JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


BILIONI MBILI ZATENGWA KUBORESHA SEKTA YA AFYA JIMBO LA SEGEREA

Share This
Mbunge wa jimbo la Segerea Mh Bonnah Kaluwa amekutana na Wananchi wake na kufanya Mkutano uliozungumzia changamoto mbalimbali na kutengeneza mikakati ya kuhakikisha jimbo hilo linapiga hatua za kimaendeleo.

Kaluwa amefanya mkutano huo jana Jumapili februari 10/2019 na Wananchi wa kata ya Vingunguti ,viwanja vya relini ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamejadiliwa huku wananchi wakikishirikishwa kueleza mawazo yao.

Akizungumza kwenye mkutano huo,Kaluwa alisema kuwa moja kati ya mambo ambayo aliyazungumzia ni suala la barabara ya Vingunguti ambayo imekuwa kero kwa wananchi wake,Kalua amewaeleza wananchi ambavyo amekuwa akifuatilia kuhusu ujenzi wa bara bara hiyo,akawafafanulia kuwa ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

" Kabla ya kuanza ujenzi wa barabara nawaomba Wananchi waliojenga juu ya mitaro kupisha mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa ujenzi huo",aliwathahadharisha Wananchi hao. 

Alisema pamoja na mambo mengine pia lilijadiliwa suala la Afya,ambapo ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuelekeza kiasi cha fedha takribani bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya jimboni Segerea.

"Ndugu wanannchi wa jimbo la Segerea naamini tunakwenda vizuri na tuko pamoja,kiukweli namshukuru sana Rais wetu Dkt Magufuli,ambaye amekuwa akihakikisha usiku na mchana nchi yetu inapiga hatua za kimaendeleo,hivyo fedha tulizopewa nna hakika sekta ya afya jimboni kwetu itaimarika maradufu" alisema Kaluwa.

Katika Mkutano wake,Kaluwa aliambatana na Naibu Meya wa Manispaaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti Mh Omari Kumbilamoto.
Mbunge wa jimbo la Segerea,Mh Bonnah Kaluwa akimuelekeza jambo mmoja wa wananchi wake  aliefika kumsikiliza kwenye mkutano wake.

 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Bonnah Kaluwa (hayupo pichani).
 Mh.Bonnah Kaluwa akiteta jambo na baadhi ya wananchi wake 
 Mmoja wa akina mama akichangia jambo kwenye mkutano huo wa kuhakikisha jimbo la Segerea linapiga hatua kimaendeleo 
 Mbunge wa jimbo la Segerea,Mh Bonnah Kaluwa akizungumza na wananchi wake  .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad