UKAGUZI WA TFDA WAKUTANA NA DAWA ZA SERIKALI KATIKA MADUKA BINAFSI , DAWA BANDIA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

UKAGUZI WA TFDA WAKUTANA NA DAWA ZA SERIKALI KATIKA MADUKA BINAFSI , DAWA BANDIA

Share This
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo akionyesha kopo lenye dawa aina ya Ampicilin isiyosajiliwa na mamlaka ya TFDA leo jijini Dar es Salaam.

………………………………………………………………………………..
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) iliendesha ukaguzi maalum wa dawa , vifaa tiba na vitendanishi katika Halmashauri na Manispa zilizo Kanda ya Kati na kubaini kuwepo kwa vifaa tiba na vitendanishi bandia duni ambavyo hajasajiliwa pamoja na dawa za serikali katika maduka ya dawa binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo , Agnes Kijo amesema kuwa mamlaka haitawaacha watu wafanye vitu kiholela pamoja na kuwafikisha watu hao mahakamani.

Amesema ukaguzi huo umefanyika kati ta Februari 5 hadi 7 mwaka huu katika Manispaa ya Dodoma , Morogoro na Mkoa wa Singida umefanyika katika wilaya ya Manyoni ,Iramba , Wilaya ya Gairo ,Mvomero , Kongwa na Chamwino.

Kijo amesema jumla ya maeneo yaliyofanyiwa ukaguzi 172ambapo 48 ni Famasi za dawa za binadamu , tano ni Famasi za dawa za mifugo ,tatu ni Hospitali na tatu zingine vituo vya afya , 76 ni maduka ya dawa muhimu za binadamu , 30 ni maduka ya dawa muhimu za mifugo, 1 ni zahanati pamoja na sita vituo vya huduma za tiba za mifugo .

Amesema kuwa katika ukaguzi wamepata makopo 12 ya dawa bandia aina ya Ampicillin 250mg ambapo ni tofauti na dawa halisi ya Ampicillin iliyosajiliwa na TFDA.

Amewataka ambao wenye bidhaa ambazo wanaziuza na kuweka katika mitandao wajisalimishe bila kufanya hivyo hatua kali za kisheria  zitachukuliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad