JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KAMATI YA MIJI DADA YA DURHAM NA ARUSHA WAMKARIBISHA BALOZI ELZIE KANZA KWENYE MIAKA 60 YA UHURU

Share This

Picha ya pamoja
Picha juu na chini wageni waalikwa wakiwemo wadau wakibadilishana mawili matatu kabla ya maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara kuanza.

 

Picha juu na chini ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa Meya wa Durham anayemaliza muda wake akiwemo Rais wa SCD (miji dada ya Durham na Arusha) na wadau wengine kwenye maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Picha juu na chini ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akitoa neno la shukurani kwa kamati ya miji dada Durham na Arusha kwa kumkaribisha kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo katika kuendelezamashirikiano kati ya nchi za Tanzania na Marekani katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo uwekezaji. Picha na Vijimambo Blog
Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya miji dada Durham na Arusha (SCD) Bi. Ronda Pierce akieleza historia ya kamati ya miji dada na mashirikiano yao na mji wa Arusha na Durham tangu mashirikiano hayo yalipoanzishwa.
Maya wa mji wa Durham anaemaliza muda wake. Steve Schewel akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza na kuelezea mashirikiano ya mji wa Durham na Arusha na safari yake nchini Tanzania hususani kwenye mji wa Arusha.
Rais wa miji dada ya Durham na Arusha (SCD) Bwn.Tom Harris akitoa salamu kwa Mhe. Balozi kutoka kwa Kamati ya miji dada ya Durham na Arusha (SCD)
Kansela wa Chuo Kikuu cha NCCU ( North Carolina Central University) Bwn. Jonson Akinleye akimkaribisha Mhe. Balozi na kamati ya miji ya Durham na Arusha chuoni hapo siku ya Jumapili Disemba 5, 2021 siku SCD walipomkaribisha Balozi kwenye maadhimisho ya miaka 69 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya miji ya Durham na Arusha Bi.Gwendolyn Bookman akitambulisha Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza kwa kusoma wasifu wake na baadae kumkaribisha kuongea na hadhala iliyojumuika pamoja na kamati ya miji dada ya Durham na Arusha katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Meya mteule wa Durham Bi. Elaine Neel akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza
Meya wa zamani wa mji wa Durhan Mhe.William Bell akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza
Kansela wa Chuo Kikuu Cha NCCU ( North Carolina Central University Bwn. Johnson Akinleye akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza
Mwenyekiti wa Jumuiya ya waTanzania North Carolina Scolastica akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza
Kuyshoto ni Afisa Ubalozi Bi Jean Msabila na Mku wa Utawala na Fedha Bi. Eva Ng'itu wakifuatilia jambo kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyokua yameandaliwa na Kamati ya miji dada ya Durhan na Arusha katika Chuo Kikuu cha NCCU (North Carolina Central University) siku ya Jumapili Disemba 5, 2021.
Picha juu na chini wageni waalikwa wakiwemo wadau mbalimbali wakifuatilia maadhimisho hayo.
Picha juu na chini wadau mbalimbali wakiuliza maswali wakiwemo wawekezaji wanaowekeza nchini Tanzania wanaotokea North carolina.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad