kila la kheri na maisha marefu

Tuesday, March 31, 2009
Rais Jakaya Kikwete akilimsha keki (fest lady ) Mama Salma Kikwete kwa kutimiza miaka yao 20 ya ndoa.Jiachie inawapa hongera na kuwatakia maisha marefu na Mungu awaongoze na kuwalinda vyema katika shughuli zenu za kila siku zikiwemo za kujenga wa Taifa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

wasanii wa tht ni somo kwa wasanii wengine

Barnaba na Pipi wakiwa wamepozi mbele ya kamera ya Jiachie.Barnaba amekwisha kamilisha nyimbo kadhaa kwa ajili ya albamu yake ya kwanza ambayo bado hajaipa jina,nyimbo hizo ni kama vile Njia Panda ambao uko hewani hivi sasa, Kodi Manga, Nivumilie, Huruma, Shemeji pamoja na nyingine nyingi.Barnaba pamoja na uwezo wake mkubwa wa kuimba pia anapenda kuwa mmoja kati ya waandaaji wa muziki hapa nchini na kutambulika kama Felegora ama Bilia Bell.

Baadhi ya wasanii mahiri kutoka kituo cha THT a.k.a Nyumba ya vipaji wakionesha umahiri wao kwenye moja ya maonyesho yao hivi karibuni.Wasanii kadhaa sasa kutoka THT wamekuwa wakifanya vizuri katika anga ya muziki huu wa kizazi kipya,kiukweli ni vijana wadogo lakini wanaonyesha juhudi kubwa katika kufanya vizuri,mfano Mwasiti ametoka vyema,Marlow nae anafanya vizuri na sasa ni zamu ya Barnaba na Pipi ambao wametoka na wimbo wao mpya uitwao njia panda ambao kiukweli umekamata ile mbaya kwenye vituo kadhaa vya redio hapa bongo.Kimsingi wasanii wa THT ni mfano wa kuigwa hata kwa wasanii wengine wa hapa bongo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

mambo ya House Of Glamour Spread haya.!

Other Products at House of Glamour
40ft x 100ft Marquee - Green and Gold deco

40ft x 100ft Marquee - Red deco outside


Clear Span Marquee at Bongo Fiesta 1



Clear Span Marquee at Bongo Fiesta

Wakodishaji wa Mahema, Viti, meza, bouncy castles, red carpet n.k; tupo Dar es Salaam, Tanzania.
Mahema yetu ndio yanaongoza kwa uzuri na ubora; kama yalivyoonekana kwenye shows za Mbiliabeli, Fat Joe, Joe Thomas, Bongo Fiesta; na list inaendelea.
Kwa bei poa na huduma nzuri, Wasiliana nasi kupitia
Simu Namba:
+ 255 788 90 5001
+ 255 715 90 5002
Au ingia kwenye tovuti yetu
www.houseofglamourtz.com
House of Glamour Hire means Business and Always Deliver!!
Or your money back!!!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

DALLAS IS BACK WITH A SWAGGER!!!!!!!




The Dallas Easter Extravaganza




Friday 8pm till down




East Africa Concert




Kwa mara ya kwanza show itakayojumuisha wanamuziki wanaokuja juu kwa nguvu kutoka Tanzania, Kenya, Burundi na Sudan. Dj maarufu kutoka Kenya TakeOver djs watakuwepo pia kuhakikisha unapata burudani ya uhakika..Usikose. .




Saturday 2pm to 8pm:




The Kids All Star Event/Family Day.




For the 1st time this year we are hosting an event for kids of all ages. We are encouraging you to come and bring the children to this event. Kids will meet and enjoy others like never before.




Songs and Games (chei chei, maua, mazuri, etc).




Physical (Music, Bouncer, Ready, Kamba, Mbio, etc).




Educational (Quizes, Information, etc).


Picture taking (to be featured on the 2010 Calender).


Final Presentation, Announcements, Raffle and Gifts.


Saturday 10pm till down: Wale magwiji wawili wa kupiga disco kutoka Tanzania Dj Bonnie Luv na Dj Joe Catdaddy (Washington D.c) watakuwa jukwaani kutoa burudani ya mwaka…Old skul vs New Skul nani zaidi usikose!!!!!!!!!!!!!! Pia kutakuwa na onyesho maalumu kutoka kwa vijana machachari wa hiphop kutoka Washington DC



....... Sunday 1pm – 8pm



PICNIC at the park..



Music and Dj Skills by local and guest djs. Expect Suprizes.



BBQ, chips mayai, nyama choma, fish, etc.



A hang-out at one of the local night club.


Please keep checking this more info is still under way.




KARIBUNI WOTE.....
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

MCHONGO KWA WAANDISHI WA HABARI

Online Course in Science Journalism (FREE)

An online course in science journalism that covers major practical and conceptual issues in science journalism has been launched in English, French and Arabic by the World Federation of Science Journalists in close cooperation with SciDev.Net, the London-based Science and Development Network

The course was designed for use by professional journalists, journalism students and teachers. It consists of eight lessons on topics including: how to find and research stories, exposing false claims, how to pitch to an editor, turning crisis reporting to advantage and more.
Each lesson consists of an e-lecture with examples, self-teaching questions, and assignments.
To learn more and to get started, go to http://www.wfsj.org/course/
SOURCE: CLICK HERE MAKULILO Jr, www.makulilo.blogspot.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, March 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Benz Deep Blue inauzwa

Monday, March 30, 2009

Wadau popote mlipo Kuna Benz C200 Kompressor, rangi ni Deep Blue na aina za taa ni ile wanaita namba NANE ( kama inavyoonyesha picahani juu).

Country of Origin: Germany
Year :2000.

Bei ni Tsh 23,000,000, ngoma iko mma kabisa, wasiliana nami kwa namba 0786 142 617

Imeingizwa Feb 2009 toka Japan na Imelipiwa ushuru wote.

Natanguliza Shukurani
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 30, 2009 | | Permalink | Maoni 7

hivi ndivyo shangwe albam ilivyozinduliwa mjini mbeya

Ebwanaaae.! Pichani nilikutana na wadau kutoka chuo Mzumbe,kulia ni Rehema,Mdau wa kutoka Dar Cathbert Kajuna,Irene ,Mie,Amina pamoja na swaiba.Haya Wikiend ijayo tukutane ndani ya Moro halafu tuone wadau au sio.PAMOKO
Dj wa Clouds FM Mully B aliyekuwa akikamua mbaya kwenye mashine akiwa amepozi na kichwa kingine mahiri katika safu ya utangazaji ya wana wa Clouds B 12 wakishangaa mmoja wa washabiki alipopandisha mzuka wa kucheza kiaina
Wasanii wa kizazi kipya kutoka mjini Mbeya waitwao Isanga Family wakiwa jukwaani na mabegi yao kama wasafiri halafu wamekosa nauli,lakini wamejiandaa kwa safari
Mdau kutoka kijiji cha Isanga mbeya nae hakutaka kuyamis matukio ya shangwe ndani ya Dhandoo,alirekodi taratiiiibu
Prof Jay akicheza na moja ya shabiki wake jukwaani kupitia wimbo wake uliowahi kutamba sana hapa bongo uitwao Zali la Menatal
Prof Jay akiwarusha wakazi wa Mbeya vilivyo,na pasi hiyana walijiachia ile mbaya

Prof Jay akiwauliza wakazi wa Mbeya waliofika kwenye uzinduzi wa Albamu ya Shangwe ndani ya Dhando wanataka nini

Watu walikuwa kibao ndani ya Dhando hall,kwa aliyekosa shangwe za uhakika shauri yake
Dj Choka akifanya vitu vyake kwenye mashine kabla ya Prof Jay hajapanda jukwaani

Moja ya wasanii mahiri katika makamuzi ya hip hop hapa bongo,Mangwea akiwarusha wakazi wa Mbeya hivi karibuni
Kulikwepo na shangwe za kila aina Jukwaaani kama uonavyo pichani mdau
Nature akiimba moja ya wimbo mpya uliopo kwenye albamu yake ya Tugawane umasiki ambayo iko sokoni kwa sasa, uitwao Afrika nambari one

Agghaa, aaghaaaa, aghaaa..Waali Naziii!!Juma Nature akiangusha moja moja kwa staili ya kipekee kabisa,Nature aliwakonga vilivyo wakazi wa Mbeya
Rich One na Juma Nature wakishambulia jukwaa kwa vina mbele ya umati mkubwa uliofika kushuhudia uzinduzi huo wa aina yake mjini mbeya
Kundi Wanaume Halisi TMK likiongozwa na Juma Nature aliyezindua albamu yake ya tugawane umasikini hivi karibuni, wakijiachia vilivyo jukwaani mbele ya washabiki wao ambao walionekana kuvutiwa mno na staili mpya ya Wanaume Halisi.Pichani kulia ni Dollo na Juma Nature akijiduarisha na moja ya wimbo wao uliopo kwenye mahadhi ya mchiriku
Pichani ni mtangazaji wa Clouds Fm B 12 akiiinadi albamu ya Shangwe kwa washabiki wa Mbeya, ambao kwa asilimia kubwa waliikuwabali albamu hiyo yenye CD mbili,kwamba imesheni nyimbo murua kabisa,ambapo mtu akiinunua basi atakuwa amefaidika kwa kiasi kikubwa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

kamuzi la shangwe tour albamu mjini mbeya

Feroouz na akimdis Mr Policeman mbele ya wakazi wa Mbeya waliofurika ndani ya ukumbi wa Dhando mwishoni mwa wiki
Ilifika zamu ya Mr Policeman a.k.a Ferooz (shoto) akiimba pamoja na mtu mzima Pro Jay wimbo wao wa Starehe ambao ulikubalika kwa kiasi kikubwa ndani ya washabiki wa muziki wa bongofleva,kati ni Kiboya kutoka kundi la Wanaume Halisi alikiwapa tafu

Ilikuwa ni shangwe tu kwa wakazi wa Mbeya

Matonya akiwa amenaswa kwa ukaribu kabisa na kamera ya jiachie


Matonya akiimba kwa hisia wimbo wake wa Anita mbele ya wakazi wa Mbeya


Eehbwana.! Vichwa vyote kutoka Tanga hivi ambayo vinafanya vyema katika muziki wa kizazi kipya,Kasim pamoja na Matonya wakiimba kwa pamoja hali ambayo iliwavutia mno wakazi wa mbeya,hasa kwa mpangilio wa sauti zao zilizojaa hisia kali za kumbembeleza


Kasim akiimba kwa makini moja ya wimbo wake wa AWENA mbele ya washabiki wake mjini Mbeya

Wakazi wa Mbeya wakishangweka ile mbaya



Moja ya wasanii wakali katika miondoko ya kuimba taraatiibu huku akibembeleza ile mbaya,anaitwa Kasim mtoto wa Kitanga huyu akiwaimbia wakazi wa mjini Mbeya mwishoni mwa wiki


Mwishoni mwa wikend Ziara ya uzinduzi wa Shangwe albam inayodhaminiwa na kampuni ya sigara ya TCC kupitia kitengo chao Str8 Muzik,ilikuwa mjini Mbeya ndani ya ukumbi wa Dhando na kuhudhuriwa na wakazi kibao wa mjini humo.Pichani ni msanii wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la kisanii PNC akifanya mambo jukwaani
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 30, 2009 | | Permalink | Maoni 3

Mdau anaomba email ya ali kiba

Mambo vipi huko?
Muna weza kunitumiya e-mail ya ali kiba msanii wa Tanzania? ya kwangu ni:ndianne@live.ca.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

naomba maelekezo ya kwenda spider net cafe wadau

Hi
Nahitaji kwenda au kufika kwenye ile net cafe inayoitwa spider net cafe naomba nielekeze vizuri ilipo kwani net nyingi mtaani mbovu.
lyimo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 30, 2009 | | Permalink | Maoni 2

MUUNGANO'S CELEBRATIONS

Hello Mr. Michuzi jr,
Heshima yako mkuu. Hongera sana kwa libeneke lako la kuonya, kuelimisha, kukosoa, na kuburidisha jamii., tafadhali pokea shukrani za dhati kutoka Montreal. Kwa niaba ya ya Chama cha Watanzania hapa Montreal (MTA), naomba unitundikie tangazo letu la sherehe za Muungano zitakazofanyika April 25, 2009 hapa Montreal Quebec.


Tunawakaribisha Watanzania wote waishio North America, hosusan Ottawa, Toronto, Calgary, Vancouver, New York, Boston, NJ, na kwengineko.

Ahsante sana msaada wako.


M.Massoud.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, March 30, 2009 | | Permalink | Maoni 4

bagamoyo shule ya msingi

Saturday, March 28, 2009
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bagamoyo wakicheza michezo yao kama ambavyo kamera ya Jiachie ilivyowanasa
Kibao cha shule ya msingi Bagamoyo kinavyoonekana leo mchana,hii ndiyo shule ambayo nilisoma miaka hiyoo,nimepita pale kusema kweli majengo yake yamechoka sana na yanatia huruma,miaka ya nyuma ilikuwa ni moja ya shule ambayo ilikuwa inafaulisha wanafunzi kwa asilimia kuwa tu sijui kwa miaka ya sasa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, March 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

jicho la Jiachie ndani ya tukuyu

Kamera ya Jiachie ilifika pia chuo cha ualimu tukuyu kilichopo Bulyaga..Tukuyu mjini
Pichani ni wafanyabiashra wakiendelea na biashara zao za kila siku katika soko la Madaraka lililopo Tukuyu mjini

Pichani kama uonavyo hilo jengo lilikuwa ni moja ya duka kubwa la jumla na maarufu sana mjini tukuyu,lilikuwa linamilikiwa na mhindi mmoja aliyejulikana sana kwa jina la Kaka,na ndiye aliyekuwa anaimiliki timu ya Tukuyu Stars a.k.a Banyambala.Kwa habari nilizozipata ni kwamba mhindi huyo alifariki kitambo na kupelekea duka hilo kufa kabisa na hata timu hiyo na yenyewe kushuka kabisa


Pichani ilikuwa ni moja ya mahali marufu sana miaka ya nyuma kwa mangoma mjini tukuyu,palikuwa panaitwa Kimpo complex discotheque,ebwana palikua balaa hapa,lakini kwa sasa kama uonavyo hakuna lolote linaloendelea,pamekufa



Pichani ni barabara inayoelekea Tukuyu mjini,wenyewe wanaita njia pandaNdembela mahali ambapo nimekulia mimi.

Kamera ya Jiachie pia ilipata wasaa wa kujivinjari mjini Tukuyu,ambapo ilinasa maeneo kadhaa ya mjini humo ikiwemo shule ya msingi Mzee wa Jiachie aliyosoma miaka hiyo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, March 28, 2009 | | Permalink | Maoni 4

mitaa ya kati mjini mbeya

Jamaa akikatiza na plastiki za mafutu kwenye soko jipya la Mwanjelwa mjini Mbeya leo mchana
Ndani ya mji wa Mbeya leo mchana kamera ya Jiachie ilipokuwa ikijivinjari hapa na pale,
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, March 28, 2009 | | Permalink | Maoni 1

mambo ya ulanzi mjini iringa

Friday, March 27, 2009
Hapa tayari tuko ndani ya jiji la Mbeya,ilikuwa jioni flani hivi
kabucha makini ndani ya Iringa,bucha hii niliinasa karibu na mahali anapotoka huyo mshikaji pichani chini

Mdau aliamua kwenda kununua chupa kadhaa kama uonavyo pichani,chupa moja aliuziwa kwa shilingi elfu moja


Amekwenda kuchimba dawa

Bado nipo ndani ya Iringa,ukipita lazima ukutane na hawa jamaa ambao wanabeba pombe ya Ulanzi kwa wingi, Kaka Mjengwa nadhani atakuwa ankifahamu vyema kinywaji hiki,hapo hata ukitaka fasta fasta kabla ya kupelekwa kilabuni unauziwa bila wasi wasi
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, March 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu