WCF WAENDELEA KUWAFIKIA WADAU WENGI ZAIDI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WCF WAENDELEA KUWAFIKIA WADAU WENGI ZAIDI

Share This
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter, (kulia), akimkabidhi kifunika tairi ya spea (wheel cover), Bibi Lilian Kinyemu, kutoka kampuni ya ABC Limited ya Wilayani Maswa, baada ya kutembelea banda la Mfuko na kupatiwa maelezo huhusu shughuli za Mfuko kwenye kilele cha Wiki ya Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Agosti 7, 2018. Maonesho hayo yanatarajiwa kufungwa leo Agosti 8, 2018 na Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

NA MWANDISHI WETU, SIMIYU
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeendelea kuwafikia wadau wake wengi katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara, hii ni baada ya kushiriki katika maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yanayofikia tamati leo terehe 08.08.2018.
Maonessho hayo yalianza tarehe 01 katika viwanja vya Nyakabindi Vilivyopo Wilaya ya Bariada Mkoani Simiyu. Maonesho haya kwa mwaka huu yameratibiwa na Serikali ya Mkoa wa Simiyu chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Antony Mtaka akishirikiana na Mikoa Jirani ya Shinyanga na Mara.
Pamoja na mambo mengine wadau wote pamoja na wageni waliotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wamepata elimu kuhusu;
1.   Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi
2.   Majukumu ya Mfuko
3.   Mafao yanayotolewa na Mfuko
4.   Usajili wa Waajiri
5.   Uwasilishaji wa Michango kwa Njia ya Kielektroniki
6.   Taratibu za Uwasilishaji wa Madai
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Sebera Fulgence amewasisitiza waajiri wote wakiwemo waliotemeblea banda la Mfuko kutembelea Tovuti ya Mfuko (www.wcf.go.tz) na kufungua Online Service au (Huduma za Kimtandao) ili waweze kujionea huduma mbalimbali wanazoweza kupata bila ya wao kutembelea ofisi za Mfuko. Miongoni mwa huduma hizo ni kujisajili, kuwasilisha michango ambapo wanapata stakabadhi moja kwa moja, waajiri kuona michango wa wafanyakazi wake na kadhalika.
Maonesho hayo yanahitimishwa leo tarehe 08.08.2018. Aidha wawakirishi wa Mfuko wataendelea kuwepo maeneo ya viwanja vya Nyakabindi mpaka tarehe 12 ili wale ambao hawakupata firsa ya kufika toka tarehe moja waweze nao kufika ili wapate elimu kuhusu Mfuko huu.
 Bw. Anselim Peter, (wapili kulia), ambaye ni Mkurugenzi wa Uendeshaji, WCF, Bw. Sebera Fulgence (wapili kushoto), ambaye ni Afisa mwandamizi wa Uhusiano na Mawasilkiano wa Mfuko huo, wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi hawa waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu Agosti 7, 2018.
 Afisa Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasilkiano wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF, Bw. Sebera Fulfence, (kulia), akimkabidhi vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko, kwa mama huyu aliyetembelea banda la WCF 
 Mwananchi akisaini kitabu cha waliotembelea banda la WCF
Wananchi wakihudumiwa kwenye banda la WCF.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad