JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


tamasha la Tusker all stars 2011 laitikisa jiji la nairobi.

Share This
"Asanteni sana Wakazi wa Nairobi".!Wanamuziki wa Kimataifa,Cabo Snoop pamojana Eve E wakiwaaga maelfu ya mashabiki kwa heshima kubwa,hasa kwa kujitokeza kwa wingi na kuonesha ushirikiano mkubwa kwa wanamuziki hao ambao kiukweli walifanya vyema sana.
Pamoja na kuwepo kwa hali ya mvua mvua,lakini maelfu ya watu waliokuwa kwenye viwanja vya carnivo kujiachia ndani ya tamasha la Tusker All Stars 2011,hawakutaka kubanduka kabisa,badala yake walikuwa wakijifunika na viti ili wasikose uhondo uliokuwa ukiendelea kutolewa jukwaani.


Mmoja wa madada wakali katika miondoko ya hipo hop nchini Marekani,Eve E akiwaachia mistari wakazi wa Nairobi,ambao wengi wao walikuwa wakivutiwa nae kwa namna ambavyo alikuwa akionesha kukomaa kwake kwenye anga ya muziki wa hip hop.


Shaggy ni mmoja wa wanamuziki ambao kiukweli awapo jukwaani hana masikhara kabisa na uwanja wake,kila wakati hupenda kuhakikisha watu wanashangweka tu,na ndivyo ilivyokuwa kwenye shoo yake usiku wa leo,kila wakati alikuwa akiwaimbisha mashabiki nao bila hiyana walikwenda nae sambamba,hali iliyomfurahisha zaidi.
Bak voko wa Shaggy wakikamua jukwaani.
Shaggy na bak voko wake wakilishambulia jukwaa,huku maelfu ya mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo wakipaga mayowe kuonesha kuwa wanakunwa vilivyo na umahiri wa wanamuziki hao.
Back voko wa Shaggy akifanya kweli.
Shaggy akiwaimbisha maelfu ya watu waliofurika kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011,ndani ya viwanja vya Carnivo jijini Nairobi,usiku wa kuamkia leo.
Mkali wa Reggae kutoka nchini Jamaica,Shaggy akiimba kwa hisia jukwaani.
Ndani ya uwanja wa Carnivo jijin Nairobi,ilikuwa ni shangwee tuu.
Cabo Snoop akicheza wimbo wake wa Windek na pia alikamua wimbo wake mwingine wa Prakatatumba,daa eebwaanaeee jamaaa yuko na eneji ile mbaya.
Mwanamuziki Cabo Snoop na densa wake wakilshambulia jukwaa vilivyo,huku shangwe na mikono kupunga kwa hewa kwa mashabiki kama kawa tu.

Wanamuziki wa Kimataifa,Cabo Snoop kutoka nchini Angola pamoja na Eve E kutoka nchini Marekani wakijiachia vilivyo kwa pamoja jukwaani,huku mayowe na miluzi ikiwa imetawala kila kona ya uwanja
Utamu wa ngoma Live bwaana wee,palikuwa hapatoshi jukwaani,midomo ya bata kama kawa ilikuwepo kuongeza na kunogesha utamu wa live.
Msanii Davies kutoka Uganda ambaye ni mmoja wa vinara wa Tusker All Stars 2011 akionesha umahiri wa kucheza na kuimba jukwaani,mbele ya maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha hilo lililofana kwa kiasi kikubwa.


Mashabiki na wapenzi wa muziki wakiwa wamejitokeza kwa wingi ndani ya viwanja vya Carnivo,jijini Nairobi,kushuhudia wanamuziki wa Kimataifa wakifanya kweli ndani ya jiji hilo.
Mkali mwingine wa Tusker All Stars 2011,Davies kutoka nchini Uganda akilishambulia jukwaa vilivyo na madensa wake katika miondoko ya kindombolo ndombolo hivi.


Alpha akiimba kwa hisia kabisa mbele watazamaji wa tamasha la Tusker All Stars 2011.


Kwa mbaali kama uonavyo ndivyo ilivyokuwa kwa usiku,jukwaa likionekana kwa namna ile huku washabiki na wapenzi wa tamasha hilo wakiwa wamelizunguka kujionea yaliyokuwa yakijiri jukwaani hapo.
Mmoja wa wasanii nyota wa Tusker All Stars 2011 kutoka nchini Rwanda,aitwaye Alpha akiwakuna vilivyo wakazi wa jiji la Nairobi na wimbo wake wa Nasonga mbele.
Hivi ndivyo Wakazi wa jiji la Nairobi na kwingineko walivyotapika ndani ya uwanja wa carnivo,ambako ndiko tamasha la Tusker All Stars 2011 lilikofanyika,ama kwa hakika ni tamasha ambalo limefana sana ndani ya jiji hilo,pamoja na kuwepo na hali ya mvua mvua,lakini washabiki wa tamasha hilo ndio kwaanza walikuwa wakijiachia vilivyo uwanjani hapo huku wakipata vinywaji mbalimbali kutoka kampuni ya EABL-Kenya.Tamasha la Tusker All Stars 2011 limeratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions kwa kushirikiana na wadau wengine,huku wadhamini wakuu wa tamasha hilo ni Kampuni ya East African Breweries Ltd-Kenya kupitia kinywaji chake cha Tusker.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad