JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SKAUTI WA KIKE TGGA WAFURAHIA KUVINJARI HIFADHI YA TARANGIRE

Share ThisAskari Uhifadhi Daraja la Kwanza ,Ally Omary wa Hifadhi ya Taifa Tarangire akielezea kuhusu utaratibu wa malipo na maelekezo muhimu wakati wa kutembelea Hifadhi hiyo wakati wa ziara ya viongozi wa Skauti wa Kike wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mwishoni mwa wiki.


Mwenyekiti wa TGGA, Prof. Martha Qorro akielezea lengo la ziara hiyo iliyofanyika baada ya kuhudhuria Kambi ya mafunzo elekezi kwa viongozi wapya wa chama hicho, Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Wakiwa ndani ya gari kuelekea mbuganiTembo akiwa na mtoto
Digidigi

NyumbuWatalii wa ndani yaani wazawa wakiangalia wanyama wakiwa ndani ya gariPundamilia

Twiga

Watalii wa ndani kutoka TGGA wakipiga picha wanyama waliowaona

Tembo

Mabango yenye maumbile ya wanyama yakiwa yameandikwa kuelekeza maeneo karibu na mapokezi ya Hifadhi ya Tarangire.

Baadhi ya watalii wa ndani wa TGGA kutoka Zanzibar.

 

 Ofisi za TarangirePICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDANa Richard Mwaikenda 

VIONGOZI wapya wa Chama Cha Skauti wa Kike cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wamefurahia kutembelea Hifadhi yaTaifa ya TARANGIRE ambapo walijionea ndege na wanyama wa aina mbalimbali. Ziara hiyo ya kutembelea Tarangire iliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro ambapo zaidi ya viongozi wapya 150 na sekretarieti walipata guess hiyo. 

Viongozi hao walipata wasaa huo wa kuvinjari katika hifadhi hiyo mwishoni mwa wiki wakitokea Kambi ya Mafunzo elekezi ya siku 6 katika Shule ya Sekondari ya Fundi Moshi, Mkoani Kilimanjaro. 

Walipofika walilakiwa kwa bashasha na watumishi wa Tarangire wakiongozwa na Askari Uhifadhi Daraja la Kwanza ,Ally Omary ambao walielezwa taratibu zote za malipo na masharti yanayopaswa kufuatwa wakati wa kutembelea Hifadhi hiyo.

 Baada ya hapo waliruhusiwa kupanda kwenye magari kwenda kutembelea Hifadhi huku kila gari likiwa na muongoza watalii mahsusi kutoa maelezo na maelezo kuhusu tabia za wanyama na ndege waliobahatika kuwaona. 

Wengi wa viongozi hao kutoka mikoa 20 ya Tanzania Bara na Visiwani walifurahishwa sana na ziara hiyo kwani baadhi yao ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kutembelea mbuga na kuwaona live ndege na wanyama. 

Walibahatika kuwaona Swala, Tembo, Twiga, Pundamilia, Nyumbu, Digidigi, Mbuni, Karani ndege, Hondohondo na wengineo. Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video Askari Uhifadhi Daraja la Kwanza ,Ally Omary Tarangire akielezea umuhimu wa wazawa Kujenga tabia kutembelea Hifadhi kwa gharama nafuu, lakini pia Profesa Martha Qorro wa TGGA akielezea lengo la ziara hiyo pamoja baadhi ya viongozi wakielezea jinsi ziara hiyo ilivyowafurahisha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad