simba yaichabanga yanga goli moja tu.!

Saturday, October 31, 2009
Timu ya Simba imeichabanga timu ya Yanga goli moja katika kipindi cha kwanza,goli hilo la kuumiza mno kumoyo na la kutia hasira lilitiwa kimiani na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza. Mgosi aliunganisha kamuzi moja matata sana ya Dan Mrwanda ambaye aliwachanganya vilivyo mabeki wa Yanga na kutoa pande.Hata hivyo Dan Mrwanda alitolewa kwa kadi ya njano ya kuchupa ndani ya 18 akisaka penati,refa aliyekuwa akichezesha mtanange huo Oden Mbaga akamchapa kadi nyekundu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, October 31, 2009 | | Permalink | Maoni 1

MISS UTALII ILALA NA KINONDONI 2009 wazidi kula vichwa vya udhamini

Pichani ni warembo/washiriki wa shindano la miss utalii Ilala 2009 wakipata chakula chao leo mchana.


kampuni ya mashujaa pub and entertainment pamoja na kampuni ya usafiri ya Mamaa Sakina Trans,zimejiunga na makampuni mbalimbali nchini kudhamini shindano la Miss Utalii Ilala na Miss Utalii Kinondoni2009.

Kampuni hiyo imedhamini zawadi za washindi mataji ya Miss Utalii Ilala2009-Vipaji na Miss Utalii Kinondoni 2009 -Vipaji,kwa kuahidi kutoa zawadi kwa washindi.Washindi wa mataji hayo kila mmoja atapatiwa zawadi zenye thamani ya shilingi 300,000 kila mmoja,zikiwemo fedha taslim shilingi 150,000 kila mmoja.

Akizungumza na warembo wanaoshiriki mashindano ya Miss Utalii Ilala2009,waliotembelea Ukumbi wa kisasa wa burudani na Mikutano na,Restaurant,Mkurugenzi wa Mashujaa Pub Papa Maisha na mkurugenzi wa Mamaa Sakina Trans walisema kuwa wamevutiwa sana na mashindano ya MissUtalii Tanzania hususani kutokana na kubeba sura halisi ya utanzania na utamaduni wa mtanzania,hususani pale washiriki wanapo shindanakuwania taji la vipaji kwa kucheza na kuimba nyimbo za asili zamakabila ya tanzania.


Shindano la Miss Utalii Ilala 2009 litafanyika Ijumaa 6-11-2009 katika ukumbi wa Da'west Park Inn Tabata,ambapo bendi ya Extra Bongo chini yaAlly Choky na Diamond Musica chini ya Mulemule ambaye amehamia bendi hiyo akitokea FM Academia watachuana vikali,huku upande wa muziki wa asili utaongozwa na kundi la Mfalme Band chini ya Costa Sibka.
Habari na picha kwa hisani ya
By Aminna Bokka Machupa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, October 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

vita ni vita tuu.!

Huu utani wa jadi mmh,mie yangu yangu macho .! Leo ni leo msema kesho ni mwongo Simba v/s Yanga patakuwa hapatoshi wanja jipya la National Stadium.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, October 31, 2009 | | Permalink | Maoni 4

MISS EAST AFRICA RWANDA KUPATIKANA LEO SERENA HOTEL

Wasichana wanaoshiriki shindano la Miss East Africa wakiwakatika picha ya pamoja

Kamati ya Miss East Africa, ikiwa pamoja na Waziri wa Jumuiya ya AfrikaMashariki Rwanda, Madame Monique Mukaruliza (mwenye suti) pamoja nawarembo wanaowania shindano la Miss East Africa Rwanda. kulia kwa wazirini Bosi wa Udhamini, Matukio na Uhusiano wa New Habari (2006) Limited,Petter Mwendapole, wakati kushoto ni Rena Callist na Adam Kapama kutokaRena Events.
WASICHANA 12 leo wanatarajia kupanda jukwaani katika hoteli ya Serenamjini hapa kwa ajili ya kuwania taji la Miss East Africa Rwanda.Mshindi wa kwanza na wa pili katika shindano hilo watawakilisha Rwandakatika fainali za Miss East Africa zitakazofanyika Desemba 18 mwaka mjiniDar es Salaam.Mshindi wa shindano la leo ataondoka na kitita cha faranga za Rwandamilioni moja sawa na karibu sh milioni tatu za kitanzania.



Mshindi wa pili ataondoka na Faranga mia tano sawa na karibu milioni mojana nusu za Kitanzania.Tayari Kamati ya Miss East Africa makao makuu iko mjini hapa kwa ajili yakushuhudia shindano hilo ambapo Jaji mkuu usiku wa leo atakuwa RenaCallist, mkurugenzi wa Rena Events.

Pia Miss East Africa, anayemaliza muda wake, Claudia Niyonzima atakuwepokushuhudia shindano hili pamoja na Miss Burundi wa mwaka jana AliceKaneza.Wakati shindano hilo linashirikisha warembo hao 12, mchuano mkali zaidiunaonekana kuwahusisha warembo wanne ambao wanachuana kwa vitu vingi.Nafasi kubwa sana inaonekana kwenda kwa Sabrina kaganza, Leticia Umuizayire, Annet Mahoro na Cynthia Akazuba.



Lakini pamoja na hao wanne msichana mwingine ambaye anaweza kufanyamaajabu usiku wa leo ni Viviane Umulisa.Warembo hao juzi walikutana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wahapa, Joseph Habineza ‘Mr Joe’. Jana pia walikutana na Waziri wa AfrikaMashariki wa hapa Monique Mukaruliza.Warembo wengine ambao wanashiriki shindano hilo ni pamoja na ClariseIshimwe, Rita Uwera, Pamela Ungabire, Clarise Ushuti na SoniaUwambambazi,
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, October 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

unity of women friends gala night on sunday

Friday, October 30, 2009

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, October 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

hata wazungu wanaimani za ushirikina?sehemu ya pili

mkulima mwenye furaha na mafanikio ya sama mzuka umempanda wakati wa kuomba dua
Jumatatu asubuhi ndio tamati ya shunghuli wakitoka kanisani kuomba tena

Hiki ndio kigari kinachobebea karanga mbichi kuleta ktk tukio sio mtungi wa kusindikia waini kama tulivyozoea


hapa wanatoka kanisani wanaelekea eneo la tukio kwa ajili ya ngoma



hapa wakulima wanaelekea kanisani kuomba wakiwa ktk mavazi ya jadi


Hapa wakulima wanakwenda kanisani kuomba kabla ya ngoma ya jadi


Hapa wakulima wakielekea eneo maalumu waliloandaliwa wakiwa pea mume na mke



Kaka michuzi tunaendeleza libeneke ktk sehemu ya pili na ya mwisho ya tukio la ngoma ya samma ambayo huambatana na mila na sala za kuomba mzimu wa sama usirudi tena upotee lakini cha kushangaza tukio hili limekua ni la kudumu kila mwaka linafanyika na mzimu huo upo tu inamaana dua na mila hiyo haisaidiii jibu kwa wenyeji.


Baada ya kukutana na kunywa na kula pamoja tukio linalofuata ni kwenda kanisani ambayo hua inafanya mchana wana vaa nguo zao za jadi then wanakua pea kila mkulima na mkewe wanapendeza sana ni wakulima wa kila lika. Wakishaongozana kuingia kanisani na kusali wanatoka tena wakiwa ktk foleni nakuelekea eneo la tukio ambalo wanakua na ngoma na sala tena ya kimila ambayo hufanywa ktk kadamnasi na kunakua na wakulima wawili waliovaa kama hilo li mzimu kuashiria kua limeshindwa na limekubali kusarenda na linatoa sadaka kama hongo kwa watu wote walipo hapo ikiwa hao wakulima wawili wanagawa karanga mbichi amabazo zipo ktk kibegi kidogo cha mbao alichobeba mgongoni na karanga hizo huletwa na kigari kidogo cha mbao ambacho kina mizinga miwili ya mbao kama ile ya kuhifadhia au kusindika wine au mvinyo.


Baada ya sherehe hiyo kuisha siku ya jpili kunkua na tukio la mwisho siku ya j3 asubuhi sana ni maalumu kwa wakulima tu wanaingia asubuhi sana kanisani wanasali mpaka saa 4 asubuhi wanatoka kanisani na kuingia hotelini ambapo wanapata chakula cha mchana na vinywaji na unakua mwisho wa tukio zima Kweli ni burudani sana na tukio hili ni refu kweli lakini ilibidi niamke j3 mapema kwenda kunasa tukio la mwisho maana ile ngoma ya usiku nilishuhudia tatizo camera nilisahau nyumbani nikakosa kupiga picha tukio.



Naimani ndugu zangu hapo home watakua wamefurahi sana kusoma tukio hili la wakulima wa kiswiss next linafatia tukioa la mteja mfalme pia nilishuhudia kabla ya kuondoka kurudi venice ili na wafanya biashara wetu wajifunze. Kazi njema kaka michuzi Jiachie Libeneke super si mchezo
Malik Williams
Venice Italy
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, October 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

askari wa jiji wako likizo nini? Enzi zile aaah zamaaani.!

Thursday, October 29, 2009

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, October 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

mzigo mpya umeingia maduka ya big respect

Mkurugenzi wa maduka ya Big Respect,Biggie mwenyewe kulia akimuonesha mteja wake baadhi tshet zilizotinga dukani kwake hivi karibuni.



Wadau wa kibongo na hata mlioko huko ughaibuni huu ndio muda wenu umewadia wa kujivunia mavazi ya kihome home,kualiti ndiyo mahali pake,toka kijanja ukiwa umependeza katika muonekano tofauti kabisa katikati ya kadamnasi ya watu.Kila aina uitakayo imetinga ndani ya duka la BIGG RESPECT ambalo lipo Kariakooo karibu na kituo cha mafuta BIG BON .
Kontakt cheki bana lake pale juu
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, October 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ebwana ee mkali huyu kutua bongo na kukamua ndani ya fiesta one love 2009


Mkali huyu kufanya kamuzi la nguvu ndani ya Tamasha la fiesta one love 2009,litakalofanyika Lidaz Club,kinondoni jijini Dar,mkali huyo ataambana na crew ya watu sita,kama mdau wa burudani umejipanga vipi ? kiiingilio sio issue sana kwani ukiwahi mapema utainunua kwa buku kumi tu,ukichelewa ndiyo hivyo tena kwa elfu kumi na tano kwa kichwa,changamka wewe ukajionee kamuzi la kufa mtu kutoka kwa mchizi wa ughaibuni,Wanajamvini nina haja kweli ya kumtaja jina? nambieni kama vipi nifanye hivyo ili twende sawa,halafu unajua nini kuna kidude cha kubofya bofya hivi kwa ajili ya fiesta,bofya link hiyo uone uhondo wake ulivyotulia.
unaonaje mwana jamvini
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, October 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Ally Rehmtullah to Showcase in Cote d'Ivoire

The 10th edition of 'YEHE', placed under the patronage of Mr Jean-Louis Billon, President of the Chamber of Commerce & Industry of Côte d'Ivoire, will take place on the 28th of November 2009. A Fashion show with 32 invited countries (South Africa, Benin, Burkina Faso, Cameroon, CAR, DRC, Ethiopia, Gabon, Ghana, Guinea, Niger, Nigeria, Mali, Mauritania, Uganda, Kenya, Rwanda, Senegal, Sudan, Tanzania , Chad, Togo, Venezuela, Zambia.)

Designer Ally Rehmtullah will be represting Tanzania at this fashion show and will get an opportunity to work with 31 other designers from all over the continent. This will be a platform to network Tanzanian Fashion with the rest of Africa and to exchange ideas on how to develop fashion in Africa and to take it to the next level.

The concept of 'YEHE' was established in Abidjan, Cote d'Ivoire in 1998. It is primarily on the thematic level, an original word Yacouba (language of the mountainous region west of Côte d'Ivoire) which means 'sewing'. The creators of 'YEHE', true lovers of fashion, have invested to enhance its image as polluted by the insertion of this profession in the process of economic and social development of Côte d'Ivoire.
Like organizations reliable and relevant, the 'YEHE' began in the year 2002 a remarkable evolutionary phase with the help of the National Commission for UNESCO Côte d'Ivoire, under the leadership of its Secretary General Madame Odette YAO YAO. With the help of the National Committee UNESCO-CI and other partners, YEHE totals to date more than 600 sewing machines distributed to local and foreign artists.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, October 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

hata wazungu wanaimani za ushirikina?



















Habari kaka michuzi, pokea simulizi na picha za tukio la kijadi ambalo hua linafanywa na wakulima wa kiswiss upande wa miji inayoongea lugha ya kijerumani. Tukio hili lilifanyika mji mmoja unaitwa Giswir karibu na jiji la Bern ambao ndio makao makuu ya nchi ya swiss nilikua hapo kwa kazi ya mwezi mzima kwahiyo niliweza kuifatilia kwa ukaribu sana sherehe hii inayochukua zaidi ya wiki moja kwa matukio mbali mbali.






Kwanza kabisa hua inaanza ngoma ya kufukuza mzimu wa samma au kiangazi kwa lugha yetu ngoma hii hua inapigwa majira ya saa 3 usiku wakati jua linazama kwani kiangazi huku jua hua linachelewa sana kuzama huwa wanabeba kengele kubwa sana nyeusi wanapiga mtaa hadi mtaa kama ngoma ya daku huko nyumbani baasi ni burudani kweli najiuliza hata wazungu wanaimani za ushirikina? huo mzimu gani wa samma? ni mikogo kwelikweli ngoma hii ni maarufu sana inapokwisha samma na kuingia autumn pia huambatana na tukio la kuhamisha mifugo toka milimani na kuletwa maeneo ya tambarale ambapo pia hupigwa ngoma nyingine na ni tuzo kwa wanyama ambao walichangia vizuri kipato kipindi cha kiangazi mfano ngombe alietoma maziwa mengi sana anavishwa taji la uwa kubwa sana kuliko wenzake na anatembea kwa madaha kweli kweli utadhani anatambua kua yeye ni malikia basi barabara hufungwa na nyombe wanatawala. siku inayofuata kunakua na tukio la kwena kanisani kuomba na wanavaa nguo zao za asili wanapendeza sana wanakutana kwa chakula cha pamoja na kunywa pamoja picha tutaziona sehemu ya pili ya simulizi hili.






kwa sasa pokea picha ya ng'ombe wakionekana wapo chini ya milima wameshashushwa, pili duka la kengele wanazo vaa ng'ombe, tatu ni ng'ombe wakiwa barabarani wanatoka mlimani walikokua wakiishi wakati wa kiangazi, nne ni Gari tunayo itumia kwa shughuli za kazi gari hiyo ni nyumba tosha mzee inakila kitu ndani imepaki nje ya hotel ambayo tulifikia na tano ni picha ya muonekano wasasa barafu ndio imeanzakudondoka ni baridi kweli mzee.






Kesho nitaendelea na simulizi la sehemu ya pili na picha zaidi nitatuma za kanisani na ngoma ya mwisho. kila lakheli na kazi njema badokuna matukio kibao kama haloween na fshnati pia kuna skendo kibao za jadi nitatuma mzee kwasasa nimesharudi Italy nakofanya kazi nami ni mtanzania.




Venice Italy


Malik Williams
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, October 29, 2009 | | Permalink | Maoni 3

moja 200.!

Wednesday, October 28, 2009

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Nani kuibuka na kitita cha milioni moja fiesta mikokoteni marathon?


Jumapili hii kutakuwepo na shindano kali na lenye kusisimua litakaloitwa Fiesta Mikokoteni Marathon,hiyo ikiwa ni moja ya shamra shamra kuelekea kwenye kilele cha tamasha la fiesta one love 2009.

Katika shindano hilo la kipekee kabisa, mshindi wa Fiesta Mikokoteni Marathoni ataibuka na kitita cha shilingi milioni moja keshi, na mshindi wa pili atajinyakulia shilingi laki tano na wa tatu atajinyakulia shilingi laki tatu.Ama kweli siku hiyo itakuwa mtu kalala masikini kaamka tajiri bila ubishi, ooh mtaji tosha huo…!

Aidha mratibu wa shindano hilo, Abraham Mossi kutoka Kampuni ya Prime Time Promotions/Clouds Fm ambao ndiyo waandaaji wa Fiesta One Love 2009, alisema kuwa maandalizi ya kila kitu kuhusiana na shindano hilo yamekwisha kamilika.

“Mpaka sasa vijana wengi wamejitokeza na kujiandikisha safi kabisa kwa ajili ya ushiriki wa shindano hilo, kama ilivyoelezwa kuwa litakuwa na donge nono kwa mshindi wa kwanza, kimsingi kila mmoja ameonekana kujiamini kuwa lazima aibuke nalo” alifafanua Mossi.

Vituo vilivyotajwa katika mzunguko mzima wa shindano hilo, imeelezwa kuwa litaanzia viwanja vya Lidaz Club, Kinondoni jijini kupitia Kinondoni Makaburini, Kinondoni kwa Manyanya, Kinondoni Kanisani, Oysterbay Police, Kanisa la St. Peters na kumalizia viwanja vya Leaders Club.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Serengeti Premium lager , Zain, Prime Time Promotions, Clouds Fm pamoja na Kitangoma Magazine.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

jiachie na shear illusions utoke bombaa.!

SLEEK WIG FASHION
HUMAN HAIR STYLE TANZANITE
SLEEK WIG FASHION 100% HUMAN HAIR
THANSURA WIG
CUSTOMER CUT WIG
SLEEK WIGS FAHION 100%HUMAN HAIR
AINA MBALIMBALI ZA MAFUTA

Moja ya duka la shear Illusion linavyooneka kwa ndani



Available at :Mlimani City Mall shop no.62 Sam Nujoma.
Millenium Towers 1st floor All Hassan Mwinyi Road,kijitonyama
and Mikocheni B Old Bagamoyo Road near DIS.
Opening from 8:30am to 8:o0pmOpen 7 days a week for your convinience
http://www.shearillusionstz.com/
Contact number +255 222774730

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 4

mwana FA kuwarusha wasauzi oktoba 31, 2009


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

mambo ya hip hop wear haya


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

shokito kukamua jukwaa moja na ferre gola dar


MWIMBAJI nyota chipukizi wa Kongo Makinu Kombo ‘Shikito’ anatarajiwa kuongozana na mkali wa bolingo kutoka nchini humo, Ferre Gola Batangire.Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, msaidizi Kitengo cha Uhusiano,Udhamini na Matukio wa New Habari, Aziza Seif, alisema Shikito ni miongoni mwa wanamuziki 17 watakaokuja nchini kwa mwaliko wa New Habari(2006)Ltd.


“Katika orodha ya wanamuziki 17 ambao Ferre ametutumia majina yake, yupopia Shikito lakini mtoto mwingine aitwaye Ilunga hatakuja kwenye msafarahuu,” alisema.
Aziza Aliwataja wanamuziki wengine wanaokuja na Ferre kuwa ni pamoja naFreddy Makola Linakasi, Nikodeni Kanday Ngoy, Olenga Makiese, ClizoKalonda Lopeta, Sungu Mbobolo, De Gaule Matima Makitela, Guy NgolaMawesele, Awulu Wala Tshipanga Wale, Ngwanzu Bavuidibio Gaza, DebosSunguesabena wa Kayembe, Mabiala Mobele, Mchele Mkelele Kitongo naChristian Solo Kabongo Muyambi.



Wengine ni Vicky Moleka Leta, Patricia Isako Apakati, Renate KungaMuwangu, Nancy Mbemba-Lohuma.Shikito ni kijana mdogo ambae amejichukulia umaarufu mkubwa sana ndani nanje ya Kongo kwa kuwa mwimbaji mahiri mwenye umri mdogo zaidi katika angaya muziki wa dansi afrika.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Ombi la kutangaziwa mabadiliko ya tovuti



Naomba nafasi katika blogu yako kuwataarifu wasomaji kuwa tovuti ya mpya ya wavuti.com imechukua nafasi ya iliyokuwa nukta77.com na nukta77.blogspot.com
Naomba yeyote aliyekuwa ameweka linki ya nukta77 aihariri na kuweka wavuti.com
Karibuni sana kutembelea kwa taarifa za nafasi za masomo na kazi kwa burudani na bila kusahau habari na porojo!
Asanteni.
wavuti.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 1

Hatimaye TBC yaingia online!


Nimeibamba TBC mtandaoni leo, basi nikatabasaaamu, mwe!, anwani yake ni http://www.tbc.go.tz
Mdau Subi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 3

UJUMBE KWA WALALA HOI toka uk

IF YOU CAN'T FIND SAMTHIN' TO LIVE FOR,YOU BEST FIND SAMETHIN' TO DIE FOR' 2pac shakur 14-22.TO BREAK DOWN.KAMA MAISHA HAYAENDI MSOWANO BASI BOLA KUTAKE RISK KUWEKA SAWA,KATIKA KUTAKE RISK KUNA KUITOA,USIOGOPE KUARIBIKA KWANI TAYARI UMESHAHARIBIKIWA NA MAISHA.
MDAU AL PACHINO UK.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, October 28, 2009 | | Permalink | Maoni 7

Rais Karume Arejea Kutoka Ufaransa

Tuesday, October 27, 2009
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi,Dk. Aman Abein Karume akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuwasili kutoka nchini Paris Ufaransakatika mkutano wa 35 wa Unesco.
Rais Karume akisalimiana na viongozi wa kijeshi Zanzibar na wa Serikali ya Zanzibar waliofika kumpokea uwanja wa ndege
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, October 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

miss utalii ilala 2009 yazidi kumiminiwa wadhamini

Meneja Savannah Lounge, Lucas Paul,(kati) na Msaidiz, i Pasal Bonivanture, wakati wa kutangaza udhamini Miss Utalii Ilala leo
Ikiwa ni katika kuitikia wito wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho kikwete,rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa taifa wa chama cha mapinduzi,alio utoa mwezi machi 2006,alipo wataka wafanyabiashara binafsi,makampuni na taasisi mbalimbali binafsi na za umma kuwaunga mkono waandaaji na shindano zima la Miss Utalii Tanzania kwa hali na mali na kujitokeza kulidhamini shindano hilo,ambalo kwa kauli yake alisema “kuna mjasiliamali mmoja anaitwa Chipungahelo,ameanzisha kitu kizuri chenye manufaa kwa Taifa letu kiuchumi kupitia utalii na utamaduni,laki hawa wajasiliamali hawana kitu,tuwasaidie kaeni nao tuone jinsi ambavyo tunaweza kuwa saidia kama serikali,kwani wanafanya jambo zuri kwa taifa letu” kauli ambayo aliitoa alipotembelea wizara ya habari michezo na utamaduni tarehe 8-3-2009.

washiriki miss Utalii Ilala 2009

SAVANNAH LOUNGE tukiwa kama wadau wa sekta ya Utalii,Elimu na utamaduni,tukishirikiana na Kampala International University tawi la Tanzania ,kwa muda mrefu tumekuwa tukifuatilia mwenendo mzima wa mashindano ya urembo nchi,hususani mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania.
Tumegundua na kuridhika kuwa shindano hili ni miongoni mwa mashindano bora na yenye kufanya vizuri zaidi katika bara la Afrika hususani kimataifa,huku kitaifa likiwa lina fanya vizuri sana katika kusaidia juhudi za serikali ya awamu ya nne ya kutangaza na kuhamasisha utalii nchini na kuitangaza Tanzania ,vivutio vya utalii kitaifa na kimataifa,huku wakiwa wanashinda mataji mbalimbali ya dunia na kimataifa kila mwaka tangu kuanzishwa kwake miaka mine iliyopita.
Pamoja na mafanikio ya shindano hili kitaifa na kimataifa lakini tumeona wanatatizo kubwa la udhamini,linalochangiwa pengine na uchanga wake au mwamko mdogo wa wadau mbalimbali juu ya kuthamini utamaduni kitu ambacho shindano hili kwa kiasi kikubwa limekuwa likikabiliwa na kukosa udhamini,kitu ambacho kinatufanya tuamini kuwa iwapo watapatiwa udhamini wa kutpsha wanaweza kufanya maajabu zaidi katika sanaa ya urembo nchini na kutangaza zaidi utalii wan chi yetu,kama ambavyo wamekuwa wakifanya japo kwa ukata mkubwa.
Udhamini wetu ambao unahusisha fedha,huduma,mali na zawadi unajumuisha huduma,mali na fedha taslim ukiwa na thamani ya jumla ya shilingi 50,000,000.Ambazo ni kwaajili ya zawadi,ukumbi na huduma za chakula na. wasanii Majina ya Washiriki hao ambao ni Sauda Ramadhani(22),Roseline Sekwao(19), Janneth Samsoni(19),Nezia Gabriel(22),Neema Mangaka(19), Shaymaa Ntetema(20), Jamida Abdu(21),Flora Nicholaus(22), Sheila Said Baamary(23)Tickey Lighton(21),Tausi Thomas(21), Aghata Kilala(20

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, October 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

WAPI wiki hii.Mpango Mzima..Kazi kudhibiti kazi


Karibuni kwa mara nyingine tena, husika na WaPi ...tamasha la kila mwezi. Kama kawaida"WaPi" inaendelea kwa muundo wa kila miezi mitatu. Baada ya mzunguko wa mikoani..Iringa mwezi wa 8-08-09, Arusha 3-10-09.


Tumerejea Daa. Safari hii kauli mbiu yetu ni Mpango Mzima... kwenye mada yetu "MPANGO MZIMA...kazi kudhibiti kazi"... KIJIWE MAARIFA tutakuwa na Boyd Oyier msanii mahiri wa uchoraji na usanifu taswira. Atafanya warsha ya uchoraji, usanifu wa taswira Yawaletea Nyota kali (mziki asilia), Wakwetu (motherland), Young-D(msanii chipukizi wa rap), Maya(mshairi), Msafiri Zawose, Momo (msanii wa hiphop toka Canada), Tafakari emsii mahiri chipukizi), Manzii(msanii wa hiphop toka Rwanda) Wasanii mbali mbali wa sauti ya handaki(undeground), Katika harakati. Madijei, ma emsii, machata, mabreka ,michoro mbali mbali, ushairi,ngoma, maigizo na usanifu mitindo.


Mahali: British Council, Dar Es Salaam
(maelekezo: Samora na Ohio, mkabala na Steers kati kati ya jiji)
Jumatano, 31-10-2009 mida; saa 9 -alasiri-hadi 2 usiku Mada ya mwezi:ni MPANGO MZIMA-kazi kudhibiti kazi



-- Tuko Sayari moja, tunaishi dunia mbali mbaliMaisha chemsha bongo, jaza mwenyewe.

Ra
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, October 27, 2009 | | Permalink | Maoni 2

Kanuni za Chama Cha Wanaume wanaopigwa ndani ya ndoa Tanzania (CCWWT)

Monday, October 26, 2009
Kanuni ya Kwanza….

Huruhusiwi kumuoa Mwanamke mpaka akuletee CV yake ili ukague kama shuleni alishiriki Michezo ya kurusha Tufe na Ndondi.Hii itakusaidia kumchagua mtu right!

Pili, Mwanamke anapoanza kukudunda unaruhusiwa kutuma please Call me kwenye 911 ya Police!

Tatu, Mwanamke haruhusiwi kumpiga Mwanaume akiwa Soba,ni lazima Mwanaume awe amelewa ndo umdunde ili kuepusha Maumivu ya dhati.

Nne, Kwa kuwa wanaume wanaopigwa na wake zao huwa wanadanganya Ofisini kwamba wameanguka au wamekabwa na vibaka, tumegundua huo uongo umepitwa na wakati kwa hiyo Chama kimeamua kuwaajiri waandishi wa script za Filamu za Kibongo ili wasaidie kuandaa Uongo mpya!


Tano, Kanuni nyingine ni kwamba kila Mwanaume unapopigwa, nenda ukweni upunguze kitu kimoja kwenye Mahari uliyotoa. Kama ulitoa Mahari ya Ng’ombe 10 baada ya Vipigo tisa tunategemea kitakuwa kimebaki kipigo kimoja tu umalizie Ng’ombe wako wa kumi na ndoa kwisha!


Sita, Marufuku kwa Mwanamke kumpiga mme wake kwenye Foleni unless gari liwe na vioo vya Giza, tinted! Lakini ikitokea ulazima,Mwanaume ukipigwa kwenye gari lisilo na tinted jifanye unacheza ile style ya Busta Rhymes katika wimbo wa Arab Monay!


Saba,Kwa wakati huu ambapo kuna mgao wa umeme,kwa hivyo redio na TV zinakuwa zimezimwa,ni marufuku kwa Mwanamke kumpiga Mmewe kwa kuwa Sauti zitaenda mbali.


Nane, Mwanaume unapopigwa ni lazima kulia kwa kutaja jina la Chama na sio ulie Mamaaa!


Tisa,Mwanamke unatakiwa unapompiga mmeo iwe ni mwisho wa mwzi au tarehe kama hisia ili jioni asirudi na awe na pesa ya kusogeza katika mbili tatu baa ya jirani.


Na Kanuni ya Mwisho ni lazima siku ambayo mama umepanga kumpa Kipigo Baba, watoto wote wawe wamepelekwa kwa Bibi kwa kisingizio cha kwenda kusimuliwa hadithi za kale!

Hizo ni Kanuni 10 za Katiba ambayo bado ni Rasimu na una nafasi ya kuongeza Kanuni nyingine kupitia namba 0786 000884 na utajibiwa na Mwenyekiti Paulo James au Katibu Gerald Hando! Barbara ni shahidi tu! Ova!Imeandaliwa na Detective, Chairman wa CCWWT - PJ na Katibu Gerald Hando kwa niaba ya wanachama wote wa CCWWT.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 26, 2009 | | Permalink | Maoni 5

number 10 liko mitaani sasa,wahi kopi yako mapema

chukua tu copy yako uone...
please please tuwasiliane kupitia info@number10.co.tz
au shadaka20@yahoo.co.tz
+ 255 713 350833
cheers shaffih dauda

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 26, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Ally Rehmtullah to showcase in TUNISIA!


After the stunning success of the Miami edition, Catwalk For Africa 2009 - Afrochic A La Mode is officially on. A bigger show, a spectacular venue, top-notch entertainment, live performances and world-class exhibits.
African fashion's new wave, represented by Bot I Lam and Pacy Kone, will rock the runway together with internationally acclaimed and award winning designers, Imane Ayissi, Ally Rehmtullah and Martial Tapolo.
They will be welcomed and accompanied through the journey by top Tunisian designers. The fashion show will be taking place at the Oasis Night Club, one of the biggest night clubs in Africa, located at the heart of Yasmine Hammamet, on Saturday, the 5th of December.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 26, 2009 | | Permalink | Maoni 2

haya hii TAXI YA STOCKHOLM


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 26, 2009 | | Permalink | Maoni 20

fiesta one love ndani ya shoo love ndani ya Tanga

Suzzy bartazaly (njano) na Zamaradi Mketema na mwisho kabisa mama lao Gea Habib wote wa leo tena ya Clouds Fm wakiwa na wasikilizaji wao mahiri kabisa wa Tanga
Wasanii wa kike waliobaki kwenye muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva,Maunda Zorro akiwa amepozi na Baby Madaha.
Wana wa mjengoni hawa,kulee Clouds Fm,Zamaradi na Antonio Nugas a.k.a Swahiba wangu
Walimbwende kutoka kundi la THT wakiwa wamepozi safi kabisa
Wasanii kutoka nyumba ya vipaji ya THT wakiwa katika picha ya pozi katika usiku wa tamasha la fista one love lililofanyika mwsihoni mwa wikend katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 26, 2009 | | Permalink | Maoni 3
Idadi ya watu