Kwa wanaopenda kwenda kusoma Malaysia

Wednesday, September 30, 2009

Kwa wanaopenda kwenda kusoma Malaysia WWSL watakupatia ushauri ni chuo gani na kozi gani ya kuchukua.Tuna uzoefu na mazingira na tunaijua Malaysia, sio kila chuo kinafaa hivyo basi tutakupatia chuo chenye ubora na elimu bora kwa gharama nzuri.Wasiliana nasi kwa address hiyo hapo kwenye tangazo au tuma mail kwa piusmicky@yahoo.co.uk
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, September 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

MAGARIBEIPOA.COM







Gari hii inauzwa Tsh 6.9M tasilimu,ni gari ya mwaka 2000,imetembea km 33000,ina kila kitu kama AC,CD player,PW,PS ,MATAIRI MAPYAna vingine vingi.Mnunuaji atatakiwa kufunga plate number na kulipia Insuarance na kuingia barabarani.
Kwa magari zaidi ya bei poa tembelea http://www.magaribeipoa.com/. pia unaweza kuuza gari lako kupitia hapa bila gharama yoyote,unachotakiwa kufanya ni kujisajilia bila gharama yoyote ili uweze kutuma picha ya gari lako.
Maajenti wa kuuza magari pia mnakaribishwa kutumia mtandao wa magaribeipoa.NOTE:lugha zinazotumiaka humu ni mbili,ukitaka kiswahili nenda mpaka mwisho wa page na utaona bendera ya Tanzania,gonga hiyo bendera kwa ajili ya Kiswahili.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii +255713439707
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, September 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

13 TANZANIAN WOMEN ARTISTS OFFERED STUDY SCHOLARSHIP TO USA

Tuesday, September 29, 2009

INTERNATIONAL NEWS RELEASE
Arts Council Lake Erie West & The Great Lakes Consortium
for International Training and Development
1700 N. Reynolds Road •
Toledo, Ohio 43615
• Toll free 877.297.6645
• 419.531.2046
• Fax 419.531.5049
FOR IMMEDIATE RELEASE September 29, 2009
Contact: Martin Nagy Cell: 419-290-0995 Office: 419-531-2046

Fatma Amor Hamad’s Fashions to Show in the United States
with Twelve Tanzanian Women Artists Selected for the
‘Arts Exchange on Women’s Issues’ with U.S. Artists
Dar es Salaam fashion designer, Fatma Amor Hamad of Famour Designs, will introduce her fashions and accessories in several shows in the United States as part of the “Arts Exchanges on International Issues with Tanzania” grant funded by the U.S. Bureau of Educational and Cultural Affairs and organized by Arts Council Lakes Erie West and Great Lakes Consortium for International Training and Development.
Twelve additional Tanzanian women artists will also travel to the U.S. from October 6 to November 3, 2009 in conjunction with the program and participate in the U.S. National Arts & Humanities Month activities.
Ms. Hamad has designed fashions for fifteen years and has been featured in numerous magazines and television programs in Africa. Most recently, Ms. Hamad presented her fashions at ‘World Women’s Day’ at ‘DarAlive’ (Kakakuona) on March 7, 2009 in Dar es Salaam.
She was crowned Miss Redd’s Ambassador 2006/2007 for her outstanding designs and was the winner at Redds Africa fashion designer awards for three consecutive years in 2005/2006/2007. Ms. Hamad’s exquisite handwork, detailed beadwork and creative ensemble embellishments have made Fatma Amour Hamad a sought after brand name in the fashion market. She continues to receive letters of invitation by other top designers in Tanzania to introduce her country theme fashions.

Ms. Hamad’s dreams of becoming an international fashion designer have come true and she will introduce her fashions at the ‘Magic of Tanzania’ fundraiser event for “Arts Exchanges on International Issues with Tanzania” in Sylvania, Ohio, USA on October 12, 2009. Twelve other Tanzanian women artists including: Harieth Bitanuzile and Miriam Mzee from Bagamoyo, Zena Walakai also from Dar es Salaam, Miriam Mussa
and Kauthar Khalfan from Zanzibar, Mefakii Jumbe and Kulthum Omary from Tanga; Maria Chuwa and Martha Ntoipo and Veronica Mushi and Regina Mfoy from Arusha, and Scolastica Malecela from Dodoma will also participate in an exhibit “Art in a Woman's World” at the Magic of Tanzania event.

Tanzanian artists will also participate in arts business development and women’s gender issues workshops, make connections with artists and arts organizations, work on joint artwork with U.S. artists while in the U.S. The artists will visit different communities in the State of Ohio (Toledo, Bowling Green, Sylvania, Fremont, Findlay, Columbus, Cleveland) and in the State of Michigan (Detroit, Ann Arbor, East Lansing and Okemos).

The Great Lakes Consortium for International Training and Development and the Arts Council Lake Erie West are regional nonprofit agencies working in collaboration on this grant program funded by the U.S. State Department Bureau of Educational and Cultural Affairs Cultural Division. WSOS Community Action Commission, Inc. is the U.S. grant contract agent and manager.

For further information about the program contact
Martin Nagy at 419-290-0995 (USA)
or Elizabeth Balint at 419-530-8572
or at glcevents@hotmail.com. (USA).
In Tanzania contact: Mlongetcha L. Mkuku at 0754 272691
or at mmkuku@yahoo.co.uk
--- END ---
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, September 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

tamasha la kimataifa la injili kurindima desemba 25



KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, imeandaa tamasha la kimataifa la nyimbo za injili, litakalofanyika Desemba 25, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama, hilo ni tamasha litakalounganisha waimbaji kutoka nchi za Kenya, Malawi, Uganda, Burundi Zambia na Afrika Kusini.

Alisema, lengo la tamasha hilo ni kusaidia watu wenye ulemavu na yatima na wengine wenye mahitaji ambao wanapaswa kusaidiwa katika jamii.

“Ujue kuna baadhi ya watu wenye ulemavu ambao wanahitaji misaada mbalimbali, kwa mfano baiskeli, hivyo kampuni yangu imeliona hilo, hivyo tumepanga kuelekeza nguvu kwa walemavu wa mikoani,” alisema Msama na kuongeza.

Fikiria kuna wengine wanatamani kusoma, lakini kwa kukosa usafiri na huduma nyingine muhimu, wanashindwa, hivyo tumeona ni vizuri kama tutawakumbuka,” alisema Msama.
Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili akiwa mwasisi wa matamasha ya injili, alisema katika tamasha hilo, pia kutakuwa na waimbaji wapya walioingia katika albamu ya Haleluya Collections Volume 5, wakiwamo kutoka Tanzania.

Msama alisema kamati hiyo imeamua kufanya matamasha mara mbili kwa mwaka ikiwa ni kufanyia kazi maoni ya wapenzi na mashabiki wa muziki huo. Kuhusu misaada kwa makundi mbalimbali ya kijamii, Msama alisema kamati yake imekuwa ikifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kusaidia wenye mahitaji katika jamii.

Alisema, kamati hiyo imekuwa ikimuomba Mungu azidi kuijalia uwezo kwani lengo ni kugawa baiskeli 100 kila mwaka badala ya 70, ilizowahi kugawa na kusomesha yatima. Mbali ya baiskeli, kamati hiyo imewahi kutoa vitanda vya wagonjwa katika hospitali mbalimbali nchini ingawa kwa kipindi hicho hawakuwa wakitangaza hadi pale waliposhauriwa kufanya hivyo.

Alisema kuanzia sasa, watakuwa wakitangaza hata mapato katika matamasha mbalimbali ili kuwa wazi zaidi, kwani hiyo pia itawajengea imani zaidi kwa jamii. Aidha, Msama ametoa wito kwa watu mbalimbali katika jamii kuguswa na suala hilo, kwani linalenga kusaidia makundi maalumu katika jamii. Sambamba na hilo, Msama ametoa wito pia kwa jamii kuunga mkono juhudi za kamati hiyo kwa kununua albamu ya Haleluya Volume 5 iliyoko madukani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, September 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

mazingira:nitunze nikutunze usiponitunza sitakutunza.!

Wanajamvini tutunze mazingira yetu,tuache kuchoma misitu yetu hovyo kama hivi pichani
Ufugaji wa wanyama hovyo hovyo pia ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira yetu,tunapaswa kuwa makini katika suala zima la utunzaji wa mazingira yetu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, September 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

wanachimba dawazzzz.!


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, September 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Ni nani kati ya hawa warembo ataibuka na taji la Redds Miss Photogenic 2009?

namba 00027
namba 00000
namba 0001
namba 0002
namba 0003
namba 0004
namba 0004
namba 0005
namba 0007
namba 0007
namba 0008
namba 0008
namba 0009
namba 00010
namba 00011 namba 00013
namba 00016
namba 00015
namba 00014
namba 00019
namba 00018
namba 00017
namba 00021
namba 00020
namba 00022
namba 00023
namba 00024
namba 00025

namba 00026


warembo 29 wa Vodacom Miss TZ 2009 wanaochuana kuwania taji la Redds Miss Photogenic 2009, katika shindano linaloratibiwa na globu ya jamii ya issamichuzi.blogspot.com na kudhamniwa na kilaji cha Redds Premium Lager.
Mshindi atapata shs. 1,000,000/- taslimu, mkataba wa mwaka mmoja kufanya kazi za umodo na kampuni inayongoza ya umodo nchini ya Beautiful Tanzanie Agency pamoja na portfolio ya ulimbwende. Mdau unaombwa kupendekeza ni nani kati yao ni photogenic ama mrembo mwenye mvuto wa picha.

Mshindi atatangwazwa October 2, 2009 siku ya fainali za Vodacom Miss Tz 2009 zitazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Conference Centre jijini Dar. Kazi kwako mdau......

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, September 29, 2009 | | Permalink | Maoni 8

ajinyakulia Nokia E-66 na tuzo, baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Gofu


Mratibu wa Gofu wa kampuni ya Illovo Ltd, Pieter Van Eeeden (kulia) akimkabidhi mcheza gofu, thian Myburgh (kulia) Simu mpya aina ya Nokia E-66 na tuzo, baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Gofu yaliyofanyika wiki iliopita katika uwanja wa gofu wa Illovo, Kilombero Mkoani Morogoro. Mashindanon hayo yalidhaminiwa na Kampuni ya Zain na kukutanisha wacheza golf mbalimbali wa mkoa wa Morogoro.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, September 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

taifa letu la kesho,nani wa kulitetea leo?

Monday, September 28, 2009

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, September 28, 2009 | | Permalink | Maoni 12

nani kasema rasta hali nyama ?!


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, September 28, 2009 | | Permalink | Maoni 3

mdau anauliza swali.!

Kumradhi wanajamvini,kuna mdau anauliza hivi ati sehemu uionayo mbele ya mlima huo wa morogoro kwanini na sisi tusiandike maandishi makubwaaaa kama vile KARIBUNI MOROGORO KASORO BAHARI kama ya wenzetu wa kule nanihiii walivyoandika maandishi ya HOLLYWOOD.! Au kuna hitajika nini mpaka mpango mzima kama huu utimie ??!!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, September 28, 2009 | | Permalink | Maoni 6

Job opportunity

Youth Action Volunteers (YAV) is a Non Governmental Organization registered in Tanzania in the year 2000. It has engaged in promoting equitable policy, service delivery, and governance in the health and HIV/AIDS sector in Tanzania.


The aim of our work is to achieve healthy and responsible young men and women with the ability to participate in their own development process, in order to realize Tanzania’s development vision 2025. The primary target group is young men and women from the ages 10 to 24.


YAV intends to enable greater social accountability within Tanzania by assessing district planning and resource allocation for the health sector and, expenditure and performance.
We are frequently seeking consultants who have experience in analytical work and the health sector.

The qualified candidate should have:
At least Masters degree in Social Science or any relevant field
Familiarity with the Tanzanian Social Accountability System
Familiarity with the Health and Local Government Budgets and Health Budget Processes
Familiarity with the context of Good Governance
Ability to analyze and draw conclusions, policy recommendations, and implications for achieving an equitable health service delivery system in Tanzania.


Interested consultants should send CV and cover letter to:
The Executive Director,
Youth Action Volunteers,
and P.O Box 12183,
Dar es Salaam, Tanzania
or by e-mail to mailto: info@yav.or.tz
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, September 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

wanafunzi wa kibasila wafunga barabara ya chang'ombe na mandela road leo mchana

Ebwanaeee.! hii kali hadi kigofu cha askari pia kilizuiwa kabisa kupita eneo hilo
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kibasila wakiwa wamelizuia lori la mafuta lisipite eneo hilo
Wanafunzi wakilizuia gari la abiria kupita kama uonavyo pichani
Kaazi kweli kweli
Moja ya kiongozi kutoka jeshi la polisi akizungumza na wanafunzi wa Kibasila leo mchana kuhusiana na maandamano yao ya kuziba barabara ya chang'ombe na mandela road kufuati ajali za wanafunzi ambazo zimekuwa zikitokea kila mara.
Kikosi cha usalama kutoka jeshi la polisi wakijaribu kubadilishana mawazo ni kitu gani kifanyike ili kuweka mambo sawa.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamewazunguka watangazaji wa televisheni ya Taifa TBC 1 ambao nao walifika kwenye tukio hilo leo mchana.


Polisi wakiwa eneo la tukio wakijaribu kubadishana mawazo nini kifanyike mchana huu,mara baada ya barabara hiyo kufungwa na wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari Kibasila
Kiongozi wa wanafunzi akijaribu kuwatuliza wanafunzi wenzake kuwa wasubiri kila kitu kitaeleweka muda si mrefu
Mmoja wa wapita njia akipokonywa piki piki yake na wanafunzi hao ambao walionekana kuwa wamecharuka na wanachokifanya,na kweli jamaa ilibidi awaachie
Malori yakiwa yamekwama kutokana na wanafunzi wa kibasila kuziba barabara hiyo leo mchana
Tuliii katikati ya barabara leo mchana
Wameamua kucheza huku wakijiimbia nyimbo zao za kuhamasisha eneo hilo lazima liwekwe alama za usalama

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari ya Kibasila wakiwa wamezuia barabarani leo mchana barabara ya chang'ombe na Mandela road

Wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari ya kibasila leo mchana wamefanya maandamano ambayo hayakupewa baraka zote na uongozi husika,na kuamua kuziba barabara za makutano ya Chang'ombe na Mandela road a.k.a Machinjioni jijini Dar kwa kile walichokidai kuwa wamechoka kupoteza maisha ya wanafunzi wenzao kutokana na eneo hilo kutokuwekwa alama ya aina yoyote .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na JIACHIE iliofika eneo la tukio mara baada ya kutaarifiwa na mmoja wa wadau wa blog hii,wamesema kuwa wamechoka kupoteza wanafunzi wenzao na ndugu zao kila baada ya siku kadhaa kwa kugongwa na magari,yote hiyo inasbabishwa na sehemu hiyo ambayo ni kiungo cha barabara nne kukota alama aina yoyote ya usalama.
Wanafunzi hao ambao baadhi yao walimua kulala barabarani ,wengine wakiwa wamekaa huku wakiimba nyimbo zao mbalimbali,walionekana kukubaliana na chochote kitakachotokea mbele yao kutokana maandamano yao kunyimwa kibari ama kupewa baraka zote ili kulitimiza leongo.
Aidha mmoja wa wanafunzi ambaye hakutaka kutaja jina lake,kidato cha tatu amebainisha kuwa wao madai yao makubwa katika maandamano hayo ni kuutaka uongozi wa serikali i.e Mkuu wa mkoa,Mkuu wa jeshi la Polisi waje eneo la tukio na kutoa tamko la wazi kabisa kwamba eneo hilo litawekwa alama za usalama lini,vinginevyo hatutaondoka hapa hata ikifika usiku wa maneno mapa kieleweke.
"Juzi Ijumaa mwanafunzi mwenzetu wa kidato cha sita amegongwa hapa hapa na kupoteza maisha,haya leo hii asubuhi wamegongwa wanafunzi wanne na mwalimu wao ambaye alijitolea kuwavusha eneo hili,lakini wakagongwa na lori,wanafunzi wawili wamefariki na wengine ndiyo hivyo wanaendelea vizuri wapo hospitali, hali hii itaendelea mpaka lini,hivyo tumeamua tufanye hivi kabla hali haijawa mbaya, na serikali itambue wazi kabisa kuwa eneo hili si salama kabisa"alisema mwanafunzi huyo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, September 28, 2009 | | Permalink | Maoni 7
Idadi ya watu