728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, March 22, 2018

  TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii  inayodai kutakuwa na tatizo katika mfumo wa manunuzi ya LUKU kuanzia Machi 25 hadi Aprili 5 mwaka huu.

  Taarifa hiyo ya kutunga inadai kutokana na hali hiyo wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho.

  Tanesco kupitia Ofisi ya Uhusiano imesema taarifa hizo si za kweli na uzushi wenye nia ya kupotosha umma kwani haijatokea taarifa yoyote kuhusu hitilafu katika mifumo ya manunuzi ya LUKU.

  "Ikumbukwe kwamba taarifa kutoka Tanesco hazitolewi na mtu binafsi bali ofisi ya uhusiano iliyo chini idara ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo ni msimamizi wa utoaji taarifa za shirika hili,"imesema taarifa ya Tanesco.

  Imewaomba wateja wote wa Tanesco waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote ."Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida."
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top