SOLOMONI MUKUBWA,CHRISTINA SHUSHO WATHIBITISHA KUNOGESHA TAMASHA LA PASAKA 2018 KANDA YA ZIWA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

SOLOMONI MUKUBWA,CHRISTINA SHUSHO WATHIBITISHA KUNOGESHA TAMASHA LA PASAKA 2018 KANDA YA ZIWA

Share This

Waimbaji wa nyimbo za Kiroho (Injili), Afrika Mashariki na Kati Christina Shusho na Solomon Mukubwa wanatarajiwa kuwaburudisha kiroho vilivyo,watakapokuwa wakitumbuiza katika jukwaa la Tamasha la Pasaka 2018,ambalo safari hii linafanyika Kanda ya Ziwa,mkoa wa Mwanza na Simiyu. 

Akiwatangazia Mashabiki wa Tamasha la Pasaka jijini Dar Es Salaam hapo jana,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw, Alex Msama alisema kuwa mbali ya uzinduzi wa Mwimbaji Nyota wa nyimbo za Injili,Rose Muhando pia waimbaji hao wamethibitisha kuzindua na kuzitangaza nyimbo zao mpya.

Msama amesema kuwa Waimbaji hao wana  nyimbo nzuri na zenye kumuimbia,kumsifu na kumtukuza Mungu,nyimbo ambazo anaamini zitavuta hisia za wengi watakapozikia.

"Solomoni Mukubwa na Shusho wote hawa hawajasikika muda mrefu katika majukwaa,hivyo wakazi wa Kanda ya Ziwa wakae mkao wa kuzifurahisha roho na wajitokeze kwa wingi katika maonesho hayo yatakayofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Aprili 1 na Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu Aprili 2 mwaka huu",alisema Msama.
Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maandalizi ya tamasha la pasaka linalotarajiwa kurindima Kanda ya Ziwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad