WAZIRI MKUCHIKA ATAKA POLISI KUWA MSTARI WA MBELE KUKEMEA RUSHWA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WAZIRI MKUCHIKA ATAKA POLISI KUWA MSTARI WA MBELE KUKEMEA RUSHWA

Share This
Aipongeza Taasisi ya Uongozi kuwaandaa watumishi wa Serikali kuwa uongozi wazuri

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika amewataka Jeshi la Polisi kuwa mstari wa mbele katika kukomesha vitendo vya rushwa huku akisisitiza kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya utawala bora.

Mkuchika ametoa kauli hiyo jana jioni jijini Dar es Salaam kwa maofisa wa Jeshi la Polisi 32 kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao wamehitimu mafunzo ya Stashahada ya Uzalimi ya Uongozi kutoka Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute).

Mafahali hayo ni ya kwanza kutolewa na taasisi hiyo ambayo wameshirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland na hivyo kufanya mafunzo hayo kutambulika na kukubalika kimataifa kuhusu masuala ya uongozi.

Hivyo akizungumza na maofisa hao pamoja na wageni wengine waalikwa ,Mkuchika amewapongeza wahitimu hao lakini awakata kuwa mstari wa mbele wao pamoja na jeshi la polisi kwa ujumla wake kupambana na komesha rushwa.

Amesema katika mataifa mbalimbali maeneo ambayo rushwa inaangaliwa sana ni katika Mahakama na Polisi .Hivyo ni vema polisi nchini wakawa mstari wa mbele kukomesha rushwa.

"Mataifa mengi yanapimwa katika mambo ya kupambana na rushwa pamoja na kuangalia maeneo mengine pia wanaangalia na Jeshi la Polisi.Na kwa bahati mbaya kwenye nchi nyingi baadhi ya polisi wamekuwa wakituhimiwa kujihusisha na rushwa, hivyo ni vema waliopata mafunzo hayo ya uongozi wakawa mabalozi wa kukemea rushwa nchini,"amesema Mkuchika.

Amefafnua wizara anayaoingoza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), ipo chini yake na ndio maana amezungumzia suala la kupambana na rushwa na kueleza hata akipata mualiko kwenye sherehe za harusi bado atazungumzia umuhimu wa kukomeshwa rushwa nchini kwani ni adui wa haki.

Amewataka Polisi nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuheshimu misingi ya utawala wa bora na kusisitiza kuwa taaswira ya nchi wakati mwingine inapimwa kwa kulitazama jeshi hilo.Hivyo waliopata mafunzo hayo ya uongozi watakuwa washauri wazuri kwa maofisa wengine wa Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yao na mafunzo hayo yawe chache katika maeneo ya kazi.

Mkuchika amesema anatambua gharama ya mafunzo hayo, hivyo wahitimu wajue wanalo deni kubwa la kuwatumikia Watanzania na kuthibitisha kwa vitendo wameiva kwenye mafunzo ya uongozi ambayo yamewajenga katika kutoa maamuzi ya kimakakati.Kuhusu Taasisi ya Uongozi, Mkuchicha amesema anatambua kazi kubwai inayofanywa na taasisi hiyo chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu wake Profesa Joseph Semboja ya kupika na kuandaa watumishi wa umma katika masuala ya uongozi nchini.

"Kutokana na umuhimu wenu ndani ya nchi yetu, nilikuwa Dodoma na nilichofanya ni kuwaombea bajeti kwa ajili ya kuendesha shughuli zenu.Niwaambie bajeti ile imepitishwa.Serikali tunatambua mchango wenu katika kuandaa watumishi kuwa viongozi wazuri."Nikiri wapo ambao wamezaliwa na kipaji cha uongozi lakini ukweli uko palepale tafiti zinaonesha uongozi unasomewa na kujifunza kutoka kwa wengine kupitia vitabu, majarida na kukaa darasani,"amesema Mkuchika.

Amewapongeza wahitimu hao pamoja na wale ambao wamejiunga katika taasisi hiyo kwa ajili ya mafunzo hayo ambayo yanatarajia kuanza hivi karibuni na miongoni mwa waliomba mafunzo hayo yupo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Kwa upande Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja amesema mahafali hayo ni kwanza kwa Stashahada ya Uzalimi ya Uongozi ambayo taasisi hiyo wameianzisha.Stashahada ya Uzamili ya Uongozi ni programu ya mafunzo ya utawala yanaendeshwa na taasisi hiyo pamoja na Chuo Kikuu cha Kifini cha Aalto cha Mafunzo ya utawala.

Programu hiyo inalenga hasa kutoa mbinu na nyenzo za uongozi kwa viongozi wa Serikali wa ngazi za juu,nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla ili kufikia maendeleo endelevu.Stashahada hiyo ina moduli 10 na ni ya kipindi cha mwaka mmoja.Kundi la kwanza la washiriki wa Stashahada hiyo wamehitimu jana na walianza mafunzo Aprili mwaka 2017.

Ambapo Profesa Semboja amefafanua mafunzo hayo yanajenga uwezo wa kiongozi katika kusimamia masuala mbalimbali na hasa kufikiri kimkakati na kutenda na kuamua kwa njia iliyosahihi."Mafunzo ya Stashahada ya Uzamili inatoa nafasi ya kumuandaa mhitimu na kuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza na kuandaa viongozu wenye uwezo wa kufikiria vema.

" Pia mhitimu wa mafunzo haya anaweza kujiendelea kielimu katika Chuo cha Aalto ambacho ni moja chuo kikubwa nchini Finland,"amesema Profesa Semboja.Amesema changamoto kubwa ya Staahahada ya Uzamili ya uongozi ni gharana kubwa na kufafanua wahitimu wapatao 32 wamehitimu na anaamini watatoa mchango mkubwa katika maeneo yao ya kazi.

Profesa Semboja amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kwa uamuzi wake wa kuomba kujiunga na taasisi hiyo ili naye apate mafunzo hayo ya Uongozi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad