rais jakaya kikwete atembelea waathirika wa mabomu mbagala

Thursday, April 30, 2009

Rais Jakaya Kikwete akimpa pole mtoto Mariam Isihaka(8) aliyelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke baada ya kuathirika kwa mshtuko kutokana na ajali iliyotokea katika ghala la kuhifadhi silaha katika kambi ya jeshi huko Mbagala jijini Dar jana mchana.Pembeni aliyeketi na Mtoto Miriam ni mama yake Husna Selemani mkazi wa Mtoni Mtongani, jijini Dar.Kwa picha zaidi nyuti hapa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

mr blue atimkia dubai kuendeleza libeneke


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mr. Bluu au 'Mapozi', ametimka jana mchana jijini Dar kuelekea Dubai ambako atapiga shoo mbili. Blu, ambaye hivi sasa anatesa na singo yake kali ya Tabasamu, amekwenda nchini humo kwa mwaliko maalumu wa Hamilton Gulf International na anatarajiwa kufanya makamuzi makubwa. Kushoto ni meneja wake Tippo Athuman ambaye ndiye mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions ya hapa jijin Dar na Mwanza
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

send off party ya sister Joan yafana usiku wa kuamkia leo

Bibi harusi mtarajiwa akiserebuka na wageni waalikwa usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa daimond VIP hall
Wenyewe wakichat huku bibi harusi mtarajiwa akitoa tabasamu laini
Kwa pamoja wamepozi,wamesimama kuonesha heshima kubwa mbele ya wageni waalikwa kwa kufika ukumbini hapo na kuifanikisha shughuli nzima
Wageni waalikwa wakijiachia taratiiiibu kwa raha zao ukumbini
Bibi harusi mtarajiwa na mpambe wake wakiwa wamepozi pamoja na kamati kabambe ilioandaa shughuli nzima ya sister Joan
Bibi harusi mtarajiwa na mpambe wake wakiwa wamepozi na wadogo zake bibi harusi mtarajiwa
Bibi harusi mtarajiwa na mpambe wake wakikaka keki ya upendo na amani
Bibi harusi mtarajiwa Joan akizungumza maneno machache mbele ya wageni waalikwa
Wadada warembo wakifungua shampeni ikiwa ishara ya upendo mkubwa kwenye hafla hiyo huku bibi harusi mtarajiwa na mpambe wake wakideku kwa jamu hivi.
Wageni waalikwa kibao kwenye send off party ya sister Joan Rachel iliofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa diamond VIP hall
Pichani kulia bibi harusi mtarajiwa Joan Rachel Kitunga akiwa amepozi na mpambe wake
Pichani ni sehemu alioketi bibi harusi mtarajiwa Sister Joan pamoja na mpambe wake
Usiku wa kuamkia leo ndiyo ilikuwa siku rasmi ya send off party ya sista Joan Rachel Kitunga iliofanyika ndani ya ukumbi wa Daimond VIP hall,hafla hiyo iliyofana sana ukumbini humo ilikuwa na wageni waalikwa wa kutosha kabisa.
Ukitaka mawasiliano ya mpambaji na keki gonga namba 0786 000 377,na piaaamm ukitaka picha za aina mbalimbali zikiwe za send off,harusi,kitcheni party na matukio mengine wala usisite bonyeza tu namba 0713 422 313 au 0783 422 313 au kwa barua pepe
Karibuni sana
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

Bongo bwaana walahi inatia raha.!








Bongo bwaana walahi inatia raha kweli kweli na wenyewe aakah tumeizoea.! Pichani ni kamvua ka muda mfupi tu kamenyesha jijiniDar,picha hizi nimezinasa maeneo tofauti tofauti barabara ya Old Bagamoyo,nadhani kuna haja kubwa kwa manispaa ya kinondoni kuitupia jicho la kutosha na kwa mapana hii barabara,kwani imekuwa kero kubwa wakati wa mvua,Mitaro mingi imeziba kwa kujaa uchafu uliokithiri,pia baadhi ya watu wamekuwa kitapisha vyoo vyao wakati wa mvua na kupelekea hali kuwa mbaya zaidi,mfano leo mchana maeneo ya mikocheni B ni balaaa.!maji machafu yamejaaa halafu yananukaa.!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

bongo bila kujituma kisawasawa mambo hayawezi kuwa mswano


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Asante kwa kuwa sehemu ya Maisha Plus

Kwa kutazama kwako vipindi vya Maisha Plus, kusoma habari zinazolihusu shindano na kutoa maoni, moja kwa moja ulikuwa sehemu ya Maisha Plus.

Timu nzima ya Maisha Plus inakushukuru wewe kwa kuchukua muda wako na kulifuatilia shindano hili, hii ndiyo ilikuwa sehemu kubwa ya mafanikio yetu kwa kuwa tulikulenga wewe.
Kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili umekuwa nasi bega kwa bega kutuunga mkono katika hili, tunautambua mchango wako kwa kuwa wewe ni sehemu ya shindano hili.

Tunamshukuru mungu kwa kuweza kulifanya shindano hili kuwa kubwa na lenye mafanikio na zaidi ya yote limekuwa sehemu ya kuwajenga na kuwaburudisha Watanzania.
Mwisho wa msimu huu ndio mwanzo wa maandalizi ya shindano la msimu ujao, tunaamini utakuwa na subira ukiwa na imani na sisi kuwa tukuandalia kitu kingine kizuri na chenye manufaa.

Mungu akubariki kwa sehemu ya mafanikio ya Maisha Plus.
regards unaweza kuendelea kupata habari mpya za maisha plus kupitia mtandao wetu wa maishaplus.g5click.com

Regards

Julieth Kulangwa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Ghala la silala lalipuka; Dar yatikisika (KLHN International)

Milipuko mikubwa ya mabomu imetokea leo huko Mbagala katika ghala ya silaha ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, milipuko ambayo imesababisha wasiwasi mkubwa kwa wakazi wa Jiji la Dar na vitongoji vyake.

Habari za awali zinasema kuwa milipuko hiyo siyo jambo la mazoezi bali ni ajali. Hadi hivi sasa idadi taarifa za awali zinasema watu watatu wamekufa na wengine wengi kujeruhiwa na kukimbizwa kwenda hospitali ya Temeke na hospitali nyingine za jirani. Taarifa za awali za kijeshi zilitoa wito kwa wananchi walioko ndani ya usawa wa kilomita 25 kuhama maeneo yao na muda mfupi uliopita Naibu Waziri wa Ulinzi Bw.

Emmanuel Nchimbi amerudia wito huo kupitia ITV na kuwataka watu waliokuwa kwenye majengo marefu kuteremka. Milio na mtikiso wa mabomu hayo umesikika hadi maaeneo ya Msasani upande mwingine wa Jiji la Dar huku maofisi na maeneo ya makazi baina ya pande hizo mbili yakiwa katika hali ya wasiwasi, na watu wakipata na mshtuko.

Kufuatia mlipuko huo Polisi wametoa maelekezo kuwa mtu yeyote akiona kifaa cha chuma ambacho kimeangukia kwenye nyumba yake au eneo lake asijaribu kukihamisha bali kutoa taarifa Polisi kwani kuna mabomu mengine yamerushwa katika mlipuko huo lakini bado hayajlipuka.

Vivyo hivyo, serikali imeahidi kuwahudumia bure wale wote ambao wamejeruhiwa katika mlipuko huo na kusaidia katika kukarabati makazi ya wale ambao nyumba zao zimeharibiwa kufutia mlipuko huo mkubwa. Vyanzo mbalimbali vya habari vinadokeza kuwa wengi wa waliojeruhiwa ni pamoja na watoto wa shule ya Msingi ambayo iko jirani na eneo hilo na wakazi ambao nyumba zao zimelizunguka ghala hilo.

Juhudi za uokoaji na udhibiti wa hali zinaendelea kukiwa na ushirikiano kati ya Jeshi la Wananchi, Polisi na vyombo vingine vya usalama pamoja na vyombo binafsi vya uokoaji kama Ultimate Security. Jiji la Dar ambalo lina wakazi karibu milioni tatu lina kituo kimoja tu cha Uokoaji na haijulikani kama Jeshi la Wananchi wa Tanzania linakituo chake cha Zimamoto kwani katika eneo la Dar na Pwani Jeshi hilo lina kambi mbalimbali, mahospitali pamoja na vikosi vingine mbalimbali.

Kwa upande wa JWTZ, kuna wanajeshi ambao wamekufa kishujaa katika jitihada za kukabiliana na mlipuko huo ili kuzuia mabomu yasidhuru jamii zaidi. Kwa hesabu yoyote leo itakuwa ni siku ya majonzi makubwa kwa Taifa kwani idadi ya waliokufa inaweza kuwa kubwa sana na ya wale waliojeruhiwa kupita hata ukadiriaji wa haraka.

Madhara kwa nyumba na vitu mbalimbali inakadiriwa kupitia mabilioni. Tunaombea hilo halitakuwa hivyo vumbi zima likishatulia. KLHN na wasomaji wake wote tunaungana na serikali kutoa wito kwa wananchi kufuata maagizo yote yanayotolewa na vyombo vya usalama wakati huu na kuhakikisha kuwa wakati kama huu kama kitu kimoja tunaweka tofauti zetu pembeni na kuhakikisha tunasaidiana.

Tusimame pamoja na kuzuia uporoji wowote ambao unaweza kutokea kwenye nyumba za wale walioathirika na tusikubali watu wachache watumie tukio hili kama nafasi ya kufanya uhalifu. Tunatoa taasisi mbalimbali ambazo zinauwezo kuanza mara moja kutoa misaada ya kiutu kusaidia wale wote walioathirika, kujeruhiwa au kupoteza vitu mbalimbali kwani tukio hili japo tutajua zaidi chanzo chake hapo baadaye ni msiba wa taifa letu na kimguse kila mmoja kama tulivyoguswa na mambo ya kipuuza ya zeutamu! Hili ndilo tukio la kutuunganisha Watanzania wote wakati huu na mambo ya nani awajibike au asiwajibike yaje baada ya kuhakikisha kuwa hali imerudishwa katika usalama, waliojeruhiwa wanajulikana na hatua madhubuti zimechukuliwa kuhakikisha usalama wa eneo hilo.

Kutoka hapo, ndipo sauti zetu zipae juu ya jinsi gani tukio hili lingeweza kuzuiliwa kwani wengine tuliandika mambo haya karibu mwaka mzima kwa sababu tunaamini Jiji la Dar limekaa katika hali ya majanga makubwa sana. Na hili yawezekana ni dokezo tu. Tutasema zaidi baadaye. Tunawaombea rehema wale waliopoteza maisha yao, unafuu na uponyi wale waliojeruhiwa na ujasiri na moyo wa kujitoa zaidi kwa wale ambao wanasimama kuhakikisha usalama wa Taifa letu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

simbasportsclubfuns hewani sasa


Mambo vp?!Kaka naomba ututangazie blog yetu mashabiki wa Simba Sc, inaitwa http://www.simbasportsclubfuns.blogspot.com/. Ni maalum kwa ajili ya mashabiki kubadilishana mawazo na kushauriana na hata kutoa maoni kwa uongozi.

Ka Kazi njema mkuu

Alfred!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, April 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

karibuni wadau kwa pamoja tuwe cheche

Wednesday, April 29, 2009

sisi wanafunzi wa chuo cha ustawi wa jamii dar es salaam fani ya ustawi wa jamii tumeanzisha blog yetu kwa ajili ya kukutana na kubadilishana mawazo na jamii nzima kwa ujumla jinsi ya kuistawisha jamii yetu.
Hivyo tunaomba utuwekee blog yetu kwenye orodha za blog zako, link ya blog yetu ni http://www.socialworkertz.blogspot.com/ Tunatanguriza shukrani.
wako,Sadath Yahya kny, social worker tanzania,
p.o.box 3375,
Dar es salaam.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Mbagala rangi tatu hali bado ni tete

Taarifa rasmi kuhusiana na kulipuka kwa mabomu huko Mbagala rangi tatu,nje ya jiji la Dar zinasema kuwa wakazi wote walioko kwenye vikwangua anga katikati ya jiji la dar na jirani ya tukio wanatakiwa kukaa mbali ama kuondoka kabisa kwani hali ya eneo la tukio bado ni tete,na kuwa baadhi ya watu wamepoteza fahamu wakiwemo watoto wakiwa katika hali mbaya kutokana kukosa hewa,Aidha juhudi za kuwakoa watu hao imekuwa ngumu kutokana na mazingira ya eneo hilo kuwa tata,kwamba hata magari kushindwa kupita badala yake waathirika wamekuwa wakibebwa kwa namna moja ama nyingine ikiwemo kubebwa kwa mikono
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

tigo yatoa ufadhili shirika lisilo la kiserikali la codert

Afisa uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando (kati) akizungumza na waandishi wa habari Dododma jana, kuhusu ufadhili wao kwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Community Development Relief Trust(CODERT) kusaidia uanzishwaji wa miradi ya kuweka na kukopa kupitia vikundi vya kijamii katika kata nne za wilaya za Dodoma. kushoto ni Gabriel Landa,Meneja mauzo wa kanda ya kati na Isaka Wilegi, Mkuu wa miradi ya Shirika hilo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

breeekiiinnnngg newzzzzzzz.!

Pichani ni baadhi ya wafanyakazi wakitoka nje ya maofisi yao mara baada tikisiko kubwa kupita kwenye majengo yaliopo katikati ya jiji leo mchana,ambako kumezuka tafrani na hofu kubwa ya kila mmoja kutaka kukimbilia anakokujua yeye,wengine wakidai ni tetemeko la ardhi wengine ni mlipuko wa mabomu huko mbagala.

Watu wakitoka katika maofisi yao kwa vurumai kubwa mara baada ya kupita kwa mtikisiko wenye kishindo kikubwa katika maeneo mengi ya jiji la dar mchana huu.

Kila mtu alitoka nje ya jengo la JM Mall kutaka kujua ni kitu gani kinaendelea huko nje,bila ya kupata jibu lililo sahihi,maana wengine wanasema ni tetemeko la ardhi linapita,wengine wanasema kuna mabomu yanalipuka huko maeneo ya Mbagala ,nje kidogo ya jiji la Dar..
Kwa taarifa zilizotufikia hivi sasa kwa njia ya simu kutoka kwa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio anasema kuwa chanzo cha mtikisiko huo kutokea katikati ya jiji na kwingineko imetokana na Mabomu ambayo yamelipuka katika kambi ya jeshi ya Mbagala na kusababisha tafrani kubwa kwa wakazi waishio jirani na eneo hilo.
Shuhuda huyo ambaye amekana kutaja jina lake, amesema kuwa kufuatia milipuko hiyo ya mabomu mtu mmoja mpaka sasa amepoteza uhai wake na nyumba moja kuteketea kwa moto na watu kadhaa kuzimia kutokana na moshi mkubwa uliokuwa umetanda eneo hilo, ameongeza kuwa kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiendelea hapo Magari ya zima moto yamekuwa yakifanya kazi ya ziada kuokoa baadhi ya watu walioathirika kwa namna moja ama nyingine ikiwemo pia na kusaidia kuzima moto.
Tutaendelea kutaarifiana zaidi kwa kitakachokuwa kinajiri...!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

kweli ualimu ni wito?


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 4

nani mkali ?

Rose Muhando
Christine Shusho

Wadau kuna mpambano mkali unaendelea hapa ndani kati ya mwanamuziki Rose Muhando pamoja Shusho kwamba nani mkali ama nani zaidi,ukitaka kupiga kura ingia hapa .Unachotakiwa kufanya ni kupiga kura yako kwa mwimbaji unayeona nyimbo zake zina ujumbe zaidi, huku ukizingatia mpangilio wa sauti na kutawala jukwaa. Kwa sasa Shusho anasumbua na wimbo wake wa ‘Unikumbuke’, wakati Muhando anatesa na ‘Nibebe’. Kazi kwako kumpigia kura mwimbaji unayeona ni zaidi ya mwenzake!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 25

OFFICIAL BONGO AFTERPARTY IN HOUSTON


TETEMESHA ENTERTAINMENT IKISHIRIKIANA NA SHWARI DOT COM, WANAKULETEA 'THE HOUSTON OFFICIAL BONGO AFTER PARTY'.
USIKU WA KUJIDAI NA KUCHEZA NGOMA ZA UKWELI KUTOKA KWA MA DJ WA UKWELI, WALE WAPENZI WENYE KIU YA KUCHEZA NA KUSIKIA BONGO FLAVA, OLD SKUL ZA KUANZIA 80's, 90's, 2000's, BOLINGO NA BAKULUTU ZA KUFA MTU BILA KUSAHAU 'NYU SKUL, SASA NDO WAKATI UMEWADIA, NI NDANI YA CLUB ADDIS ABABA (restaurant) ILIOPO NDANI YA HOUSTON

MAHALI : CLUB ADDIS ABABA

ADDRESS: 7668 DE MOSS DR, HUSTON TX 77036

DATE : 2nd MAY

COVER: $ 10 GUYS & LADIES FREE TILL 1:00 PM

TIME: DOORS OPEN FROM 11 PM

DJ KAYCEE a.k.a THA POST & DJ ISSAR (PEOPLES CHOICE)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

bongo inazidi kuwa tambarareee


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Coming Soon to Dar-es-Salaam!


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 2

Watajeni hata vigogo - alisema Lowassa


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, April 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

wanafunzi bora tz nao kuneemeka na tuzo za heshima

Tuesday, April 28, 2009
Profesa,Wakali Kwanza,Tundaman kusindikiza tuzo za Wanafunzi bora TZ.

Hii ni kwa mara ya kwanza kabisa nchini kushuhudia tuzo za elimu zikitolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye ngazi za shule za msingi pamoja na sekondari na katika utoaji huo wa tuzo wanamuziki mbalimbali ambao ni Profesa Jay,QJ na Makamua,Tundaman,Spark pamoja na kundi zima la Bongo Dar-Es-Salaam wakiwemo kusindikiza utoaji wa tuzo hizo mwezi ujao ndani ya viwanja vya Leaders.

Tumezoea kusikia tuzo zinatolewa kwa wanamuziki bora,waigizaji bora wachezaji bora na tuzo nyingine mbalimbali lakini kwa hapa nchini hatujawahi kusikia tuzo zinatolewa kwa wanafunzi bora nchini lakini kwa mara ya kwanza PTECHS inakuletea tuzo kwa wanafunzi bora nchini ambazo zitakuwa na lengo moja kuu na la muhimu la kutaka kuwapa moyo wanafunzi ili waweze kufanya vizuri na kuinua elimu nchini.

Mmoja wa waandaaji wa tuzo hizo za elimu,Godfrey Maginga alisema kwamba yeye pamoja na wenzake waliweza kukaa chini na kujiuliza maswali kwanini kila siku zinaibuka tuzo mbalimbali na elimu inakuwa inapewa kisogo na ndiyo maana wameamua kuchukua uamuzi wa kuandaa tuzo hizo maalumu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Tanzania.

"Kila siku tunasikia tuzo kwa wasanii mbalimbali lakini hata siku moja hatujawahi kusikia tuzo kwa wanafunzi ambao ni kizazi chetu cha kesho hivyo ndiyo maana tuliamua kuandaa tuzo hizi za wanafunzi wanaofanya vizuri nchini"Alisema Godwin Maganga.

Akielezea kuhusu mchakato mzima wa tuzo hizo,msemaji huyo alisema tuzo haziwezi kutolewa bila ya burudani yeyote ile hivyo kusindikiza utoaji wa tuzo hizo wameamua kuwaalika wanamuziki mbalimbali ambao nao watahamasisha wanafunzi kushiriki mashindano ambayo yanawapelekea kupata tuzo hizo pamoja na burudani.

Bongo 5 iliweza kuongea na baadhi ya wanamuziki hao ambao watatoa burudani siku hiyo na walisema kwamba ni moja ya changamoto ambayo itaweza kuamsha juhudi za wanafunzi nchini kufanya vizuri mashuleni.

"Kwakweli ni moja kati ya tuzo ambazo zitawapa mwamko wanafunzi wa kusoma kwa bidii ili waweze kupata tuzo hizo"Makamua.

Naye Profesa Jay,mzee wa mitulinga alisema kwamba tuzo hizo ni moja kati ya tuzo zinazotakiwa kupewa heshima zake nchini kwakuwa ni moja kati ya tuzo ambazo zinaweza kuibua viongozi wa kesho.

Tuzo hizi zinatarajiwa kutolewa may 23 ndani ya viwanja vya Leaders.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, April 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ALI KIBA AKIWA NA WADAU WA ITALY JUMAPILI BAADA YA SHOW






ALI KIBA AKISAINI CD KWA MDAU










ALI KIBA,LADY JUDY & PROMOTER RICKY B.





PROMOTER CHARLES G. KATIKA AFTER PARTY JUMAPILI
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, April 28, 2009 | | Permalink | Maoni 2

wana wa leo tena ndani ya clouds fm

Watangazaji mahiri wa Clouds Fm 88.4 kupitia kipindi cha Leo Tena kinachorushwa kila siku ya jumatatu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana.Kutoka shoto ni bibie Gea Habib ambaye anakamua kipande kiitwacho heka heka,kati ni Zamarad Mketema ambaye anafanya kipande cha Bongo Movie pamoja na mama lao anaendesha kipindi kizima cha Leo Tena, Dina Marious wakiwa wamepozi na mwana wa Clouds Mwingine aitwaye Athuman a.k.a Suka
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, April 28, 2009 | | Permalink | Maoni 7

Kwa Mawasiliano: + 225 773 777 550
+255 773 467 467
+255 713 267 267

Karibuni sana
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, April 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu