JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

SHAIRI: ENYI WATU WA TAKWIMU! (JIBU)

Share This
hELO! 
MAMBO VIPI, KUNA MTU ANAITWA MWAMGONGO alitunga shairi  katika Globu ya jamii (Issamichuzi) juzi juu ya Sensa kuweklwa Kipengele cha dini na Serikali kugoma. Nami nimetoa Jibu.

SHAIRI: ENYI WATU WA TAKWIMU! (JIBU) 

Salamu nyote wadau, wa habari za bloguni
Rubani na wapiga dau, hata mlio maskani,
Sensa haita wasahau, namlio gerezani,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Si kazi ya serikali, kutambua wenye dini,
Msaada wa serikali, hauendi kwa  wenyedini,
sHuwafikia wa suruali, na wavaao magauni,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Katika nyumba za ibada, humo wanajuana,
Wakwetu anaitwa Sada, wenzetu wanae Anna,
Daima hakuna shida, na bado tuna zaana,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Hakika limekupa shida, Mwagongo kutoka Tanga,
Tujione ni wakawaida, dini wasipo ipanga,
Wala tusiwape shida, wakianza kujipanga,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

 Serikali haina dini, hakuna asofahamu,
Haishabikii udini, bali amani idumu,
Tuishi kama zamani, wala tusishutumu,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Mbona tupo wapagani, tunaishi masikani,
Tumejaa majumbani , hatupajui makanisani,
Hata huko msikitini, napo pako shakani,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Umeongelea hesabu, za watu pia makazi,
Dini isiwe ni sababu, tukageuka wakambizi!
Watu wawe mabubu,kisa dini hakuwekwa wazi?
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Watu tunahamasisha, kuhesabiwa majumbani,
Dini zinawakumbusha, kutokimbilia mashambani,,
Lipi lina chekesha, tusipende ‘uhayawani’,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

 ‘Una iga za  dipatimenti’, ya watu wa Marekani,
Kuanda  tovuti, dini zote kuweka ndani,
Ushoga hamuutaki, sisi unataka Umarekani?
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Dini haina tofauti, kwa mzungu na msukuma,
Haina mvaa suti, wala Mchaga asie soma,
Ni haki kupiga shuti, katika Takwimu daima,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Mapadri makanisani, hata nanyi maasikofu,  
Hamasisheni waumini, wahesabiwe bila hofu,
Wabakie majumbani, watoto hata vipofu,
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Kalamu naweka chini, sore nilipokosea
Jalalu ibariki nchi, Amani sije potea,
Zoezi bado bichi, Sensa wasije kosea.
Kutambua  wenye dini, si kazi ya serikali.

Mroki Mroki ‘Father Kidevu’
www.mrokim.blogspot.com
Kinyenze, Morogoro
18  Juni 2012 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad