STENDI YA KISASA MAILMOJA - KIBAHA KUKAMILIKA MACHI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

STENDI YA KISASA MAILMOJA - KIBAHA KUKAMILIKA MACHI

Share This
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

STENDI ya mabasi ya Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani inatarajiwa kukamilika Machi baada ya mkandarasi wa kuongezewa muda kutokana na mradi huo kukumbwa na changamoto kadhaa.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Renatus Makoye msimamizi wa ujenzi wa stendi hiyo kutoka kampuni ya Mhandisi alipokuwa akielezea maendeleo ya ujenzi huo kwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Pwani Ramadhani Maneno ambaye alikwendakukagua mradi huo .Alisema awali mradi huo ulitarajiwa kukamilika Novemba mwaka jana.

Makoye alisema kuwa stendi hiyo ambayo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.9 itakuwa ikihudumia wasafiri wa mabasi ya kwenda mikoani pamoja na mabasi madogo ya Daladala yanayofanya safari zake ndani ya mkoa imefikia hatua za mwisho.

"Awamu ya kwanza ilikuwa ni ujenzi wa fensi, choo na kituo cha polisi, awamu nyingine ni ujenzi wa sehemu ya mabasi kupaki na sehemu za magari binafsi," alisema Makoye.Alieleza ujenzi huo umezingatia viwango ambapo sehemu ya mabasi makubwa ujenzi wake ni kiwango cha zege huku ile ya mabasi madogo imejengwa kiwango cha lami.

Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Ramadhan Maneno aliishukuru serikali kwa kuwa na taasisi na benki ya dunia ambao ndiyo waliofadhili wa ujenzi huo.Alielezea kwamba thamani ya fedha zimetumika kwa usahihi.

Maneno alisema ujenzi wa mradi wa stendi utainua uchumi wa mkoa wa Pwani na kuwataka watumiaji wa stendi hiyo kuitunza ili iweze kudumu na kutoa huduma nzuri.Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Jeniffer Omolo alisema baadhi ya majengo yatajengwa ikiwa ni pamoja utawala litajengwa na vibanda vya kukatia tiketi sehemu za abiria kusubiria mabasi, migahawa na majengo ya huduma mbalimbali za kijamii.

Omolo alisema baadhi ya majengo hayajajengwa kutokana na fedha kutokuwa ya kutosha kuweka vitu vyote hivyo .Alisema lengo lao ni kuwa na stendi ya kisasa ambayo ina huduma zote.
 Hali halisi ya ujenzi unavyoendelea katika stendi Mpya ya kisasa inayojengwa mjini Kibaha Mkoani Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno (wa tatu kutoka kulia) akimsikiliza mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jennifer Omolo (wa pili kutoka kulia)wakati alipokuwa akitoa taarifa ya miradi ya soko la Loliondo na ujenzi wa stendi Mpya ya kisasa katika ziara ya siku moja aliyoifanya mwenyekiti huyo mjini humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad