jack swing) & Afro Beatz (Bongo flava's, Lingala, Zouk, Soca & Rhumba)

Also "BBQ AKA NYAMA CHOMA (GOAT,RIBS, CHICKEN WINGS & SOUP) BY IBRA HAKUNA MATATA & FLEX SPECIAL WILL BE ON SALE ALL NIGHT" WITH LAUNCH OF SUNDAY FAMILY DAYS BBQ & CHILL OUT NIGHTS EVERY SUNDAY THEREAFTER FROM SUNDAY 11th APRIL 2010

"WE GUARANTEE TO GIVE YOU EVERY SIXTY SECONDS OF HAPPINESS FULL STOP" PASS IT ON & STAY BLESSED
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

msikilize ismail na mwasiti na wimbo wao wa baby girl

Monday, March 29, 2010
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

SEMBENE AWARD ZIFF 2010


Ousmane Sembene Award at ZIFF 2010

The Deutsche Gesellschaft fuer Technische Zusammenarbeit GmbH (GTZ) in cooperation with ZIFF will be awarding the Ousmane Sembene Films for Development Award for the third time in July 2010. The prize will be awarded to films that take a particular look at topics such as HIV/AIDS, gender, education or poverty. It carries prize money of US$ 5000 and is designed towards enhancing creativity in African film production.

Entry is open to documentary and feature films of at least 20 minutes. The final selection will be made by ZIFF and an international jury. Filmmakers can compete for this award if they are nationals or permanent residents of an African country.

The submission deadline is 30th April 2010 please use the general entry form at www.ziff.or.tz

Tuzo ya Ousmane Sembene katika ZIFF 2010.

Mshindi kupata kitita cha Dola 5,000/=

Shirika la GTZ likishirikiana na Tamasha la nchi za Jahazi (ZIFF) kwa mara ya tatu tena mwaka huu 2010 watatoa tuzo ya Filamu ya Ousmane Sembene, tuzo hii italenga hasa katika filamu fupi ambazo hazijazidi dakika 20 na ambazo zitakua zimezungumzia au kugusia masuala yanayoikabili jamii ya kitanzania hasa katika mambo ya Ukimwi, Jinsia, Elimu na umasikini.

Mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 5,000 taslimu papo hapo kwaajili ya kumsaidia katika kutengeneza filamu nyingine ama kuboresha kazi zake.

Wale wote watakaotaka kushiriki katika tuzo hii wawasilishe filamu zao kabla ya tarehe 30/04/2010 kwa kujaza fomu za kawaida zinazopatikana katika tovuti yetu www.ziff.or.tz

Daniel Nyalusi

Events and Film Program Coordinator

Zanzibar International Film Festival
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 29, 2010 | | Permalink | Maoni 3

karibu mdau libenekeni


Mimi ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha redio cha 87.8 Ebony fm cha Iringa lakini mimi niko Dar-Mini Studio, naitwa Renatus Kiluvia,ni mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa blog yako,naomba msaada wako wa kunitangazia blog yangu mpya www.muzikinamaisha.blogspot.com blog yangu inahusu muziki na maisha katika nyanja tofauti-tofauti,pia itahusika kuzungumzia burudani zingine kama filamu n.k.
Akhsante!!!!!!!!!!!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 29, 2010 | | Permalink | Maoni 13

mwakilishi wa unicef aaga ikulu zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DK Amani Abeid Karume,akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Heimo Laakkomen,aliyekuja kumuaga Rais,Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya kumaliza muda wake wakazi Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DK Amani Abeid Karume,akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Heimo Laakkomen,aliyekuja kumuaga Rais,Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DK Amani Abeid Karume,akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Heimo Laakkomen,aliyekuja kumuaga Rais,Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya kumaliza muda wake wakazi Nchini.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.Zanzibar
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

haya wana hip hop bongo somo hilo kutoka kwa mdau


Ndani ya Jiachie leo King Kif kutoka www.kingkif.blogspot.com najiachia na madude ya muziki wa Hip-Hop ambao hapo zamani hapa Bongo tuliuita muziki wa kufokafoka , hiyo ilikuwa mwishoni mwa miaka ya themanini na tisini mwanzanzoni.Basi bwana, hapa kwanza kabisa kunahitajika kufahamu nini maana ya sayansi na nini maana ya Philosophy.

Science means a techinique to simplify work which includes branches such as mathematics anda Geography.

SAYANSI NA HIP-HOP

Sayansi na Hip-Hop ; Hip-Hop ni lazima iandikwe kwa kutumia mizani , hii ina maana lazima uwe na idadi maalum ya mizania katika mistari ili mashairi yako yaweze kuimbika(kuchanika).


Pia beats (midundo) ya Hip-Hop lazima igonge katika mahesabu maalum ambayo kwa Hip-Hop ni 4 (four) , hivyo hata mistari inahimizwa kuangukia kwenye hesabu hiyo hiyo ya vigawe vya 4(nue) yaani 4,8,12 na kuendelea .


Hapo tunaona wazi hesabu inavyotawala katika uhunzi mzima wa mashairi na beats(midundo) ili kufanya ama kujenga kitu kinachoitwa HipHop.

PHILOSOPHY

Means love anda wisdom (hekima na upendo ) , ni neno (lenye asili ya Kigiriki). Philo means love and Sophia means Wisdom.

Philosophy na Hip-Hop ; ni wazi kabia na haipingiki kwamba muziki huo unaleta upendo ikiwa ni pamoja na kutumika njia ya kuleta ama kudai haki , kukemea unyonjaji katika jamii na kadhalika.

Aidha, mistari ama mashairi bora ni yale yaliyo na hekima yasikilizwapo katika masiko ya watu na si vinginevyo , mfano ni mistari inayopatikana kwenye traki kali iitwayo " I know i can" ya Nas . Traki hii ina maneno ya hekima na upendo ndani yake juu ya maisha kuanzia utoto hadi utu uzima.

MIFANO MINGINE DHAHIRI

Hii hapa mifano mingine kadhaa ya watu ama niandike maemsii walioweza kujiita Hip-Hop mathematic ambao ni kama vile RZA ambaye ni kiongozi wa kundi mahiri la Wu Tang Clan , yupo Cani-Bus , yupo Mos Def .Pia yupo jamaa mmoja aitwaye Keith Muray wa kundi la DEF Squad na wengine wengi .


King kif kutoka www.kingkif.blogspot.com namaliza hapa huku nikisisitiza Hip-Hop bila Science $ Philoph ni pumba tupu na hata mashabiki hasa hapa Tanzania waufuatilie kwa undani muziki huu na waache ushabiki mandazi.


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 29, 2010 | | Permalink | Maoni 5

3 Door Pajero 2800 Turbo Automatic inauzwa

Front
Back
Front Left Side
Driver's Seat

Colour Blue,
Engene 4 slinder Tube,
Contact:
Ibrahim Mitawi
0713 300997, 0773 300997, 0783 300997

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 29, 2010 | | Permalink | Maoni 2

hepi bethidei to you da' Foibe

Sunday, March 28, 2010
Wadau wakiserebuka baada ya kula na kunywa usiku huu kwenye hafla fupi ya kuzaliwa ya Da' Foibe iliofanyika Mikocheni jijini Dar usiku huu na kuhudhuriwa na watu mbalimbali
Jikeki safi kabisa,Da' Shamim upoo!
Mdau wa Mtaa kwa Mtaa (kijani) akitoa neno la shukurani kwa kualikwa kwenye mnuso huo wa kiana
Da' Foibe ambaye anazaliwa leo akitimiza miaka yake 26, akikata keki huku akiimbiwa ule wimbo maarufu kabisa ambao huwa ni maalumu kwa shughuli kama hii
Flowerz wa ukweli wakishoo love kwa pamoja usiku huu
Wadau wakishoo love kwenye hafla fupi ya Da'Foibe
Da'Foibe akiwa ameketi na wageni waalikwa kwenye sherehe yake ya kuzaliwa usiku huu,Foibe amekiri kuwa anatimiza miaka yake 26,Kwa hilo anamshukuru Mungu na anamuomba zaidi amuongezee afya njema ili miaka yake iongezeke ana asherehekee tena siku yake ya kuzaliwa miaka kadhaa ijayo
Cheerzzz
Kila mmoja alihakikishiwa anapata kinywaji hiki
"Mmmh..! hiki kilevi chake sio kikali wang"! Wamiminie hivyo hivyo wachangamke

Mdau akininimininia kinywaji,da nakiona kama kiko safi hivi kwa kuchangamsha mwili,ng0ja nijaribu kunywa nione utamu wake ukoje
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, March 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu