shoo love ndani ya Str8Muzik Festival ilivyokuwa
Monday, November 30, 2009
Wadadazz wakigombea taulo alilokuwa akilitumia D banj alipokuwa jukwaani,mara baada ya kumaliza shoo akalitupa kwa mashabiki wake wakiwemo hawa walimbwende ambao walibahatika kulidaka kwa raha zao,tatizo walikuwa watatu sijui nani alikubali kumuachia mwenzake,kaaazi kweeli kweli.!
Wazee wa GENGE,shoto ni Nonini na Juacali wakiwa wamepozi mwishoni mwa wikend kwenye tamasha la Str8Muzik Festival;Intercollege special 2009,kabla ya kukamua jukwaani.
Mkali wa Crank bongo Cpwaa akiwa amepozi na Juacali
"Ebwanaee mzee wa genge unajua nini inabidi tutoe singo moja matata sana,au unasemaje ?"Prof Jay anaonekana akimwambia maneno hayo mkali mwenzake wa kufloo Juacali.
Marlow naye alipata ladha ya kupozi na msanii wa kihip hop toka kwa watani wetu wa jadi,aitwaye kwa jina la kisaniii Juacali.
Wote wakali katika anga ya muziki wa kufoka foka,shoto ni msanii wa hip hop kutoka Kenya ambao wao wanauita 'Genge',Nonini akiitazama kwa makini Cd ya albamu mpya ya muziki wa hip hop hapa bongo a.k.a bongofleva Albert Mangwea iitwayo Nn'ge.Ni bonge ya albamu ambayo kiukweli imeandaliwa vyema kabisa,iko sokoni kwa sasa,inasambazwa na Zizzou Entertainment.
































.jpg)








