JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AITAKA SUMA JKT KUMKABIDHI JENGO JIPYA LA UHAMIAJI JIJINI DODOMA BAADA YA MIEZI 18, WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO, LEO

Share This

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa Jengo hilo ambalo litakua na ghorofa nane unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Katibu Mkuu ameitaka Suma JKT kumkabidhi jengo hilo kwa wakati.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na wa Wizara yake, kabla ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Suma JKT wanatarajia kujenga jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane, na litakamilika baada ya miezi 18. Kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Martin Busungu. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, akizungumza kabla ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, leo. Suma JKT ndiyo Mkandarasi wa jengo hilo lenye urefu wa ghorofa nane, na linatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kushoto), akimuaga Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taida (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, mara baada ya kumaliza kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Suma JKT wanatarajia kujenga jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane, na litakamilika baada ya miezi 18

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (watatu kushoto), Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu (watatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa JKT na Wizara, mara baada ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa Jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

………………..

Na Mwandishi Wetu, MOHA

KATIBU Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu amelitaka Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT), kujenga jengo la Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kwa ufanisi mkubwa na akabidhiwe jengo hilo baada ya miezi 18.

Akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa jengo hilo, kati ya Wizara yake na Suma JKT ambayo iliongozwa katika kikao hicho na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, iliyopo Mji wa Serikali, Kata ya Mtumba, jijini Dodoma, leo, alisema hana shaka na uwezo wa Mkandarasi huyo, ila anaamini ujenzi huo utakua bora na utakamilika kwa wakati.

“Baada ya maandalizi ya ujenzi huu kuchukua muda mrefu lakini hatimaye tumekamilisha, hivyo nawaomba ndugu zangu tufanye kazi vizuri kabisa, na leo ndio siku ya kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi huu,” alisema Meja Jenerali KIngu.

Meja Jenerali Kingu alisema Wizara yake itafuatilia kwa karibu ujenzi huo, ambapo Mkandarasi ni Suma JKT na Mshauri Elekezi ni Chuo Kikuu cha Ardhi, hivyo jengo hilo anatarajia kuwa bora zaidi kutokana na uwepo wa wadau hao.

Kwa upande wake, Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Busungu, alisema aliishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuwa na imani na Suma JKT na kuipa kazi ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya uhamiaji jijini Dodoma.

“Tunaishukuru Wizara yako kwa kutupa kazi hii ya ujenzi wa jengo hili ambalo ni la ghorofa nane, tunaahidi kulikamilisha baada ya miezi 18, na tutapiga kadiri inawezekana, tupo tayari kwa kazi yenye uweledi wa kuzingatia muda na ubora ambao utawauza zaidi Suma JKT,” alisema Meja Jenerali Busungu.

Mkataba huo ulisainiwa na viongozi hao huku ukishuhudiwa na wanasheria wa taasisi hizo ambao ni Mkurugenzi wa Sheria, Marlin Komba wa Wizara hiyo na Kapteni Joyce Mwaikofu kutoka JKT.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad