JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHUGHULI ZA KIBANADAMU HUCHANGIA KUCHAFUA BAHARI, WAFANYAKAZI UMOJA WA MATAIFA, YUNA WAFANYA USAFI 'COCO BEACH'

Share This

 












Baadhi ya wwafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Asasi mbali mbali za Kiraia za Vijana ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakifanya Usafi katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.


DUNIA ikiwa inaelekea kuadhimisha kilele cha siku ya Bahari, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umeamua kuiadhimisha siku hiyo kwa kusafisha Fukwe ya Coco jijini Dar es Salaam.

Leo tarehe 25 Juni 2022 umoja wa Mataifa sambamba na Asasi mbali mbali za Vijana ya Umoja wa huo nchi imeamua kuihami bahari kwa kuondosha Plastiki na taka zingine hatarishi kwenye maji ili kuokoa maisha ya viumbe hai baharini.

Akizungumza leo Juni 25, 2022 wakati zoezi hilo la usafi lililofanyika katika fukwe za Koko Beach jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa kitengo cha habari Umoja wa Mataifa ( UN) Stella Vuzo amesema kuwa kitendo hicho ni sehemu ya Mkutano Mkuu wa Bahari unaotarajiwa kuanza Juni 27 hadi Julai Mosi, 2022

Amesema, Mkutano huo wa muhimu utakaoongozwa na Kenya pamoja na Portugal utahudhiriwa na nchi wanachama 128 wa umoja huo qmbapo Mataifa yatakutana kujadili Hali ya bahari.

Amesema kuwa kwa sasa bahari imechafuliwa na Plastiki na shughuli za kiuchumi zinazofanywa na binaadamu.

Amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka huu itakita kwenye matumizi ya Bahari na Sayansi.

"Kuna mahusiano ya karibu ya Hali ya Hewa duniani na Bahari kwa kuwa asilimia 25 ya Hewa chafu inapunguzwa kwa kunyonywa na Bahari" asema Vuzo.

Naye, Nafisa Didi, Afisa habari kutoka kituo habari cha Umoja wa Mataifa jijjni Dar es Salaam, amesema, wameamua kushirikiana na vijana kutoka Taasisi mbali mbali kwa kuwa vijana ni Taifa la kesho, na ndio sehemu kubwa sana ya idadi ya watu hususani Tanzania.

Ametoa wito kwa wananchi hususani vijana kuhakikisha wanaitumia bahari na kuicha katika mazingira safi kwani eneo hilo ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na hata kujipatia ajira hivyo wakiitunza hata vizazi vijavyo vinaweza kuja kuikuta kama ilivyo ama ikiwa bora zaidi kwa matumizi.

Naye, Ally Mwanzola Mweka Hazina wa YUNA amesema, Bahari inaumuhimu mkubwa katika maisha yetu tunaitegemea kwenye uchumi, tumeona hata Uchumi wa Blue kule Zanzibar unategemea Bahari kwa hiyo ni lazima tuitunze.

Amesema kuwa Binaadam amekuwa chachu ya uchafuzi wa bahari na kusababisha mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kuwa wao kama wanaharakati wa mazingira wameamua kufanya usafi kwenye fukwe ya bahari. Kiwango cha uzalishaji duniani Bilioni 10 ni aslimia kumi tu inaweza kuwahifadhiwa kwa hiyo Kiwango kilichobaki kinakwenda kuchafua mazingira.

Amesema kuwa uamuzi wao wa kwenda kusafisha fukwe za bahari unatokana maoni yao ya kuondosha Plastiki ili kuokoa viumbe hai vinavyokufa kutokana na athari ya Plastiki.

"Tumeona kuna viumbe hai vingi vinakufa kutokana athari ya Plastiki kwa hiyo miaka inayokuja kuna viumbe baharini vinaweza vikatoweka na vizazi vyetu vitashindwa kuviona, hata matumbawe yataharibika na maisha ya watu wanaovua samaki yatakwama."

Kwa upande wake, Kelvin Edward amesema.."Tumeamua kuisafisha bahari kwa Vitendo ili kuhakisha vizazi vijavyo vinarithi tulivyorithi pamoja na kutoa elimu ya kutunza bahari" .

Amesema kuwa kuna uchufu aina nyingi unaoweza kuhatarisha maisha ya viumbe bahari ndio sababu ya YUNA kujumuika na wafanya baishara wa Kokobeach pamoja na wakaazi jirani wa Ufukwe huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad