Saturday, February 28, 2009
INTRODUCING FLAVA NITE !!!!

MEET REAL FRIENDS AND DANCE VARIATIONS OF HITS WITH DJ BONILUV,DJ VENTURE AND DJ MACKAY, 2NITE SATURDAY AT BULL DOGS MASAKI HAILE SELLASIE ROAD ,500 FROM IST

KARIBUNI WOTE
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, February 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

timu ya netball ya clouds fm ikijifua kwa ajili ya nssf



Timu ya netball ya Clouds Fm 88.4 ikijifua vilivyo kwenye viwanja vya Lidaz Club kwa ajili ya mashindano ya kombe la NSSF yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Dar
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, February 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

kila kitu kinawezekana !

Hizi ni ngazi zilizopo nyuma ya steji kwa ajili ya kupandia jukwaani.
Kama nilivyowahi kuwaeleza hapo mwanzo kuhusu suala la ujio wa mapinduzi mapya ya muziki hapa Tanzania. Nikabandika na baadhi ya picha zilizokuwa zikionyesha ujenzi wa jukwaa zima ulivyokuwa ukiendelea,jukwaa ambalo naamin hakuna Tanzania nzima kama kuna anaejua lililipo kama hilo basi sio vibaya akatuweka wazi tujue sasa anga ya burudani inazidi kupata wakunaji, lakini mimi binafsi naamini hivyo HAKUNA.
Kwa hivyo jukwaa zima limeishakamilika,Steji ni kama uionavyo pichani ni ya vioo, hizo nyingine ni trasti kwa ajili ya kuning'iniza full system pamoja na full lights,Yaani ni bonge la jukwaa kusema kweli,kiasi kwamba msanii akipanda jukwaani atajisikia kweli yupo juu ya bonge la steji na anahitajika kufanya jambo la maana kuiburudisha hadhira na sio kubabaisha tu.
Kwa hiyo Wadau habari ndio hiyo na jukwaa hilo limefungwa toka siku kadhaa katika viwanja vya burudani ya lidaz pale Kinondoni Jijin Dar.Vimefungwa hapo kwa ajili ya kuhakikisha je kila kitu kiko sawa na kwamba likifungwa sehemu kama ile je muonekane wake utakuwa vipi na kama vipi kesho linaweza litakatestiwa na wana wa Twanga na kupepeta kwenye bonanza lao linalofanyika kila siku ya jumapili Lidaz club.Njooo ushuhudie mabadiliko katika anga ya muziki hapa Tanzania kama vipi sio vibaya ukimtonya na mwenzio kwamba sasa hivi mambo ni mswano bongo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, February 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

wikend njema wadau

Friday, February 27, 2009
Nawatakiwa wikend njema wadau wooote, kama vipi sio mbaya tukionana pale La Prima Victoria-Mwenge hiyo kesho jioni,tukapate kukumbushwa yale ya kale yaliyokuwa matamu na hata ya sasa kutoka kwa wakongwe wa muziki hapa nchini kama King Kikii na skwadi la zima la Chungulia huku ukiwa na kitambaa cheupe hewani kwa ishara upendo.Uchakavu umepangwa kuwa buku tano tu kwa kila kichwa,njoo wewe na yule tukaserebuka mpaka lyamba au vipi.!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

kp


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

2009 Karibu Fair








Dear Participant,

We invite you to participate in the tenth anniversary of Karibu Travel and Tourism Fair to be held in Arusha - Tanzania from 5th to 7th JUNE, 2009 at the Magereza Grounds next to Arusha Airport.

Book and pay for your booth, Best locations are offered on a "first come, first served" basis.

BOOKING
Bookings are now open, Prices are reasonable, we have stands from $270 and upwards.
Booking is made easy. You can book a stand online by clicking
http://www.karibufair.com/flash/bkstand.swf; Simple instructions will guide you through the booking procedure.

DELEGATES
You can register yourself as a Delegate (International Visitor) on
http://www.karibufair.com/flash/bkstand.swfvisit/deleg.php so as to have an opportunity of meeting several services at the fair.

For further information please visit our website
http://www.karibufair.com/

Looking forward to see you in Arusha on JUNE.


Thanks and Best Regards,
Bonny


Bonaventure Bernard
Karibu Trade Fair Ltd
P.O. Box 6162
Dodoma Road, Ngaramtoni ya Chini,
ARUSHA, TANZANIA

Tel: +255 788 749550
Cell: +255 784 686 528
Fax: +255 27 2506430
E-mail:
http://mail.google.com/mail/h/1r9n9jcovc0su/?v=b&cs=wh&to=info@karibufair.com
Web:
http://www.karibufair.com/
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

WAANDISHI WA HABARI - JOURNALISM FELLOWSHIP 2009

APPLICATIONS INVITED FOR UNITED NATIONS JOURNALISM FELLOWSHIPS

The Dag Hammarskjöld Scholarship Fund for Journalists is now accepting applications from professional journalists from developing countries for its 2009 Fellowship Program. The application deadline is Friday, March 20, 2009.

The Fellowships are available to radio, television, print and web journalists, age 25 to 35, from developing countries who are interested in coming to New York to report on international affairs during the 64th session of the United Nations General Assembly. The Fellowships will begin in mid-September and extend to late November and will include the cost of travel and accommodations in New York, as well as a per diem allowance.

The Fellowship Program is open to journalists who are native to one of the developing countries in Africa, Asia, South America and the Caribbean, and are currently working full-time for a bona fide media organization in a developing nation. Applicants must demonstrate an interest in and commitment to international affairs and to conveying a better understanding of the United Nations to their readers and audiences. They must also have approval from their media organizations to spend up to two months in New York to report from the United Nations. Click here for full eligibility and documentation requirements and Fellowship application form.

The journalists who are awarded Fellowships are given the incomparable opportunity to observe international diplomatic deliberations at the United Nations, to make professional contacts that will serve them for many years to come, to interact with seasoned journalists from around the world, and to gain a broader perspective and understanding of matters of global concern. Many past Fellows have risen to prominence in their professional and countries.

This is the 48th year the Dag Hammarskjöld Scholarship Fund has sponsored the Fellowship Program for Journalists. The program is administered on a volunteer basis by journalists at the United Nations, who raise money from foundations, corporations and diplomatic missions.

Questions about the program, eligibility and application process can be directed to info@unjournalismfellowship.org

SOURCE http://unjournalismfellowship.org/node/468
FOR MORE SCHOLARSHIPS, VISIT www.makulilo.blogspot.com
MAKULILO Jr,
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 27, 2009 | | Permalink | Maoni 1

Bi. Yoo Ban Soon Taek ndani ya viwanja vya wama

Misoji akiimba kwa hisia wimbo uliohusu elimu ya ukimwiWasanii waliowahi kutamba sana kwenye shindano la bongo star search mwaka jana, Rogers pamoja na mwanadada Misoji wakiimba mbela ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla fupi ya kumkaribisha mke wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa (UN) Bi. Yoo Ban Soon Taek

Wanaonyeshana picha za vivuli vyao zilizochorwa na vijana wawili fasta fasta viwanjani hapo


Mama Salma Kikwete akimfafanulia jambo Bi. Yoo Ban Soon Taek


Mama Salma Kikwete akipeana mikono na Mgeni rasmi Mke wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Yoo Ban Soon Taek mara baada ya kusoma hotuba.
Aidha katikaa hotuba hiyo mama Salma alisema kuwa "dira yetu ni kuhakikisha tunajenga jamii isiyo na maambukizi ya virusi vya ukimwi.Lengo kuu la mradi mingi tuliyoiona ni kuhakikisha hakuna tena maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yanayotokea kwa vijana.Lakini kuyafanikisha haya kunahitaji nguvu ya pamoja.Tunashukuru kwamba kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi miongoni mwa vijana kimeanza kupungua",
Amesema kuwa kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2007/2008 kiwango cha maambukizi Tanzania kimepungua kutoka asilimia 7 (iliokuwa mwaka 2003/2004) hadi kufikia asilimia 5.8
Bw. Benedicto Luvanda ambaye ni meneja wa TAYOA akitoa ufafanuzi wa picha mbele ya Mgeni rasmi Mke wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Yoo Ban Soon Taek ambaye aliambatana na mwenyeji wake fest lady Mama Salma Kikwete katika Tamasha la Vijana na Ukimwi lililofanyika katika viwanja vya WAMA jijini Dar es Salaam.


Muwakilishi kutoka Femina Hip, Gloria Mkoloma akifafanua namna majarida ya Femina yanavyoisaidia kuielimisha jamii katika masuala mbalimbali yanayohusu elimu ya Ukimwi mbele ya mgeni rasmi Mke wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bi. Yoo Ban Soon Taek pamoja na fest lady Mama Salma Kikwete pamoja na wageni waalikwa walipokuwa wakitembelea baadhi ya mabanda yaliokuwemo ndani ya viwanja hivyo.


Mke wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Yoo Ban Soon Taek pamoja na fest lady Mama Salma Kikwete wakiwasili viwanja vya mfuko wa Wanawake na maendeleo WAMA jana jioni jijini Dar kwa ajili ya hafla fupi aliondaliwa na wenyeji wake.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 27, 2009 | | Permalink | Maoni 1

ujio wa ban ki-moon bongo

Bw.Ban Ki-Moon akizungumza na umati mkubwa (chini pichani) ndani movenpick hotel jana jioni
Baada ya kuwasili katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon aliwahutubia wanadiplomasia,mawaziri,wanataaluma,jumuiya ya wafanyabiashara na wananchi waliojumuika kwenye hoteli ya movenpik jijini Dar jana jioni

"karibu mgeni wetu" kati akielekeza jambo mara aliposhuka hotelini hapo


Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Bw.Ban Ki-moon akiwasili kwenye hotel ya Kempisk jana mchana jijini Dar kwa ziara ya siku mbili
Baadhi ya akina mama wakiwa wamekusanyika jana mchana kwenye hotel ya Kempisk zamani Kilimanjaro wakisubiri kumpokea katibu mkuu wa umoja wa mataifa Mhe.Ban Ki-moon na mkewe Yoo Ban Soon Taek.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

House Of Glamour Spread

40ft x 100ft Marquee - With Green_Gold_Cream Deco
40ft x 100ft Marquee - Gold and Cream deco



Wakodishaji wa Mahema, Viti, meza, bouncy castles, red carpet n.k; tupo Dar es Salaam, Tanzania.


Mahema yetu ndio yanaongoza kwa uzuri na ubora; kama yalivyoonekana kwenye shows za Mbiliabeli, Fat Joe, Joe Thomas, Bongo Fiesta; na list inaendelea.


Kwa bei poa na huduma nzuri, Wasiliana nasi kupitia

Simu Namba:

+ 255 788 90 5001

+ 255 715 90 5002

Au ingia kwenye tovuti yetu http://www.houseofglamourtz.com/.


House of Glamour Hire means Business and Always Deliver!!

Or your money back!!!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

kuhusu rah p habari ndiyo hiyo.!

Thursday, February 26, 2009

Wadau kama mtakuwa mnakumbuka vyema niliweka post kuhusu huyu mwanadada Rah P kwamba yuko wapi na anafanya nini?
Habari za uhakika nilizotumiwa hivi punde kutoka kwa mdau G. Sengo ambaye ni moja ya watangazaji mahiri jijini Mwanza kupitia redio ya Clouds Fm,ameitonya JIACHIE kuwa Rah P kwa sasa anaishi nchini Marekani ambako anasoma katika chuo cha Huston Community College akichukua masomo ya International Bussiness akiwa mwaka wa 3,kama vile haitoshi mwanadada huyo tayari amekwishaolewa na mtasha mmoja wa huko huko ughaibuni.kuhusu suala la muziki mwanadada huyo mzaliwa wa Shinyanga lakini wazazi wake wote wanaishi jijini Mwanza,inaelezwa kuwa kauweka kando kwanza,aidha inanyetishwa kuwa maandalizi ya reception party ya harusi yake ambayo yalifana sana yalifanyika jijini Mwanza na Braza G Sengo ndiye aliyekula shavu la msema chochote (MC) na pia kuwa mkuu wa kamati ya burudani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 26, 2009 | | Permalink | Maoni 8

prof Lipumba na Maalim Seif walivyoibuka kidedea mkutano mkuu wa cuf

Mgombea Ukatibu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif,(Zanzibar) akipiga kura yake wakati wa Uchaguzi wa chama hicho katika ukubumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.

Wagombea Ukatibu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif,(Zanzibar) na Maalagande(Dar es Salaam) wakiteta jambo wakati wa Uchaguzi katika Mkutano mkuu wa Chama hicho, uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Katika mkutano huo mkuu Profesa Lipumba aliibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa chama cha wananchi CUF katika uchaguzi mkuu uliohitimisha mkutano mkuu wa 4 wa chama hicho katika ukumbi wa diamond jubilee uliofanyika jana jijini Dar
Profesa Lipumba alipata kura 600 kati ya kura 669 zilizopigwa na kuwashinda wagombea wengine wawili kwa asilimia 98.6. Wagombea wengine koplo stephen masanja alipata kura 10 (asilimia 1.5) na profesa abdalah safari aliyepata kura 6 (asilimia 0.9). Maalim Seif naye aliweza kutetea vyema kiti chake cha katibu mkuu baada ya kuzoa kura 657 (asilimia 99.5) ambapo nne zilisema hapana na mbili ziliharibika. Maalim Seif alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo kama alivyokuwa makamu wa mwenyekiti aliyepata kura 653 (asilimia 98.6) ambapo 5 ziliharibika na 4 zilisema hapana.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 26, 2009 | | Permalink | Maoni 1

kpzz


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 26, 2009 | | Permalink | Maoni 0

mradi wa umeme vijijini ukijadiliwa leo

Wednesday, February 25, 2009
Mkurugenzi wa Umeme wa EWURA Eng. Anastas Mbawala akiwafafanulia baadhi ya mambo waandishi wa habari waliohudhuria mkutano kati ya Ewura, Tanesco, wawekezaji na wadau mbalimbali uliojadili mradi wa umeme vijijini kuhusu bei, uwekezaji na jinsi ya kupata mikopo na kanuni zake unaofanyika leo kwenye Hoteli ya New Africa jijini, mkutano huo umeandaliwa na Ewura
Mkutano wa EWURA ulipokuwa ukiendelea asubuhi ya leo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, February 25, 2009 | | Permalink | Maoni 0

baada ya festive collections sasa aja na onesho la kakakuona

Kulia ni Meneja mahusiano wa CXC bw,Phil Mmari,Msanii wa kizazi kipya Angeris Faber,mamodoz watakaoshiriki kwenye onesho hilo pamoja na meneja wa kampuni ya Dollywood bw. K Malosha wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja leo
Mratibu wa onesho la KAKAKUONA,Asmah Makau akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na onesho hilo litakalofanyika machi 7 ndani ya ukumbi wa Dar Live zamani Malaika kule Mikocheni jijini Dar

Baadhi ya mavazi yatakayooneshwa na mamodoz (pichani) siku ya onesho

Pichani kulia ni muwakilishi kutoka kampuni ya Dollywood Bw.K Malosha (mdhamini),Meneja Mahusiano kutoka kampuni ya CXC Africa Ltd Bw.Phil Mmari (mdhamini) pamoja na msanii wa kizazi kipya atakaetoa burudani murua kabisa ndani ya onesho hilo aitwaye Angeris Faber

Mbunifu Fatma Amour akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo leo asubuhi kuhusu maandalizi ya onyesho lake la mavazi litakalojulikana kwa jina la KAKAKUONA ambalo litabeba ujumbe usemao "Unavyovaa ndivyo Ulivyo" litakalofanyika Machi 7 ndani ya ukumbi wa Dar Live zamani Malaika Mikocheni jijin Dar,ambapo pia siku hiyo itakuwa ni siku ya wanawake Duniani ambayo husherehekewa kila mwaka

Aidha katika onesho hilo kutakakuwepo na burudani mbalimbali akiwemo mwanadada chipukizi katika muziki wa kizazi kipya Angeris Faber kutoka Arusha, kikundi cha ngoma za asili cha Simba Arts, Exel Music Band pamoja na Lips Entertainment,.

Amour amewataja baadhi ya Wabunifu watakaoshiriki kwenye onesho hilo ambalo kiingilio chake kimepangwa kuwa 20,000/= kwa kichwa kuw ani Gabriel Saktamole mavazi ya kimasai, Ras Mizizi mavazi ya Kiafrika na Fatma Amour mwenyewe atakayeonyesha mavazi mbalimbali aliyoyabuni likiwemo vazi la waja wazito,harusi,kicheni pati,mavazi yenye bendera ya Taifa,begi za mikononi zitakazotengenezwa kwa ngozi pamoja na magunia.

Onyesho hilo limedhaminiwa na jarida la Exel, Dollywood, DTP, Vayle Spring JD Entertainment,Aqua Well Drill, Clouds Fm, Easy Finance,British Council Sofia Prodution na CXC Tours.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, February 25, 2009 | | Permalink | Maoni 0

mapinduzi mapya ndani ya anga ya muziki bongo

Hapa linawekwa sawa ili kuikamilisha nusu safari ya ujenzi wa jukwaa hilo litakalokuwa la aina yake Tanzania nzima.Wadau hapa kitu bado hakijakaaa sawa,kikikamilika leo jioni ile full jukwaa ntakuja hapa hapa tena kuonesha hali halisi itakavyokuwa ya jukwaa hilo la Kimataifa
Baadhi ya wadau wakishuhudia ujenzi wa jukwaa hiloo

Jukwaa likiinuliwa kwa winchi ili liweze kukaa sawa

Ujenzi wa jukwaa ukiwa unakamilika kamilika
Mapinduzi mapya katika anga ya muziki hapa bongo inazidi kuongezeka siku hadi siku,hii ni kutokana na baadhi ya wadau wakubwa wa muziki kugundua mapungufu kadhaa katika anga hii adhimu ya muziki hapa bongo.Hivi karibuni kampuni bingwa ya burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd/Clouds FM 88.4 imeshusha bonge la steji,hii ikiwa ni sehemu mojawapo yaliyoonwa na wadau hawa wakubwa katika anga ya muziki.Pichani ni steji ikianza kufungwa hatua kwa hatua ndani ya viwanja vya Lidaz Cluba,Kinondoni jijini Dar, ikiishakamilika ruksa kila moja wetu atakaebahatika kupata nafasi kwenda kujionea mabadiliko hayo ambayo kiukweli si ya kuyabeza hata kidogo,hawa wanahitaji pongezi kubwa kwa hatua ya mafanikio walioifikia
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, February 25, 2009 | | Permalink | Maoni 1

mdau prosper


Mdau prosper akiwa amepozi mbele ya michuma ya nguvu kwenye free show ya magari mbali Mbali hapo Yokohama,Jana juzi usiku
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, February 25, 2009 | | Permalink | Maoni 3

kpz


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, February 25, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Cheche Mitaani - Nini kinafichwa kuhusu vitambulisho?




Salaam,
Mradi wa Vitambulisho bado unavuta hisia za watu na bado umegubikwa na wingu kubwa la maswali. Tunaendelea katika sehemu ya pili kujaribu kutafuta majibu ya maswali hayo. Lakini pia kuna habari na maoni motomoto ambayo huwezi kuyapata kwenye chombo chochote cha habari kwa kiwango, kina, upana na uwazi unaopatikana kwenye kijarida chako ukipendacho tena cha bure kabisa cha "Cheche za Fikra".

Pata nakala yako kwenye http://www.mwanakijiji.com/ au omba ujiunge nasi na utakipata kwa njia ya barua pepe ukimuandikia mhariri@klhnews.com
Nasi sote na twende tukawe "Cheche"!
Mhariri
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, February 25, 2009 | | Permalink | Maoni 0

albamu ya shangwe ndani ya kasseti

Tuesday, February 24, 2009
Albamu ya Shangwe yenye CD mbili ambayo bado ipo madukani kwa sasa inakuja katika mfumo mpya wa Kasseti,hii ni kuhakikisha kila shabiki wa albamu hiyo hakosi kushangweka kwa namna moja ama nyingine.Kwa hiyo mdau kaa mkao wa kushangweka.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, February 24, 2009 | | Permalink | Maoni 0

wakali kwanza kuanzisha bendi.!


Niko na baadhi ya wasanii kutoka kundi la Wakali Kwanza linaoundwa na wasanii sita ambao wameonekana kuja vyema kwenye anga ya muziki huu kizazi kipya a.k.a bongofleva.Pichani shoto ni Mac Paul a.k.a Makamua,Mshakaji wa wakali kwanza,Binti anaechipukia kwenye fani ya utangazaji Clouds FM Saida pamoja na Joseph Kelvin a.k.a Qj tukiwa tumepozi mchana huu.

Wasanii hao wanaounda kundi la Wakali Kwanza wamenitonya leo kuwa wako mbioni kuanzisha bendi yao ambayo watakuwa wakipiga live kama bendi nyingine za muziki wa kizazi kipya,na kuwa kwa sasa wako mbioni kuikamilisha albam yao ambayo inafanyiwa kazi na Mj Records .Kwa habari zaidi kaeni mkao wa kula
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, February 24, 2009 | | Permalink | Maoni 0

mawakala wa ndege waikandamiza timu ya mashirika ya ndege

Pichani ni timu ya mawakala wa ndege tanzania wakiwa wamepozi
Pichani mbele ni naibu waziri wa mawasiliano,utamaduni na michezo wa Zainzibar,Mh Mahmoud Thabit Kombo akisaidiwa na timu ya mawakala wa ndege katika mchezo wa kuvuta kamba kwa upande wa wanaume.

Mwishoni mwa wiki timu ya mawakala wa ndege iliibuka kidedea baada ya kuikandamiza kwa magoli 3-0 timu ya mashirika ya ndege ya bongo,hiyo ilikuwa ni siku ya Michezo iliyoandaliwa na Galileo Tanzania,katika viwanja vya leader Club.Katika mashindano hayo kulikuwepo na mashindano ya michezo mbalimbali ikiwemo ya kukimbia kwa kutumia magunia,michezo ya kamba na mingineyo kibao
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, February 24, 2009 | | Permalink | Maoni 1

zain yaendelea kutoa zawadi za valentine kwa wateja wake

Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Costantine Magavilla (kushoto) akikabidhi simu aina ya Sony Ericsson kwa mteja wa Zain, Mariam Juma ambaye ni mwanafunzi wa Neema Trust High School aliyeibuka mmoja wa washindi 25 wa promosheni ya Valentine jijin Dar jana
Washindi watatu wa promosheni ya Valentine ya Zain, Issa Amani (kushoto), Mariam Juma na Amiri Songoro wakionyesha simu aina ya Sony Ericsson walizokabidhiwa jijini Dar jana
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, February 24, 2009 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu