MWILI WA HAYATI MZEE RASHID KAWAWA KUAGWA KESHO viwanja vya KARIMJEE!!

Thursday, December 31, 2009


Mwili wa Hayati Mzee Rashid Mfaume Kwawa unatarajiwa kuagwa kwenye ukumbi wa Karimjee kesho ambapo viongozi na wananchi mbalimbali watapata nafasi ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa keshokutwa Jumamosi nyumbani kwake Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaaam.


Akizungumzana wandishi wa habari jioni hii Naibu Katibu mkuu kiongozi wa Ikulu Mh George Yambesi amesema viongozi pamoja na watu mbalimbali ndugu na Jamaa wataanza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kuanzia saa nane mchana kabla ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake Madale hiyo Jumamosi

Mwili wa hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Jeshi la Wananchi Lugalo, hayati Mzee Rashid Kawawa amefariki leo asubuhi kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

nawatakia heri na fanaka ya mwaka mpya Wadau

Kimsingi yamesalia masaa machache katika kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka 2010 kwa furaha kabisa,ama kwa hakika ni vyema tukamshukuru Mungu kwa kila jambo kwa wale ambao yeye atawachagua kuingia mwaka 2010 wakiwa wenye afya njema ama kwa namna yoyote ile ali mradi mwaka mpya umeuona.Wadau tusiachane wapweke na wanajamvini wengine pia katika suala zima la kutumiana picha wakati wa kuuaga mwaka na kuukaribisha pia,ruksa kutuma picha mbalimbali za matukio maalumu za usiku wa leo na hata kesho nami ntazirusha bila hiyana humu bloguni.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

pati ya aina yake kufanyika usiku wa leo ndani ya hoteli sea cliff

Pichani ni sehemu ya maandalizi ya pati hiyo yanayoendelea hivi sasa hapa kwenye fukwe ya hoteli ya kitalii ya Sea Cliff,jijini Dar.


Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia chapa yake ya CAMEL imeandaa hafla kwa wanachama wake na wageni waalikwa kwa ajili kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2010,itakayofanyika leo usiku kwenye hoteli ya kitalii ya Sea Cliff jijini Dar.

Hafla hiyo ambayo imepewa jina la "Red carpet event 2010" itakuwa na mambo mbali mbali kwa wageni waalikwa ikiwemo mambo ya Fire works,Internal buffet,Live band pamoja na zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa na wadhamini wa hafla hiyo itakayokuwa ya aina yake.

Aidha wadhamini wengine wa hafla hiyo ni kampuni ya simu ya za mikononi ya Zain,kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji chake cha Ndovu pamoja na Pepsi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

rais karume atoa salamu za mwaka mpya kwa wananchi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akitoa salamu za mwaka mpya wa 2010,kwa wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar,na kuwatakia Kheri ya Mwaka mpya amani na utulivu katika maisha yao,huko Ikulu Mjini Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi AL haj Dk Amani Abeid Karume, akizungumza na mashekhe na viongozi wa Dini mbali mbali wa mikoa mitano ya Ungja na Pemba,ikulu Mjini Zanzibar leo.
Picha na Ramadhan Othman Ikulu,Zanzibar
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 1

masikini kibajaji



Hii nimekutana nayo jii hii msasani wakati narejea kuwacheki washkaji kule mjengoni Clouds Fm,kibajaji nimekikuta kimepigwa dafrau na kama ukionavyo kiko chali kabisa,sasa sijui kilikuwa na abiria ama la na wametoka salama?,kwa sababu nilikuwa kwenye mchuma nimepewa lift tu hivyo sikuweza kusimama angalau kujua mengineyo,Lakini kikubwa Madereva lazima wawe makini wakiwa barabarani wakiendesha ili kuepuka ajali ambazo si za lazima kila mara na kila wakati
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

shindano la maisha plus kuanza kurindima leo usiku

Pichani ni waratibu wa shindano la Maisha Plus linaloanza kurindima leo kijijini usiku na kurushwa live na televisheni ya Taita TBC One.Kulia ni Francis Bonda,Masoud Kipanya pamoja na David walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kuhisiana na utambulisho rasmi wa washiriki wa Maisha Plus kuingia kijijini


Pichani ni baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus wakiwa ndani ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya City Style Sinza jijini Dar walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya utambulisho wao wa kuingia kijijini rasmi leo usiku



MAISHA PLUS 2010
Msimu wa pili wa maisha ya kijiji cha plus unatarajiwa kuanza rasmi usiku wa
mkesha wa mwaka mpya kwa fainali zitakazopelekea washiriki 18 kuingia kijijini
kuianza safari ya siku zisizopungua 56.


Msimu huu ulioanza kwa usaili katika maeneo 13 ya tanzania bara na visiwani,
ulianza mwezi wa nane kwa kuchagua washiriki kumi bora ya kila mkoa kutoka
katika maelfu ya washiriki waliojitokeza.


Baada ya washiriki kumi kuchaguliwa na waandaaji, majina hayo kumi
yalipelekwa kwa watazamaji ambao walipiga kura kuchagua 3 bora ya kila mkoa.
Jumla ya washiriki walioingia tatu bora za maeneo yote ni 42 ambapo tanga ilitoa
washiriki wawili badala ya watatu kutokana na matatizo binafsi ya mshiriki
mmoja. Zanzibar imetoa washiriki wanne badala ya watatu kutokana na kupewa
heshima ya kutoa mshindi wa msimu wa kwanza.

Dar es salaam nayo imetoa washiriki 6 kutokana na kuunganishwa na mkoa wa
pwani. Maisha rasmi ya kijijini yanatarajiwa kuanza asubuhi ya tarehe 1 januari
2010 na kumalizika mwishoni mwa mwezi wa pili 2010.


Marafiki wema waliosaidia msimu wa pili wa maisha plus ni city style hotel
iliyoko sinza, infinity communications na aurora.

Baadhi ya watazamaji waliokuwa wakituma meseji kupigia kura washiriki katika
hatua mbalimbali wamebahatika kupata zawadi mbalimbali ikiwemo ya
kushuhudia live fainali zitakazofanyika kijijini usiku wa tar 31 desemba 2010.
Zawadi nyingine ni pamoja na vikombe na mafulana ya maisha plus
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA KUzichapa kesho uwanja wa uhuru

Mabondia Rashid Matumla (Snake Man) kulia na Joseph Marwa na (Smart Man) wakitunishiana misuli wakati walipokuwa wakitambiana baada ya kupima uzito kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo asubuhi mara baada ya kuongea na waandishi wa habari juu ya mpambano wao unaotarajiwa kupigwa kesho kwenye uwanja wa Uhuri jijini Dar es salaam.

Joseph marwa ana kilo 87 wakati Rashid matumla ana kilo 86 na pambano lao litakuwa la uzito wa 86 na litakuwa la Raundi 10 na Rashid Matumla ameshawahi kuchukua mataji ya IBU,WBU na WBA wakati Joseph Marwa amewahi kuchukua mataji ya PABA na UBO , kiingilio katika mapambo hayo kitakuwa kati ya 3000. 5000 na 10.000 waote mnakaribishwa ili kujionea masumbwi hayo maziito.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

KAPUMZIKE KWA AMANI MZEE WETU KAWAWA


RAIS JAKAYA KIKWETE AMETANGZA RASMI LEO KUHUSU KIFO CHA SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA MAPEMA ASUBUHI IKULU, JIJINI DAR. RAIS JK AMETANGAZA PIA SIKU SABA ZA MAOMBOLEZO KITAIFA AMBAPO BENDERA ZITAPEPEA NUSU MLINGOTI NCHI NZIMA. MAANDALIZI YA MAZIKO YANAENDELEA NA JK KAOMBA SUBIRA NA ITATANGAZWA WAKATI WOWOTE MAMBO YAKISHAKAMILIKA.MZEE KAWAWA AMEFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 80.

PICHANI CHINI NI RAIS JAKAYA KIKWETE NA MKEWE WALIPOKWENDA KUMJULIA HALI MZEE KAWAWA JANA JIONI KWENYE CHUMBA CHA WAGONJWA MAHUTUTI,HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ALIPOLEKWA KWA AJILI YA UCHNGUZI WA AFYA YAKE AMBAYE ILIBADILIKA GHAFLA.


MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI -AMEN

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

hali ya mzee kawawa inaendelea vizuri

Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jana jioni. Kulia ni profesa Victor Mwafongo. Mzee Kawawa alipelekwa hapo Muhimbili baada ya kujisikia vibaya na kupelekwa hapo kwa kuangaliwa. Vipimo vinaendelea kujua anasumbuliwa na nini na hali yake kwa sasa inaendelea vizuri. Picha na Freddy Maro wa Ikulu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 31, 2009 | | Permalink | Maoni 2

ama kwa hakika safari bado ni ndefu sana wanajamvini

Wednesday, December 30, 2009
Wanafunzi wa shule ya Msingi Juhudi iliyopo Wilaya ya Kigoma Vijijini mkoani Kigoma nchini Tanzania wakiwa darasani.hii inaonyesha ni kiasi gani hali ni mbaya katika maeneo mengi ya vijijini,viongozi husika mnaliona hili lakini??picha kwa hisani ya Mch. Emmanuel Bwatta wa Kanisa la Anglikana Kigoma
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 15

cheka kimya kimya.!



 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

beef la wasanii hawa linawafundisha nini wasanii wenzao ?

Wakazi
Beezy

Wasanii nyota wa kizazi kipya, Wakazi na Beezy, wamekuwa na mkwaruzano wa kimuziki hivi karibuni na inasemekana chanzo cha malumbano hayo ni ugomvi uliopita kati ya producer Marco Chali na Beezy.

Inasemekana Beezy alimpa Marco Chali kitita cha fedha tasilimu cha shillingi milioni moja ya kitanzania kwaajili ya kazi za muziki kati yao wakati Beezy akiwa nchini Ujerumani. According to Beezy, Marco Chali hakutekeleza wajibu wake baada ya kupokea huo mkwanja na hicho ndicho kilikuwa chanzo cha Beezy kumsema katika wimbo wake wa “My people”.

Wakazi amejiingiza katika mtafaruku huo kutokana na uhusiano wake na Marco Chali. Yeye na producer huyo ni marafiki tangu wakiwa wadogo na pia kabla hajaondoka kuelekea masomoni nchini Marekani walikuwa wameanza kufanya kazi za kisanii pamoja.

Wakazi alitoa video ambayo akawa anaongea na kuwahamasisha watu kutomuunga mkono Beezy juu ya swala hilo akidai kuwa jamaa anasema hivyo ili apate umaarufu kwa kupitia mgongo wa huyo prodyuza.
Wapo waliodai Wakazi nae anatafuta umaarufu kupita mgongo wa Beezy ila cha msingi ni kwamba, Vita ya maneno imeanza na ni juu ya mashabiki kuamua nani zaidi au nani yupo sawa.

Zifuatazo ni link ya majibishano hayo:
Wakazi - dissin Beezy

Beezy – Last Words to Marco Chali & Wakazi

Wakazi – Blazed (reply to Beezy)

Wakazi – Blazed 2 (48 hours later)
http://www.youtube.com/watch?v=LFfejqAs6Jg
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 6

rais jakaya kikwete atoa salamu za pole kwa wakuu wa mikoa


Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametuma salamu za pole kwa wakuu wa mikoa minne ambayo imekumbwa na maafa yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Aidha, Rais Kikwete amepongeza jitihada zinazofanywa na uongozi katika mikoa hiyo kukabiliana na maafa yanayosababishwa na mvua hizo.


Rais Kikwete ametuma salamu hizo za pole leo (jana) Jumanne, Desemba 29, 2009, kwa wakuu wa Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Ruvuma na Rukwa.


Katika mikoa hiyo, baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na mafuriko, wengine wamejeruhiwa kutokana na radi, na kumekuwepo na upotevu wa mali, na mamia ya watu kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo ulioambatana na mvua kubwa.

Katika salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Dkt. James Alex Msekela, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Luteni Kanali (mst) Issa Saleh Machibya, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Christine G Ishengoma, na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay, Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na upotevu wa maisha, upotevu wa mali na hasara ya watu kuezuliwa nyumba zao.

“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa ambayo yameambatana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Mkoa wako. Nakupa salamu za pole wewe binafsi Mkuu wa Mkoa, na kupitia kwako, natoa mkono wa pole kwa watu wote waliopatwa na maafa kutokana na mvua hizo,” amesema Rais Kikwete katika sehemu ya salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali Machibya.
Rais ametuma salamu zenye ujumbe kama huo kwa Mhandisi Dkt. Msekela, Mheshimiwa Ishengoma na Mheshimiwa Njoolay.


Katika Wilaya ya Kongwa ya Mkoa wa Dodoma watu 220 hawana mahali pa kuishi wakati idadi ya wasiokuwa na mahali pa kuishi katika Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro imefikia 2, 152 kufuatia nyumba zao kuezuliwa ama kuharibiwa na upepo ama mafuriko. Katika wilaya hiyo hiyo ya Kilosa, nyumba 922 zimefurika maji.

Katika Mkoa wa Rukwa, watu 27 wamelazwa katika Kituo cha Afya cha Kakese baada ya kuwa wamepigwa na radi katika tukio ambako mtu mmoja amepoteza maisha.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amewaelekeza wakuu hao wa mikoa kuendelea kuchukua hatua za dharura kukabiliana na maafa yanayotokana na mvua hizo na kuahidi kuwa Serikali yake iko pamoja na wananchi waliopatwa na maafa katika mikoa hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Desemba, 2009
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

TANZANIA, ZAMBIA NA CHINA ZATILIANA SAINI MKATABA WA KUIMARISHA RELI YA TAZARA


Joseph Ishengoma

MAELEZO


Tanzania, Zambia na China kwa pamoja zimetiliana saini mkataba wa kuifufua reli ya TAZARA wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 39. Mkataba huo wenye lengo la kuikwamua reli ya TAZARA umesainiwa hivi karibuni nchini China . Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo jijini Dar Es Salaam , Waziri wa Miundombinu Dr. Shukuru Kawambwa ameeleza kuwa mkataba huo utajumuisha ukarabati na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya usafirishaji vikiwemo vichwa vya traini na mabehewa.

“Fedha hizo tutakazolipa taratibu zitatumika kununulia vichwa sita vya traini, mabehewa sita na kukarabati mabehewa 1,200 yaliyochakaa,” amesema na kuongeza kuwa katika mazungumzo hayo pande hizo tatu (china, Tanzania na Zambia ) zimekubaliana kufanya kazi kwa pamoja kuinua hadhi ya erli hiyo. Pande hizo pia zimekubaliana kupata punguzo la ujenzi wa reli ambayo hata hivyo hakuifafanua zaidi ni kiasi gain cha punguzo hilo .


Amesema, “tumekubaliana kwa pamoja kuhakikisha reli ya TAZARA inarudia katika hali yake. Kuanzia sasa wataalam wataanza kufanya tathmini na kuchambua kitugani kifanyike ili abiria na mizigo inayopitia reli ya TAZARA isafirishwe kwa ufanisi wa hali ya juu.” Reli ya TAZARA inayounganisha Tanzania na Zambia ilijengwa mwanzoni mwa miaka ya 1970 baada ya Tanzania na Zambia kukopeshwa dola za kimarekani milioni 500 na serikali ya Jamhuri ya watu wa China.

Deni la fedha hizo bado linaendelea kulipwa taratibu hadi sasa. Wakati wa utiliaji saini mkataba huo, Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Miundombinu (Mhe. Shukuru Kawambwa), Waziri wa Fedha na Uchumi (Mhe.Mustafa Mkulo), Waziri wa Viwanda, Biashara na na Masoko (Dr. Mary Nagu) na naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Seif Idd. Zambia kwa upande wake iliwakilishwa na mawaziri wawili.

Waziri wa Uchukuzi na Waziri wa Fedha. Kwa mujibu wa Waziri Kawambwa , Zambia inataka TAZARA iimerishwe zaidi kutokana na reli hiyo kuwa tegemeo katika usafiri na usafirishaji wa madini ya Copper. Zambia inampango wa kuongeza uzalishaji wa madini ya copper kwa wingi na reli ya TAZARA ndiyoinayotegemewa kusafirisha madini hayo hadi katika bandari ya Dar Es Salaam .
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Tanzanian women dying for white skin


THE zeal to look beautiful and a colonial mentality that white skin is superior is fast driving Tanzanian women into their graves as they risk their lives by using skin lightening creams that in the end turn lethal.The problem is not only confined to Tanzania as selling of whitening creams is a lucrative business in Africa worth millions of US dollars a year.


In some countries that allow the use of these lethal substances, shelves in pharmacies are stacked high with lotions, creams and soaps all promising to make women whiter and supposedly more beautiful.But, in countries like Tanzania, where the use and importation of skin lightening creams is banned, the business is thriving as these dangerous creams are smuggled into the country while dealers on the other hand are discrete. Read the rest of this entry »
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

toto tundu anataka kuslide

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

shangilia taifa stars ishinde dhidi ya Ivory Coast.

Hii ni kampeni ya kuhamashisha Umma wa watanzania kwenda kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania wakati watakapopambana na Timu ya Taifa ya Cote d' Ivoire (Ivory Coast) mechi itakayofanyika tarehe 4 Januari 2010.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

precision air yatoa msaada kwa yatima kituo cha cornel ngaleku, moshi



Watoto wa kituo cha kulelea yatima wa Cornel Ngaleku Children Centre (CNCC) wakicheza na mfanyakazi wa Precision Air, Nia Mbaga mjini Moshi, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho kutoa msaada wa chakula kwa Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya wikiendi. Precision Air inaasili watoto wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kutekeleza programu ya huduma zake kwa jamii.
Wafanyakazi wa Precision Air wakikabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali kwa Mtawa Catherine, anayetunza watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Cornel Ngaleku Children Centre (CNCC) mjini Moshi wikiendi. Precision Air inaasili watoto wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kutekeleza programu ya huduma zake kwa jamii.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

semina ya biashara na ujasiriamali arusha


HABARI! NINA KUKARIBISHA KATIKA SEMINA YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI ITAKAYOFANYIKA IKWETA HOTEL ARUSHA MJINI SIKU YA JUMAMOSI SAA 9 MCHANA. KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0719 886 193
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
KARIBU KWENYE FURSA YA BIASHARA JE wewe ni mwajiriwa au sio mwajiriwa nani tegemezi wa KIPATO chako? JE unayo familia na wewe ndiyo kiungo cha kuendesha familia?JE una watoto,ndugu na marafiki wanaokutegemea?Ikitokea bahati mbaya ukawa kilema wa maisha au Mungu amekuchukua,
JE familia yako na watoto wako watalipwa na ofisi yako maisha yao yote?JE, ungependa uwaache wapo kwenye shida nakuomba misaada kwa marafiki zako?JE wewe ni mmoja kati ya watu wanaosumbuliwa na KIPATO? Au unafikiria kuwa na NYUMBA NZURI, GARI ZURI, AMANI, au KUSOMESHA WATOTO?
JE unafahamu kuwa watu wengi wanamaisha duni kwa sababu tu hawana MTAZAMO sahihi wa maisha?JE unafahamu familia ngapi ambazo zinaishi kwa taabu sababu tu kiungo cha familia hiyo ambacho kilikuwa chanzo cha mkate wa siku Mungu amekipumzisha mahali pema peponi?
JE una ndoto(Malengo) yoyote mwaka huu? Imekamilika au ipo mbali kukamilika? Umepanga chakufanya?Umefika wakati wakabadili mfumo(mawazo mgando) wetu wakufikiri na tutumie muda wetu kwa manufaa yetu wenyewe.
Karibu kwenye semina ya Bure itakayokupa fursa nyingine mbadala kwa kutumia muda wako wa ziada uweze kufikisha malengo yako uliyojipangia.
MAHALI: DSM, ELITE CITY BUILDING 2nd Floor. ARUSHA ,BLUE ROCK HOUSE MKABALA NA GOLDEN ROSE,MWANZA PPF PLAZA SECOND FLOOR .DODOMA UKUMBI WA VETA,MBEYA FOREST HILL HOTEL ,IRINGA –KIHESA KICHANGANI STUDENT CENTRE
MUDA: SAA 9:00 ALASIRI
SIKU: JUMAMOSI NA JUMAPILIKWA WAKAZI WA ARUSHA WIKI HII TUPO IKWETA HOTEL KARIBU SANA
Mawasiliano:- 0719 886 193
JACKIE
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

kamuzi la mdau la culinary chamber kuzinduliwa mwaka mpya

mambo ya kuchonga chonga pia
yatakuwepo ktk blog ya culinary chamber
Nikiwa na chef Leonard senior lecture wa culinary manchester metropolitan univeristy
usiku baada ya mashindano ilikua ni bonge la party na bendera za nchi washiriki zote zilipandishwa. Cheki bendera yetu inavyowaka.


Wajina, blog yetu ya CULINARY CHAMBER itazaliwa rasmi tar 1/1/2010. Hivi sasa article za awali zinamaliziwa pamoja na picha baadhi. Imani yangu ni kuwa wataalamu wa fani hii watachangia kwa moyo mmoja ili wadau wote wapenda misosi waweze kufaidika kwa utaalamu wa mapishi mbali mbali yatakayoporomoshwa.
Nnaimani ushirikiano utakua mzuri ili tuboreshe blog yetu. Mwanzo mgumu ila penye nia pana njia tutafika tu kwa juhudi na uchakarikaji.Pokea picha hizo ambazo nilibahatika kushiriki pia mashindano ya finger foods ambayo lengo haikua kupata mshindi ila ni kubadilishana ujuzi toka kwenye vyuo mbali mbali vya culinary duniani vyenye ushirikiano wa pamoja toka nchi za Croatia, USA, Uk, France, Italy, Malaysia , Indonesia, India, Korea, China, Singapole, German, Austria, Swistzerland, Netherland, spain na Belgium.

Picha za vyakula na habari zaidi watazipata ktk blog ya Culinary Chamber.
Baada ya mashindano hayo jioni ilikua ni bonge la party wanafunzi waliochukua kozi ya general hotel management na mambo ya matukio walitoa perfomance safi yenye ladha ya mataifa yao ilikua super sana ankal michuzi.
Ila kubwa kuliko yote ni pale nilipooona bendera ya taifa langu imepanda juu kama heshima ya mshiriki toka Tanzania. ohhhhhh.... nilihisi machozi kunidondoka kwa furaha.Ndugu zangu nawaomba sana sana tushirikiane.


Shule hii ni bure wala hakuna gharama yeyote kwa hiyo yeyote mwenye ujuzi atoe, msijifiche. Huu ndio wakati muafaka wa kubadilishana utaalamu kwani hakuna anaejua zaidi. Wote tunajua kiasi kwa hiyo tukichanganya maarifa inakua safi mambo yanakamilika na kunoga au vipi kaka misupu? hahahahhahaa
HAPPY NEW YEAR TO ALL !
nashukuru sana kwa maoni yenu yote
nayaheshimu sana mungu awabariki.

Chef Issa

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

FRI 1StJAN2010 THE OFFICIAL NEW YEAR AFTER PARTY


THE OFFICIAL NEW YEAR AFTER PARTY ON FRI St1 JAN2010 @ THE ONLY PLACE 2 BE FACE CLUB READING RG1 7JE FROM 10PMTILL3.30AM ENTRY 10 WE PARTY IN STYLE GIRLS''DRESS EXTRA SEXY ITS A BIG PARTY NOT TO BE MISSED C U THERE HOSTED BY BONGODJS ENTS
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Watangazaji wa coconut fm watinga mjengoni,wapigwa msasa wa nguvu tayari kwa 2010

Tuesday, December 29, 2009
Mmoja ya watangazaji mahiri wa Coconut Fm Husna B a.k.a Mgeni wa bahari katika pozi la kushangaa umeme ndani ya ofisi za (cheki nyuma yake),huku swahiba wake kulia akimshangaa kwa pozi lake la kimtindo.Zanzibar kwa sasa inakabiriwa na tatizo kubwa la kukosa umeme,inaelezwa umeme utarejeshwa kisiwani humo hadi mwezi februari.
Pichani ni watangazaji wa kiume wa Coconut Fm,Yoram na Boha wakishoo love baada ya kupata msaada wa kutosha
Watangazaji wa redio ya Coconut Fm 88.2 ya Zanzibar,wakiwa mjengoni Clouds Media Group wakipigwa msasa na Meneja Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga jioni hii,msasa huo unafanyika kwa ajili ya maandalizi yao ya ushindani mkubwa dhidi ya wapinzani wao kwa mwaka 2010
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

happy bethidei prof jay

.

Lei ni siku rasmi na kubwa sana kwa msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa bongo,si mwingine bali ni Prof Jay a.k.a Big Dad a.k.a Mzee wa Mitulinga,Ama kwa hakika Wanajamvini shime tumtakie kheri na fanaka njema katika siku yake hii adhimu ya kuzaliwa,Tumwombee kwa Mungu azidi kumjalia afya njema na mafanikio tele katika kazi zake.Na piaa kama vipi Jiachie inamzawadia kavidio hako ajiachie nako kiaina.
Kila la Kheri Prof Jay
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

wasafiri wa treni reli ya kati wakwama dodoma

Zaidi ya abiria elfu moja wanaotumia usafiri wa treni katika reli ya kati wamekwama katika stesheni ya Dodoma baada ya kutokea mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua kubwa zianzoendelea kunyesha mkoani Dodoma.



Mafuriko hayo yaliyotokea kati ya stesheni ya GULWE na MSAGALI wilayani MPWAPWA yamesababisha treni kushindwa kupita na hivyo kusababisha abiria waliokuwa wakitokea katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma na Tabora kuelekea mikoa ya Morogoro na Dar es salaam kukwama katika stesheni ya Dodoma .


Adha iliyowakumba abiria hao inatokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Dodoma ambapo zimesababisha miundombinu ya reli kati ya mikoa ya Dodoma na Morogoro kufunikwa na maji hali ambayo imesababisha safari za treni kuishia stesheni ya Dodoma.



Kukwama kwa abiria hao kunawakumbusha wasafiri wa reli ya kati adha na machungu waliyokuwa wakiyapata wakati wa mvua za Elnino zilizotokea miaka kadhaa iliyopita ambapo safari za treni zilikuwa zikiishia mkoani Dodoma na wasafiri kulazimika kupanda mabasi kuelekea mikoa ya Morogoro na Dar es salaam na hapa baadhi ya abiria wakiwa wamepoteza matumaini ya kufika kule waendako wanazungumzia hali hiyo.


Ili kufahamu kulikoni abiria hao kuendelea kupiga kambi katika stesheni ya Dodoma nalazimika kupiga hodi katika ofisi za stesheni hiyo na kuzungumza na mkuu wa kituo cha reli mjini Dodoma, Bakari Athumani.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Pombe za Krismasi




Mambo vipi kaka?

Kuna picha hizi za kutoa stress tungependa tushee na wadau

Picha zaidi unaweza ukawapa wadau link hii

http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=667579

THANKS

NIFAHAMISHE.COM TEAM

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

askofu atangaza nia yake ya kugombea ubunge kigoma

Na Mwandishi Wetu
KIGOMA
Wakati mwaka wa 2009 ukielekea ukingoni na kuukaribisha mwaka wa 2010, Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Dakita Gerard Mpango ameamua kukatiza muda wa kuitumikia Dayosisi hiyo na kutangaza nia yake ya kuingia katika kinyanganyiro cha kugombea ubunge katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 jimbo la kasulu Mashariki

Mpango ametangaza nia yake hiyo ya kuingia kwenye ulingo wa siasa katika kanisa la Anglikana mjini kasulu baada ya wajumbe wa baraza la SINODI kuridhia ombi lake la kutaka kustaafu mwishoni mwa mwezi Juni mwaka ujao ili kupitia bungeni aweze kupambana na mambo ya ufisadi.

Mtumishi huyu wa Mungu anachukua uamuzi huo baada ya kutoa huduma ya kueneza injili na kuwachunga kondoo wa mungu kwa muda wa miaka arobaini na ameahidi kuishi maisha ya uaskofu ndani ya siasa

Akitangaza uamauzi huo ndani ya kanisa na wakati akizungumza na waandishi wa habari,amesema amemua kukatiza muda wake wa kustaafu ambao ungekuwa mwezi march 2012 ili kupitia bungeni aweze kupambana na rushwa,ufisadi,kutetea haki za wananchi na maslahi ya Taifa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 29, 2009 | | Permalink | Maoni 2

BLOG MPYA ya mdau moviesblog-gameroom.blogspot.com



MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEARHONGERA KWA KAZI YAKO NZURI, JINA LA BLOG YANGU NI moviesblog-gameroom.blogspot.comKAMA JINA LA BLOG LINAVYOENDA BLOG HII NINAWALETEA MOVIE TRAILERS ZA NOW PLAYING NA COMING SOON.

NA PIA NINAONYESHA TV TALK SHOWS MAARUFU KAMA WENDY WILLIAMS/THE MONIQUE SHOW NA PIA REALITY SHOWS KAMA KEEPING UP WITH THE KARDASHIANS. NIA YANGU YA KUKUANDIKIA EMAIL NI KUKUKARIBISHA/KUWAKARIBISHA KWENYE BLOG NA PIA UWEZE KUPOST KWENYE BLOG YAKO( KWA MAELEZO YAKO MWENYEWE) ILI WADAU WOTE WAWEZE KUKARIBIA.MAELEZO ZAIDI HAPO CHINI PAMAOJA NA PICHA.




PICHA YA BLOG PIA NI KAMPUNI TOFAUTI MAARUFU ZA MOVIE PRODUCTION (HIYO TRAILER HAPO JUU NI YA LOGO/MAKAMPUNI MAARUFU YA MOVIE PRODUCTION)


Hii blog kwa ujumla inawaletea TRAILER za movie (sinema) ambazo zipo na zinatarajia kuwepo kwenye MOVIE-THEATRE (cinema).Katika hii blog Wadau mmerahisishiwa ununuaji wa movie, kwasababu kwa sasa kuna movie na dvd nyingi sana zinauzwa na machinga LAKINI wengi wetu tunanunua dvd kutokana MVUTO WA PICHA YA JUU AU COVER/KASHA bila kujua kama hiyo movie kweli ni nzuri na utae-enjoy.




Sasa hapo ndipo moviesblog-gameroom.blogspot.com inapochukua NAFASI YAKE RASMI, kuweza kuwawekea trailer za movie ili uweze kuchagua/kununua dvd ambayo umeipenda kutokana na trailer.Inatokea sana tukifika nyumbani tunalalamika wakati wa kuangalia DVD kwamba "UNGELIJUA USINGE"...
Mdau wenu nimeona bora wote tufaidi na hela zetu ziende zinapotakiwa tupate kitu roho inapenda. Movie ni kitu cha ku-enjoy katika siku ndefu na hali zetu za sikuhizi (uchumi, stress etc). Imesemekana kwamba tangia RECESSION ipige kisawasawa, soko la "movie rentals" (kuazima movie) limeongezeka na limetabiriwa kuzidi kuongezeka.


Humu ndani mnaweza kunitumia email gameroom101@ymail.com na kuniambia movie ipi mmeisikia itatoka au kama kuna movie unajua ipo mtaani ila huna uhakika kama ni nzuri na niweze kuweka TRAILER yake.HAPO MBELENI moviesblog ITAANZA KUWEKA FULL MOVIES NA MTAWEZA KUANGALIA FREE.


TAFADHALI TOENI MAONI YENU (TUNAYAHITAJI)HELA NGUMU BWANA LAZIMA IANGUKIE PANAPOELEWEKA.KARIBUNI.(kuna coming soon,na available now)




Mdau: Moviesblog

TOKA DALLAS,TX UNITED STATES.
NASHUKURU KWA MDA WAKO.S
IKUKUU NJEMA.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

aai Dj BUllaaaah.!

Monday, December 28, 2009
Mmoja wa Ma-Dj mahiri kabisa kutoka Clouds FM ,Dj Bullah pichani akikamua vilivyo kwenye moja ya mnuso hivi karibuni jijini Dar.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

kampeni ya shangilia taifa stars ishinde kuanza kuanza kesho


Pichani kushoto ni Meneja Matukio na Promosheni wa SBL Bahati Singh akifafanua jambo katika mkutano huo.

Pichani juu kabisa ni Meneja uhusiano wa kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika kiwandani hapo kuhusu promosheni ya shangilia Taifa Stars inayoanza kesho wakati timu hiyo itakapocheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya Ivory Cast Januari 4 na 7 jijini Dar .Ivory Coast inajiandaa na mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Angola.

Promosheni hiyo itawafanya mashabiki mbalimbali wa soka katika baa mbalimbali kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Bia za Serengeti, Kofia, Fulana na jezi za timu ya Taifa pamoja na tiketi za kuingilia katika michezo hiyo, wanaofuatia katika picha ni meneja mkuu wa kampuni hiyo Mr Kagusa, Bahati Singh meneja matukio na promosheni na mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa. Picha kwa hisani ya Fullshangwe.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 28, 2009 | | Permalink | Maoni 1

ebwanaee hawa si yanga kweli?


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 28, 2009 | | Permalink | Maoni 1

mdau anauliza hawa wako wapi?

Msaada tutani Pliiiiizzzzzzz ......... kuna watangazaji fulani hivi wa Radio One Stereo sijawasikia siku nyingi. Nao ni Rachel Doba na Rose Chitala. Wako wapi siku hizi? Mwenye habari atuhabarishe waungwana.

Ni mimi mdau wa Blog
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 28, 2009 | | Permalink | Maoni 7

burudika na kibao hicho murua kabisa na wikend njema

Sunday, December 27, 2009
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, December 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Computer Problems?

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, December 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Hatimaye Kelly Michael achukua jumla

Bibi na bwana harusi wakijimwaya mwaya ukumbini usiku huu kwa furaja tele mara baada ya kufunga ndoa takatifu leo mchana katika bustani za Botanical Garden jijini dar
Mc naye akijimwaya mwaya na bibi Mariam toka Clouds Fm
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Fm
John Tall a.k.a Maprint Print akiwa amepozi na mkewe usiku huu kwenye mnuso wa Kelly Michael
Wageni waalikwa wakijimwaya mwaya ukumbini usiku huu
Mc alikuwa Efrahim Kibonde kutoka Clouds Fm,pichani alikuwa akiwasisitizia jambo maharusi
Maharusi wakikata keki ya upendo usiku huu katika ukumbi wa HappyDragon,Kawe jijini Dar,Mnuso ulikuwa wa nguvu ile mbaya kila mmoja alionekana kuridhika vikiwemo vinywaji safi kabisa,Muziki kama kawa uliporomoshwa na kijana toka Mjengoni Dj Bullah
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, December 27, 2009 | | Permalink | Maoni 1
Idadi ya watu