Tutamfunga Simba kutetea ubingwa wetu-Azam fc - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

Tutamfunga Simba kutetea ubingwa wetu-Azam fc

Share This
Na Agness Francis,globu ya jamii

Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba katika fainali za kuwania kombe la kagame cup (CECAFA).

Timu hizo zote mbili za kutoka hapa nchini ambazo zimefanikiwa kutinga fainali, zitashuka dimbani kesho majira ya saa 12 jioni kuchoshana nguvu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya jana Azam FC kumuondosha Gor Mahia ya Nchini Kenya katika michuano hiyo kwa kipigo cha mabao 2-0, sasa wanakutana na wekundu wa msimbazi katika kumjua nani ataibuka kidedea wa kombe hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam msemaji wa Azam FC Jaffary maganga amesema kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanatetea ubingwa wao wa mwaka 2015 ambapo michuano hiyo ilifanyika kwa mara ya mwisho hapa nchini,Jaffary amesema maandalizi waliyofanya ni mazuri na ndio maana wamefanya vema na mpaka kufikia hatua hiyo.

"Tunaiheshimu Simba ni timu kongwe ya muda mrefu ilio na kikosi mahiri lakini sisi azam tunaliamini benchi letu la ufundi pamoja na mwalimu,tunaahidi kufanya vizuri kwa kumfunga simba"amesema jaffary.

Mtanange huo utakaokuwa wa ina yake wa kiburudani kwa mashabiki ,inaonyesha zahiri kuwa soka la Tanzania limezidi kuimarika katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
Msemaji wa Azam FC Jaffary maganga

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad