UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA? - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?

Share This
Francis Daudi, Melukote Town!

Jana dunia ilisimama kupisha ndoa ya kifalme, Mwana Mfalme Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ mwenye miaka 33 alimuoa mwigizaji wa Marekani, Bi Meghan Markle mwenye miaka 36. Hii ndio kusema Meghan Markle ambaye alishaoana na Trevor Engelson kisha kutalikiwa mwaka 2013 anakuwa Duchess wa Sussex.

Wote wawili, yaani Prince Harry na Meghan Markle wanatoka katika familia za wazazi ambao wana historia ya kutalikiana! Lakini kikubwa zaidi ni kuwa haikutarajiwa Harry kuoa nje kabisa ya Ufalme wa Uingereza. Prince Harry kwa takribani miaka 7 iliyopita alikuwa akim‘DATE’ binti Chelsy Davy, mara kadhaa waligombana na kurudiana. Wakati Fulani mwaka 2011 ilitaarifiwa kuwa wameachana. Na sasa Prince Harry akaanza kuonekana Binti Cressida Bonas hadi mwaka 2014.

Kama utani vile, Prince Harry alimrudia Chelsy Davy ila wakati huu mwana mfalme alihakikisha taarifa hizi hazisambai tena mpaka lengo la ndoa litakapotimia. Maisha ya kujificha, huku wakisubiri kutangaza uchumba mwezi June, 2016 walivurugana tena.

Mwaka 2017 tetesi zikasambaa kuwa sasa mtoto wa Mfalme Prince Harry amekuwa na safari nyingi Marekani na huko kuna ‘Shemeji’ ambaye jina halikujulikana mpaka Harry alipoutobolea umma kuwa ana mchumba ambaye ni mwigizaji Meghan Markle. Ilikuwa habari mbaya na ya kushtua hasa kwa kuwa Meghan Markle anajulikana sana na kwenye jumba la ufalme ilionekana sasa wameingiliwa na ‘Mtalikiwa’.

Pamoja na mazonge hayo yote, Prince Harry aliwaalika Ma-Ex wake hapo jana! Wote walikuwepo Kanisani St. George’s Chapel. Mara kadhaa waandishi walijaribu kuwazunguka Chelsy Davy na Cressida Bonas. Haikuwezekana kwani ulinzi ulikuwa ni Mkali sana.
Kihistoria, Prince Charles ambaye ni baba wa Prince Harry aliwaalika Ex’s wake wakati wa Ndoa yake na Princess Diana iliyofanyika Julai 29, 1981. Kati ya hao ni Camilla, ambaye alikuja kuwa mke wa Prince Charles baada ya kutalikiana na Princess Diana mwaka 1985. Hii ndio kusema, Prince Charles alipata kuwa na Camilla kabla ya kumuoa Princess Diana. Ndoa ilipovunjika Prince Charles akamuoa Camilla ambaye ni mkewe mpaka leo. 
Inaelezwa kuwa historia inaweza kujirudia kwa Prince Harry na Chelsy Davy ambapo wamekuwa pamoja kwa muda mrefu Zaidi.

Mjue sasa Meghan Markle na familia yake!

Meghan Markle amefunga ndoa hii ni ya pili, Ndoa yake ya kwanza na Trevor Engelson ilidumu kwa miaka miwili tu! Ndoa kati ya wazazi wa Meghan ilivunjika akiwa na miaka 6 tu. Baba yake Meghan, ambaye ni Thomas Markle alikutana na Bi Doria Ragland baada ya ndoa yake ya awali na Bi. Rosyln kuvunjika mwaka 1979. 
Mama yake Meghan, Doria Ragland ndiye hasa alimlea Meghan toka alipotalikiana na Bwana Thomas Markle mwaka 1985(Ndio mwaka huo huo wazazi wa Prince Harry waliachana pia yaani Prince Charles na Princess Diana).

Meghan Markle ambaye sasa ndio Duchess wa Sussex, ana ndugu ambao kila mmoja ana matukio yake! Hawa ndugu ni watoto wa baba yake tu kwani mama yake hakubarikiwa watoto wengine baada ya Ndoa kuvunjika.

Kaka yake, anayeitwa Thomas Markle Jr alimtishia kumuua mpenzi wake kwa bastola mwaka jana. Kaka huyu Mkubwa wa Meghan ana miaka 50 na bado hajaoa. Mwaka jana, 2017, Thomas Markle Jr alipata ‘umaarufu’ baada ya kumuandikia barua Prince Harry akimuonya kwamba mpango wake wa kumuoa Meghan Markle ni makosa makubwa ambayo yatakuwa ni historia katika ndoa za Kifalme. Alieleza kwamba ‘Ufalme wa Uingereza unaenda ‘kujidhalilisha’.
ALIPUUZWA na baada ya kuona hajafanikiwa aliomba radhi.

Dada yake Meghan anayeitwa Samantha Grant Markle inaelezwa ‘haziivi’ kabisa na Meghan. Inaelezwa kuwa alikuwa akimsema vibaya Meghan Markle baada ya kusikia tetesi za mahusiano ya mdogo wake huyo na Prince Harry.

Hapo Jana, Ni mama yake tu Bi Doria Ragland aliweza kuhudhuria harusi ya Binti yake na Mwana Mfalme Prince Harry. Bi Doria Ragland ni Mmarekani mweusi aliyepitia magumu ya ubaguzi wa rangi.

Uharaka wa Ndoa kati ya Meghan Markle na Prince Harry umeshitua wengi. Hasa kwa kuwa kwa miaka mingi Prince Harry alionekana na Chelsy Davy kama ambayo baba yake, Prince Charles alivyokuwa akionekana na Camilla Parker Bowles lakini akafunga ndoa na Princess Diana.

Kabla ya Ndoa ya Princess Diana na Prince Charles kuvunjika, Diana alilalamikia ukaribu kati ya Prince Charles na Ex wake Bi Camilla Parker Bowles. Hilo lilithibitika kwani haraka Prince Charles alimuoa Ex wake Bi Camilla Parker Bowles!

Prince Harry atarudia Makosa ya Baba yake?
Ufalme umeingiliwa?
Tusubiri.

Francis Daudi, Melukote Town!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad