ari mpya na kasi mpya sote tujitume

Monday, August 31, 2009

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 3

mchakato wa kuwapata watangazaji wa clouds tv ulivyokuwa


Wadadazz pia walitoka chichazzz kuwania nafasi ya utangazaji clouds Tv
Walifika huku wakisubiri kuchukua fomu ili nao wakifanyiwe intavyuu.
Mchakato wa kuwatafuta watangazaji wa Clouds Tv ulifanyika kwa umakin mkubwa
Wengi walionekana kuwa na shauku kubwa ya kuingia kwenye moja ya watangazaji wa clouds Tv itakayoanza hivi karibuni jijini dar

Majaji wa intavyuu hiyo,Ncha Kali pamoja na Barbra Hassan bila kumsahau kamera man nyuma ya majaji
Baadhi yao walijiandaa vema kwenye intavyuu hiyo iliyowakusanya vijana wengi

Mmoja wa wanaowania nafasi ya kutangaza Clouds Tv
Watu walikuwepo kibao kuwania nafasi ya utangazaji ,pichani walikuwa kwenye foleni ya kufanyiwa intavyuu,ambapo mamia ya vijana walijitokeza kuwania nafasi moja ya atakayekuwa mtangazaji nambari moja wa kituo kipya ya CloudsTV kinachotarajia kuanza kazi karibuni. intavyuu hizo zilifanyika kutwa nzima mwishoni mwa wiki viwanja vya lidaz Club Kinondoni jijini Dar





Baadhi ya watangazaji wa Clouds TV wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya lidas kinondoni jijini dar
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 8

injini kiuno za kihome


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ujumbe wa leo


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

wadau wa kikapu tizini

Mchezaji wa Mpira wa Kikapu John Simkoko wa Chang'ombe Veteran, akipenya katikati ya walinzi Asha Kiluwa(kushoto) na jumanne kessa, wakati wa Mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Sigara TCC, Chang'ombe Dar es Salaam jana, ikiwa ni maandalizi ya kushiriki bonanza la timu za Veterani linalotazamiwa kufanyika mwishoni mwa mfungo wa Ramadhani.
Mchezaji wa Mpira wa Kikapu ramadhani Khalid (katikati) wa Chang'ombe Veteran, akijaribu kurusha mpira kufunga wakati wa Mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Sigara TCC, Chang'ombe Dar es Salaam leo, ikiwa ni maandalizi ya kushiriki bonanza la timu za Veterani linalotazamiwa kufanyika mwishoni mwa mfungo wa Ramadhani.

Mchezaji wa Mpira wa Kikapu John Simkoko wa Chang'ombe Veteran, akimtoka Linto Linto, wakati wa Mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Sigara TCC, Chang'ombe Dar es Salaam leo, ikiwa ni maandalizi ya kushiriki bonanza la timu za Veterani linalotazamiwa kufanyika mwishoni mwa mfungo wa Ramadhani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

wimbi la unyang'anyi wa piki piki jijini!

Katika kile kilichodaiwa unyang'anyi ama uporaji wa pikipiki jijini Dar, Askari Polisi akiwa katika upekuzi baada ya kusadikiwa kuwapo kwa wizi huo katika stendi ya mabasi Keko, jijini Dar jana,hata hivyo haikufahamika mapema kama wezi hao walipatikana kutokana na msako huo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

number 10 liko mitaani sasa


Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wote kwa maoni yenu yaliyosababisha kuliboresha hili jarida ,number 10 tunajitahidi kuwapatia burudani wapenzi wote wa soka ndani na nje ya nchi,safari hii jarida la number 10 limefanya mahojiano na beki wa zamani wa ufaransa marcel desailly, pia tumeenda mpaka south africa na kuangalia maendeleo ya maandalizi ya fainali za kombe la dunia,mambo yapo mengi kwakweli, chukua tu copy yako uone...
please please tuwasiliane kupitia info@number10.co.tz
+ 255 713 350833cheers
shaffih dauda
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

yanga ilivyoikamua manyema mwishoni mwa wiki

Baadhi ya Mashabiki wa Timu ya Soka ya Yanga wakifuatilia kwa makini pambano la ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Dhidi ya Manyema Uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru mwsihoni mwa wiki.
Hawa Mashabiki wa Soka wao kuingia kushuhudia Mpira kwao sio Insue, wakiwa nje ya Lango la Kuingilia Uwanjani, na wakati huo huo wakiendelea kubishana kutokana na matokeo yaliyokuwa yakiendelea Uwanjani.(Leo Yanga itafungwa tu na Manyema, si unaona Manyema wanavyokaza) alisikika mmoja utadhani alikuwa Uwanjani.
Winga mkabaji wa Timu ya Soka ya Yanga ,Karongo Honore, akiruka kiunzi cha Mlinda Mlango wa timu ya Soka ya Manyema, Oddo Nombo , wakati wa Mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Yanga ilishinda 3-0.


Mwamuzi Athumani Kazi, akinyoosha mkono kuashiria Penalt katika lango la timu ya Soka ya Manyema, wakati wa Mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Yanga ilishinda 3-0.

Kiungo wa Timu ya Soka ya Yanga, Athumani Idd na Kiungo wa Timu ya Soka ya Manyema, Adamu Matunga, wakichuana kuwaniwa Mpira wakati wa Mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam jana.Yanga ilishinda 3-0.

Winga mkabaji wa Timu ya Soka ya Yanga ,Karongo Honore, akiruka kiunzi cha Mlinzi wa timu ya Soka ya Manyema, Bendict Ngassa, wakati wa Mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Yanga ilishinda 3-0.

Kocha wa Timu ya Soka ya Manyema Abdallah King Kibaden Mputa(wa pili kushoto) akiwa tayari kishapewa Dozi na vijana wa Manji katika mfululizo wa michuano ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana katika Uwanja wa Uhuru ,Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.wengine katika pichani jopo zima la KAMATI YA UFUNDI LA TIMU HIYO.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Soka ya Manyema, wakiwa katika Benchi huku wakielekezana bada ya kuwa wamepata Dozi kutoka kwa Vijana wa Manji, Yanga, katika mfululizo wa michuano ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana katika Uwanja wa Uhuru ,Dar es Salaam jana

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 2

keki ya kwenye mnuso wikend

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, August 31, 2009 | | Permalink | Maoni 1

serikali yapiga marufuku maonesho ya filamu kwenye hadhara ya watu

Sunday, August 30, 2009


Na. Aron Msigwa – MAELEZO.


Serikali imepiga marufuku maonyesho yote ya filamu kwenye hadhara ya watu, majumba yasiyo rasmi,vibanda ,kumbi ndogondogo, hoteli na maeneo ya baa bila kufuata masharti ya jumba la sinema na kwa mujibu wa sheria na 4 ya mwaka 1974 inayotumika nchini.



Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu nchini ambayo itakuwa na jukumu la kukagua na kusimamia maonyesho na shughuli za filamu nchini.



Amesema sehemu nyingi zinazotumiwa kuonyesha filamu hazina leseni halali za kuonyeshea filamu na kuongeza kuwa sio salama kwa mali na afya za watu.“Nachukua fursa hii kutoa onyo kwa mtu yeyote atakayeonyesha filamu kwenye hadhara ya watu katika majumba yasiyo rasmi ,vibanda,kumbi ndogondogo,hotelini, baa na katika vyombo vya usafiri waache mara moja” amesisitiza.



Amefafanua kuwa sehemu nyingi zinazotumika kuonyeshea filamu sasa hazikidhi matakwa ya ujenzi wa kumbi za kuonyeshea filamu na ni kinyume cha sheria kwani nyingi zimekuwa chanzo cha maficho ya wahalifu, majambazi, biashara ya dawa za kulevya na kuchochea vitendo vya ngono kwa vijana.



Amesema athari nyingi tayari zimeshajitokeza katika jamii yetu na kuongeza kuwa filamu nyingi zimechangia kubomoa na kudunisha Utamaduni wa taifa letu na hata kuchangia kwa kiasi kikubwa kubomoa misingi ya amani , Upendo , Uadilifu,heshima, uaminifu na utu ambao ni utambulisho wa mtanzania jinsi ulivyokuwa umejijenga na kuenea katika jamii yetu.



Waziri Mkuchika amewataka wanaojishughulisha na shughuli za kuonyesha filamu kwa kuzingatia sheria na kufuata kanuni za nchi licha ya kuwa ya fani ya filamu kukuza ni biashara na inakuza uchumi na pia kuleta maendeleo na kuwataka kuepuka kuonyesha filamu zinachochea vitendo viovu na mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii kutokana na filamu nyingi kutokaguliwa na kupangwa katika madaraja kulingana na matakwa ya watanzania.



Awali akizungumza kuhusu majukumu ya Bodi hiyo amesema kuwa Bodi itakuwa na jukumu la kuweka misingi ya kuimarisha utaratibu wa usimamizi wa utengenezaji wa filamu na pia kutoa vibali vya kutengeneza filamu hapa nchini.Mbali na jukumu hilo Bodi ya Ukaguzi wa Filamu itakuwa na jukumu la kuratibu, kusimamia na kushauri namna ya kukuza Tasnia ya Filamu kwa kuzingatia sera ,sheria na kanuni zikiwemo taratibu na miongozo mbalimbali ya nchi hasa sera ya Utamaduni na Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza.



Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi. Rose Sayore ameihakikishia serikali kuwa Bodi yake itafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha kuwa kanuni, sheria , maadili na taratibu za uonyeshaji na utengenezaji wa filamu zinazingatiwa kwa maslahi ya watanzania na vizazi vijavyo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, August 30, 2009 | | Permalink | Maoni 7

wana nanihii wakiwa klabuni kwao



 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, August 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

hepi besidei mkuu wa globu ya jamii

Saturday, August 29, 2009

Globu ya Jamii inapenda kutoa shukran kareem kwa wote waliohudhuria futari hii ya kusherehekea hepi besdei ya anko nanihii katika hafla iliyofana sana.
Pia Globu ya Jamii inapenda kutoa asante za dhati kwa wadau wote waliotuma salamu za pongezi za siku hii ya kuzaliwa kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo FaceBook.


Ni vigumu kutoa asante kwa mdau mmoja mmoja kwa vile ni wengi mno, hivyo anko nanihii anaomba shukrani hizi ziwe kama wakala wa shukrani zake za dhati kwa wooooote waliotoa salamu za pongezi. Anawapenda sana.
Shukrani za pekee ziwaendee Tanzania Mitindo House walioandaa hafla hii ya futari na kula keki na pia Jose Mara wa FM Academia na mai waifu wake kwa kuandaa keki maalumu hiyo hapo juu.



Asanteni sana Jose, Monica na Hadija Mwanamboka pamoja na Asia Idarous kwa ukarimu wenu.Anko nanihii pia anatoa shukrani kwa bintiye Mamou pamoja na dada yake Zahra na kaka yao Maggid kwa kuungana naye kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na ndugu, jamaa na marafiki bila kuwasahau Juma Pinto na Ben Kisaka wa Jambo Leo, Kim Tenga, Da'Kabula wa TBL, Mariam Mogella na wenzie wa TSN, Saidi Tuli, Da'Mboni, na Dada Mishi wa Virago Boutique ya Namanga pamoja wote waliohudhuria.


Michuzi
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, August 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

keki ya hepi besidei ya anko nanii ikiliwa

Mie nikilishwa keki ya hepi besidei na anko nanihii
dada Shamim wa 8020fashions akilishwa keki na anko nanii
Mbunifu wa mavazi dada Farha akilishwa keki na anko naniii kwenye besidei yake





Mpiga picha mahiri wa gazeti la Jambo leobro ben kisaka akilishwa keki




Anko nanii akimlisha keki anti monica ambaye ndiye aliyeiandaa keki hiyo kwa ajili ya futari maalumu kusherehekea miaka nanihii ya kuzaliwa anko nanihii jana jioni kwenye mgahawa maarufu wa Chef"s pride jijini dar.




Mama wa mitindo Asia idarous kutoka Fabak Fashions akilishwa keki




Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House Khadija Mwanamboka akilishwa keki,khadija kwa niaba ya taasisi yao ya Tanzania Mitindo House ndiyo walioandaa hafla hiyo ya futari




Anko Juma Pinto naye alikuwepo kwenye hepi besidei ya anko nanii,pichani akilishwa keki




Daaa kumradhi ,huyu kanitoka jina (msaada tutani) pia akilishwa keki ya hepi besidei jana jioni









Dada Mishi wa Virago Boutique ya Namanga akimlisha keki anko nanihii kweye hepi besidei yake.




Lady Jay dee a.k.a binti Machozi akimlisha keki ya hepi besidei anko nanihii




Mzee wa Mtaa kwa Mtaa akimlisha keki anko nanii




Mpango mzima wa ugawaji wa hiyo keki ya hepi besidei ikipagwa sawia




Anko nanii akikata keki yake ya hepi besidei huku wageni waalikwa wakiimba ule wimbo maarufu wa siku kama hiyo.




ooohw oohww..!




Watoto wa anko nanihii wakiwa wameibeba keki ya hepi besidei




Aahh.! jamaaani si tuanze mda unaenda.




Anko naniii amkimshukuru sana anti monica ambaye ni mke wa mwanamuziki wa Fm Academia,Jose Mara kwa kuiandaa kwa umaridadi mkubwa keki hiyo ya hepi besidei.



Anko nanihii akiwa na anti Monica pamoja na jose mara pamoja na mdau wa nanihii wakiikabidhi keki hiyo iliotengenzwa kwa ustadi mkubwa huku nembo ya bwawa la maini ikiwa imetawala vyema pale juu,ama hakika ilivutia sana




Anko nanihii akiingalia kwa umakini keki yake ya hepi besidei ikiwasili
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, August 29, 2009 | | Permalink | Maoni 8
Idadi ya watu