JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TCRA yapongezwa kwa Kusogeza huduma kwa Wananchi

Share This

Wananchi wakipata maelezo kuhusiana na usajili kwa alama za vidole katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.
 MKuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman akikabidhiwa kitabu cha Muongozo wa Mawasiliano na Mkuu  wa Kanda ya Zanzibar wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  Esuphatie Masinga (katikati) wakati wa Kampeni ya a Mnada kwa Mnada wa TCRA katika Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.K kushoto ni Mkuu wa Kanda ya Mashariki TCRA Mhandisi Lawi Odiero na watatu kutoka kushoto Afisa Habari Mwandamizi wa TCRA Makao Makuu Mabel Masasi.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman akiweka alama ya vidole wa ajili ya usajili laini ya simu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.
 Afisa Habari Mwandamizi wa TCRA Makao Makuu Mabel Masasi akimpa maelezo mwananchi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada Katika Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.
 Afisa Habari wa TCRA Judith Shao akitoa maelezo kuhusiana vitabu vya Muongozo wa Mawasiliano Katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.

MKUU wa Mkoa  wa Kusini  Pemba Hemed Suleiman ameipongeza  Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania  kwa kuandaa kampeni ya Mnada kwa Mnada kwa kuwa inasaidia  sana wananchi  kupata  huduma  kirahisi

Mkuu huyo  ameyasema hayo wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada  wa TCRA katika Viwanja vya Gombani Mjini Pemba  amesema kwa kusogeza huduma zote  muhimu  pamoja  inawarahisishia wananchi kupata huduma jambo  ambalo  linamanufaa  kwa wananchi  na serikali kwa ujumla.

 Hemed Amewataka  wananchi kutumia vema  fursa ya kampeni huyo  inapofika katika  maeneo yao.

Kampeni ya Mnada kwa Mnada Pemba  katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole. 

Wakazi wa wilaya ya Pemba na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 17 na Zanzibar lengo kuu ni nchi nzima kufikiwa na Kampeni hiyo.

 Mkuu wa TCRA Zanzibar Esuphatie Masinga amesema ni fursa kwa wananchi wa Pemba  kufika katika Viwanja vya Gombani  kwa ajili ya kusajili kwa alama za vidole pamoja na kujiandikisha kupata usajili wa vitambulisho vya Taifa  kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

Masung amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja Huduma zingine za mawasiliano..

Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Mkuu huyo amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Masinga  amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Hata hivyo amesema kuwa
 kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana  makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa.
TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu wanayoipata katika Kampeni mbalimbali.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA  tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Masinga.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole na kupata mwamko wa kutumia simu katika maendeleo.

Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad