JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KAMPUNI YA ALAF YATOA PUNGUZO LA BEI BIDHAA ZAKE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE ARUSHA

Share This
 Mteja kutoka Simanjiro alipata fursa ya kutembelea banda la ALAF katika maonyesho ya nane nane kanda ya kaskazini Arusha,  akaeleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya ALAF ambapo amewataka watanzania kupenda na kuthamini bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa kuwa zinaubora wa hali ya juu(Habari picha na Pamela Mollel Arusha)
 Afisa Masoko wa kampuni ya ALAF jijini Arusha Finias Wanguba akionyesha bati aina yaTekdek inayozalishwa na kampuni hiyo jijini Arusha,
Meneja mauzo kanda ya kaskazini Edward William akionyesha aina ya mabati yanayopatikana katika kampuni yao
 Wateja wakiwa katika banda la kampuni ya ALAFwakipewa maelezo juu ya ubora wa bidhaa hiyo


Kampuni ya ALAF inayozalisha na kusambaza mabati ya aina mbalimbali 


Na Pamela Mollel,Arusha


Kampuni ya ALAF inayozalisha na kusambaza mabati ya aina mbalimbali ya rangi  pamoja na bati maarufu simba dumu imekuwa ikihudumia watanzania kwa zaidi ya miaka 50.
 
Akizungumza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini Afisa Mauzo wa kamapuni ya ALAF Finias Wanguba alisema kuwa  mabati hayo yana ubora wa hali ya juu na bei zake ni za kawaida tu hivyo mwananchi  yeyote anaweza kumudu kununua

Pia katika maonyesho hayo ya nanenane kamapuni hiyo imetoa punguzo la bei katika bidhaa zake 

Mabati haya hupatikana kanda ya kaskazini Arusha,kanda ya kati Dodoma,kanda ya ziwa Mwanza,Nyanda za juu kusini Mbeya,Dar esaalam

Hata hivyo kiwanda cha ALAF ni kiwanda cha kwanza Tanzania kilicholeta teknologia ya bati la msauzi ambapo huzalisha bati na chuma

Kwa upande wake  Mteja kutoka Simanjiro alipata fursa ya kutembelea banda la ALAF katika maonyesho ya nane nane Mkoa Arusha,  alieleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya ALAF ambapo amewataka watanzania kupenda na kuthamini bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa kuwa zinaubora wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad