MAANDALIZI TAMASHA LA PASAKA YAZIDI KUNOGA,WAIMBAJI WAZIDI KUMIMINIKA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

MAANDALIZI TAMASHA LA PASAKA YAZIDI KUNOGA,WAIMBAJI WAZIDI KUMIMINIKA

Share This
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akizungumza mapema jana mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar kuhusiana na  maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018  litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Aprili 1 Jijini Mwanza na Aprili 2 Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.
 
Msama ameanza kuwatangaza baadhi ya waimbaji watakaoshiriki tamasha hilo ambalo limekuwa likiwavutia waimbaji wengi kila linapoanza kuandaliwa na hatimaye kukamilika,Msama amemtaja mwimbaji mahiri jukwaani Boniface Mwaiteje,Christina Shusho,Rose Muhando ambaye atazindua albamu yake mpya siku hiyo, na wengineo ambao wanaendelea kujiunga kuhakikisha tamasha hilo linafana. Pichani kulia ni mwimbaji Paul Clement pamoja na Beatrice Mwaipaja,ambao walitambulishwa rasmi hapo jana.
Beatrice Mwaipaja akifafanua zaidi namna ambayo ananendelea kujiandaa na maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka Kanda ya Ziwa kushoto ni Mwimbaji mwenzake Paul Clement.
 Mwimbaji Paul Clement akizungumza kuhusu maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka Kanda ya Ziwa, kulia ni Mwimbaji mwenzake Beatrice Mwaipaja .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad