KANGI LUGOLA AAGIZA WANAOSAMBAZA PICHA ZA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO WASHUGHULIKIWE - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

KANGI LUGOLA AAGIZA WANAOSAMBAZA PICHA ZA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO WASHUGHULIKIWE

Share This
 Waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Kangi Lugola ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watu wanaosambaza picha za watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea juzi Septemba 20,2018.

Waziri Lugola ameviagiza vyombo vinavyohusika kufuatilia wanaosambaza picha hizo kwa ni kinyume cha sheria za makosa ya mtandao.

Tangu jana kumezuka tabia kwa baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp,instagram na facebook wamekuwa wakisambaza picha za watu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye magroup na wengine kupost kwenye kurasa zao kitendo ambacho ni kinyume cha sheria,utu na maadili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad