Help! TeknoHaMa and Tanzania, can you answer some of these questions?

Saturday, May 30, 2009
A relative of mine sent me an email asking a multitude of questions, I tried to answer like 4 of them and then I gave up.
I needed some stats to back up almost everything he asked.
My apology for any repetition on some of the questions, I tried the best I could to trim them down.
Now, this is what he is looking for:
  1. What language do people in Tanzania mostly use?
  2. Do people use the internet cafe much more nowadays or is everyone not really on the internet?
  3. What do you think that everyone trying to do on the internet?
  4. Are they doing social networking Myspace? Facebook? Youtube? or creating websites?
  5. Are people usually looking for jobs on the internet?
  6. What do people do on a typical day? like college students, city folks, people with internet at home? I mean, what is their daily activity for the most?
  7. Do people listen to the news, or look for jobs? look for music online, videos?
  8. What sites are popular out there?
  9. What kind of online activity is important out there?
  10. Other than on the internet, what do people do in their regular life that uses technology?
  11. How much technology is there in Tanzania? cell-phones, laptops, pcs...
Please let me know...its for my project at school for my MASS MEDIA communication class. We are at the end of class, doing this global awareness and if I could present people with something from our Country, that would be GREAT! I want to show people in my class that our country is not just "huts" and people hunting for animals and elephants walking around. I want to tell them what exactly we do and that we are using technology and its becoming popular and that more and more people are doing it online..
Thank you very much for your time!
M.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, May 30, 2009 | | Permalink | Maoni 6

je unafahamu matumizi ya mnyaa ?

Pichani ni mti aina ya Mnyaa au kwa jina lingine unaitwa Utupa kwa kisayansi unaitwa Euphorbial Tirical,Mti huo hutumika kutibu magonjwa mbalimbali ukiwemo Ugumba,kuumwa na Nyoka,Vipele,maumivu ya koo na tumbo.Mti huu umepandwa ndani ya kijiji cha Makumbusho kama uonavyo pichani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, May 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

anaomba mchango wa mawazo!

Kumradhi Wanajamvini,kuna mdau mwenzetu ana kitambi na amekiri wazi kwamba kinampa shida na kumnyima raha kwa mambo mengi,anaomba msaada japo wa kimawazo afanyeje ili kiweze kupungua na kikipungua ni mambo gani anapaswa afanye ili aweze kukidhibiti kisirejee tena ?
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, May 30, 2009 | | Permalink | Maoni 29


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, May 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

hivi ndivyo tamasha la utamaduni wa kabila la wahangaza na washubi liliyozinduliwa leo kijiji cha makumbusho

Friday, May 29, 2009
Waziri mkuu ambaye pia alikuwa ndiye mgeni rasmi Mh Mizengo Pinda akizindua rasmi tamasha la siku tatu (kuanzia leo) la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Mh George Mkuchika akisoma hotuba fupi na pia kuwashuru baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia uzinduzi wa tamasha la siku tatu la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh Mohamed Babu akisoma hotuba fupi ya uzinduzi wa tamasha la siku tatu la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba fupi zilizokuwa zikisomwa na baadhi ya viongozi wa serikali waliofika kwenye tamasha hilo leo mchana ndani ya kijiji cha Makumbusho jijini Dar

Pichani ni wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi wa tamasha la siku tatu la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Kikundi cha ngoma za asili ya Wahangaza wakiwaburudisha wageni waalikwa leo mchana ndani ya kijiji cha Makumbusho.
Mh Pinda mara baada ya kumaliza matembezi mafupi katika banda la vitu mbalimbali kutoka kwa kabila la Wahangaza na Washubi,alikwenda moja kwa moja kwenye meza kuu,hapa alinasa kidogo kuangalia ngoma za asili ya wahangaza.
Mh Pinda akioneshwa vikapu vya asili vinavyotengenezwa na kabila la Wahangaza na Washubi kutoka wilaya ya Ngara.

Mh Pinda akioneshwa shanga za rangi mbalimbali za kiasili zilikuwa zikitumiaka na na kabila la Wahangaza na Washubi kutoka wilaya ya Ngara .
Mh Pinda akioneshwa dawa mbalimbali za kiasili zinazotumika na kabila la Wahangaza na Washubi kutoka wilaya ya Ngara,Dawa hizo imeelezwa kuwa zinaweza kutibu magonjwa mbalimbali ukiwemo kisukari,moyo,Ugumba,mapenzi,mikosi na nyinginezo.

Mh Pinda akiyatazama mahindi kwa makini yanayolimwa mkoani Kagera.
Mh Pinda akioneshwa namna pombe ya kiasili ya kabila la Wahangaza na Washubi inavyotengenezwa kutoka wilaya ya Ngara,kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Mh George Mkuchika akitazama kwa makini.
Mh Pinda akioneshwa chumvi ya kiasili iliyokuwa ikitumiwa na kabila la Wahangaza na Washubi kutoka wilaya ya Ngara,kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Mh George Mkuchika.
Mh Pinda akiliangalia zao la jimbi linalolimwa wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Mh Pinda akionyeshwa baadhi ya vyakula vya asili ambavyo hulimwa na watu wa Kagera.
Mh Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tamasha la siku tatu la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera ndani ya kijiji cha Makumbusho leo mchana jijini Dar .
Mgeni rasmi anasubiliwa azindue rasmi tamasha hilo .
Mh Pinda anabadilisha mawazo kwa muda mfupi na baadhi ya wageni waalikwa.
Mh Pinda akisalimiana na wageni waalikwa mbalimbali huku akionekana kuvutiwa na ugeni huo uliomlaki kwa shangwe mara baada ya kuwasili, shoto ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh Mohamed Babu.
Mgeni rasmi Mh Mizengo Pinda akisalimiana wageni waalikwa mbalimbali mara baada ya kuwasili, shoto ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh Mohamed Babu .
Msafara wa Waziri mkuu ambaye pia ni mgeni rasmi Mh Mizengo Pinda ukiwasili leo mchana ndani ya kijiji cha makumbusho kuzindua tamasha la siku tatu la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, May 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

leo ni siku ya utamaduni wa kabila la wahangaza na Washubi

Wanafunzi wa shule za msingi mbalimbali nao wakiwa wamejipanga na matawai ya majani kwa ajili ya kumlaki mgeni rasmi Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda leo mchana ndani ya kijiji cha makumbusho,jijini Dar
Wageni mbalimbali wakijianda kumlaki mgeni rasmi Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda katika tamasha la siku tatu la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
Eeh bwana msosi wa kabila la Wahangaza kutoka Kagera kikiwa tayari kuliwa
Njegere zikiwa tayari jikoni zinaendelea kuiva ndani ya chungu
Akina mama wa kabila la Wahangaza kutoka mkoani Kagera wakimenya ndizi na magimbi (moja ya chakula chao cha asili), katika tamasha lao ambalo limefanyika leo ndani ya kijiji cha Makumbusho,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu mh Mizengo Pinda.
Pichani ni bwawa lililopo ndani ya kijiji cha Makumbusho,ambalo hufuga samaki aina ya perege,kwa mujibu wa maelezo tuliyoyapa kutoka kwa wahusika ni kwamba ukitaka kuvua samaki katika bwawa hilo unaenda sehemu husika hapo hapo kijiji cha makumbusho,unalipia shilingi elfu moja na unapewa ndoana kwa ajili ya kuvulia samaki hao
Pichani ni mfano wa nyumba ya kabila la Wahaya ambayo imejengwa ndani ya kijiji cha Makumbusho,jijini Dar
Pichani ni wanafunzi wa shule msingi Ubungo kisiwani na mwalimu wao wakisoma maelezo yaliopo nje ya nyumba ya kabila la Wabena ndani ya kijiji cha Makumbusho leo mchana
Shule mbalimbali zilialikwa kwenye tamasha hilo la utamaduni wa makabila mawili ya Kitanzania,Pichani ni mie nikiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Msewe-Tabata wakijadiliana na kukumbusha waliyoyaona ndani ya kijiji cha Makumbusho,ambayo mengi yao hawakuwai kuyaona ama kufahamu zaidi ya kuyakuta ndani ya kijiji cha Makumbusho.
Kulikuwepo na shughuli mbalimbali ndani ya kijiji cha makumbusho siku ya leo, kama uonavyo pichani kijana mjasilia mali ajulikanaye kwa jina la Fadhili Mkude akiuza bidhaa zake mbalimbali
Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakiwa sehemu ya tukio wakimsubiri mgeni rasmi waziri Mkuu Mh Pinda katika tamasha hilo

Wadau leo mchana Waziri mkuu Mh Mizengo Pinda alikuwa anazindua tamasha la siku tatu la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera,nami nikaona ni vyema niende nikajionee mambo ya utamaduni ndani ya kijiji cha makumbusho na mambo mengine yakiwemo haya matukio ya picha mbalimbali kutoka hapo tamashani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, May 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

mfuko wa maendeleo mkoa wa rukwa wachangiwa zaidi ya bilioni 1.4

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, May 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

wabongo tunamalizwa na mengi


Mkaguzi wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Dk. Bahati Midenge akimwaga maziwa jijini Dar hivi karibuni wakati wa uteketezaji wa tani 34 za maziwa ya unga aina ya Golden Bell, kutoka China baada ya kugundulika kuwa na kemikali ya ‘Melamine’ inayosababisha maradhi ya figo kwa watoto.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, May 29, 2009 | | Permalink | Maoni 3

wanaEX BUNGE GROUPS karibuni tukutane hapa

Karibu wote kwenye group ya wana-Bunge PS!
Here is the group's description:
A meeting point of all former pupils of Bunge Primary School---Dar es salaam!
----------------------- Google Groups Information ----------------------
The owner of the group has set your subscription type as "Email", meaning that you'll receive a copy of every message posted to the group as they are posted.

Visit this group on the web by using this URL:
http://groups.google.com/group/ex-bunge?hl=en
You can unsubscribe from this group using the following URL:
http://groups.google.com/group/ex-bunge/unsub?u=MccAuggAAADfAmhCx2FjXNGOlU-7_2eO&hl=en
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, May 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU ADELINA MAPANGO

ILIKUWA SIKU,WIKI,MIEZI NA SASA UMETIMIA MWAKA TANGU BWANA ALIPOKUCHUKUA MPENDWA WETU MAMA ADELINA MAPANGO (Mama CHAHALI).PENGO ULILOTUACHIA HALITOZIBIKA MILELE.

KINACHOTULIWAZA NI MAPENZI YA BWANA.JAPO SIE TULIKUPENDA,LAKINI YEYE ALIKUPENDA ZAIDI,NA NDIO MAANA AKAKUCHUKUA SAA4.30 USIKU WA TAREHE 29/05/2008.JAPO HAUKO NASI KIMWILI,LAKINI TUKO SOTE KIROHO.

KWA NIABA YA FAMILIA YA MZEE PHILEMON CHAHALI,NACHUKUA FURSA HII KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WOTE WALIOSHIRIKIANA NASI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA SALA/DUA WAKATI TUNAMUUGUZA MAREHEMU ADELINA,NA SAPOTI MLIYOTUPATIA KUTUFARIJI BAADA YA MSIBA.BWANA AWABARIKI SANA.

BWANA ALITOA,BWANA ALITWAA.JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE,AMEN. PUMZIKO LA MILELE UMPE EE BWANA,NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE.APUMZIKE KWA AMANI.AMEEN

Evarist Chahali
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, May 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

miss kibaha kupatikana kesho kibaha-kontena

Thursday, May 28, 2009

Kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Kibaha 2009, ambaye atapata nafasi ya kushiriki mashindano ya kumtafuta Miss Pwani,kinatarajiwa kufanyika kesho kwenye Ukumbi wa Kontena uliopo Maili Moja Kibaha mkoani Pwani. Pichani ni baadhi ya warembo wanaotarajiwa kuchuana vilivyo hapo kesho wakiwa katika pozi. Kutoka kushoto ni Rose Bahai, Miriam Juma na Benina Erio.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, May 28, 2009 | | Permalink | Maoni 1

miss kigamboni kurindima jumamosi hii maeese beach resort

Samira Kafunda
Karen Lukule
Ashura Kimbengele

Clara Mwangamila
Aziza Ally
Josiane Nadola
Rhoda Enock
Sarah Lesta
Irene Christopher
Pichani ni washiriki wa miss kigambo wakiwa katika pozi leo asubuhi jijini Dar katika mgahawa wa Hadees jijini Dar .



Mashindano ya urembo ya kumsaka kisura wa kitongoji cha Kigamboni 2009 kupitia Kampuni ya Bongo5 Media Group,imefikia ukingoni kwakuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya May 30 kwenye ukumbi wa Maeese Beach Resort zamani Hunters beach Kigamboni.Washiriki mbalimbali wamejitokeza kushiriki mashindano hayo na mpaka sasa jumla ya walimbwende 11 watachuana vikali kuliwania taji hilo la Miss Kigamboni 2009,aidha katika mashindano hayo burudani itapambwa na THT Odama band,Mwasiti,Maunda Zorro,Barnabas pamoja na Pipi.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, May 28, 2009 | | Permalink | Maoni 5

SEEWEAR STYLE NA VITU VYA SUMMER


TEMBELEA SEEWEAR STYLE STORE ITALY AU WASILIANA NA SEEWEAR KWA MANUNUZI YA JUMLA NA REJAREJA :KWA MAWASILIANO NA SEEWEAR STYLE TEMBELEA HAPA: http://www.seewear.blogspot.com/
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, May 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu