NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHE.HASUNGA ATAKA USHIRIKISHWAJI KWENYE UHIFADHI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHE.HASUNGA ATAKA USHIRIKISHWAJI KWENYE UHIFADHI

Share This
NA LUSUNGU HELELA - MANYARA 

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewaagiza Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zake kuwashirikisha viongozi wa mikoa na wa wilaya wakati wanapokwenda katika maeneo yao kwa ajili ya kushughulikia migogoro ardhi kati ya Hifadhi na wananchi. 

"Nasema ni marufuku kwa Watumishi wa Wizara yangu kwenda kwenye maeneo ya Hifadhi bila kushirikisha uongozi wa eneo husika kwa jambo lolote litalohusisha wananchi  na Hifadhi" amesema Mhe.Hasunga. 

Aliyasema hayo jana kwenye mkutano mkoani Manyara kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.William Lukuvi kwa ajili ya kuzindua utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na Hifadhi utakaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi. 

Mpango huo una lengo la kutatua migogoro ya ardhi kati ya wananchi na Hifadhi utakaoshirikisha mikoa mitano ya Manyara,Dodoma,Mara,Arusha na Simiyu kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi. 

Naibu Waziri, Mhe. Hasunga alitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo kwa awamu ya kwanza kuwa ni Manyara, Arusha na Mara yenye jumla ya vijiji 95 kati ya vijiji 392 vilivyolengwa nchi nzima. 

Alisema kwa sasa Wizara imepiga hatua kubwa baada ya kupokea ushauri wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanza kuutekeleza kwa kuwashirikisha wananchi pamoja na Wizara ya Ardhi yenye dhamana kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi kati ya vijiji na Hifadhi. 

'Tumekuja kutambua kuwa sisi ni wahitaji wa ardhi na wananchi pia ni wahitaji wa ardhi hivyo hatuwezi kuamua wenyewe kwa kutambua hilo tumeanza kufanya kazi kwa ukaribu na Mkurugenzi wa upimaji na ramani kutoka Wizara yako lengo likiwa kumaliza migogoro kati ya Hifadhi na wananchi. 

Aliongeza kuwa Wizara inajikita kusaidia kufanya mipango shirikishi ya matumizi Bora ya Ardhi kati ya vijiji vinavyopakana na hifadhi kwa vile itasaidia kupunguza au kuondoa kabisa migogoro katika maeneo yanayopakana na hifadhi. 

Alisema mpango huo ni muhimu kwa vile idadi ya mifugo pamoja na binadamu wanazidi kuongezeka wakati maeneo hayaongezeki. Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema hatua ya kupanga matumizi bora ya ardhi ni hatua muhimu sana katika kumaliza migogoro kati ya Vijiji na Hifadhi. 

Aliongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya vizuri kuishirikisha Wizara yake kwa vile kipindi cha nyuma ilikuwa na migogoro ya ardhi kati ya vijiji na hifadhi isiyoisha ila kwa sasa itatuliwa kwa kubaini mipaka halisi. 

Katika hatua nyingine alisema hatua hiyo ni muhimu na hivyo viongozi wa mikoa itakayopitiwa na mpango huo watoe ushirikiano wa kutosha .Aidha, Aliwataka maafisa ardhi watakaoufanya kazi hiyo wafanye kazi kwa uaminifu na weledi wa hali ya juu na kwa haraka ili kuleta ufanisi wa Wizara yake. 

Naye, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Martin Leibook alisema sababu ya kufanya uzinduzi huo ni kutokana na ongezeko kubwa la migogoro siku hadi siku ambao unapelekea kutokuwepo na ushirikiano mkubwa kati ya wananchi na Hifadhi.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wajumbe kwenye mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara -liowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na wajumbe wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo.

 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (katikati) mara baada ya kufanyika mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. Wa tatu kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania, Martin Leibook. 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanyika mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) akiagana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge Mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo . 
1. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia) wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexandar Mnyeti.

(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad