WATOA VIBALI SERIKALINI BADO WADAIWA KUWA NI KIKWAZO KWA WAWEKEZAJI NCHINI. - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WATOA VIBALI SERIKALINI BADO WADAIWA KUWA NI KIKWAZO KWA WAWEKEZAJI NCHINI.

Share This
Na John Walter-Babati.

Mwekezaji mkubwa mkoani Manyara wa kiwanda cha Mati Super Brand kinachozalisha vinywaji vikali David Mlokozi amewaangukia baadhi ya watumishi wa idara muhimu zinazotoa vibali kuwa ni tatizo kubwa serikalini.

Aidha Mr.David Mlokozi ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo amesema kuwa mamlaka za serikali ni nyingi sana zipo kisheria lakini baadhi zinadidimiza jitihada za serikali ya Rais Magufuli kuwa na uchumi wa viwanda kukwama kwa sababu za kuchelewesha kutoa vibali.

Mlokozi amesema kuwa ulifika muda alikata tamaa na kutaka kuhamishia kiwanda hicho kwingine lakini kutokana na msaada mkubwa walioupata kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti kuruhusu kuendelea na uzalishaji wameamua kubaki.

“Kiwanda kilipofungwa kwa miezi mitatu nilipata hasara sana kwa sababu nilikuwa nikiwalipa wafanya kazi bila kuingiza chochote’.alisema Mlokozi.

Kwa sasa Mati Super Brand imeanza uzalishaji wa maji ya kunywa ambayo kwa sasa wameshapeleka sampuli mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa na muda wowote wanatazamia kuanza uzalishaji baada ya kupata majibu kutoka TFDA.

Aidha Wamefungua kampuni nyingine inayoitwa Manyara Breweries Limited ambayo itakuwa ikizalisha aina nyingine za vinywaji ikiwemo bia kwa kutumia mtama unaolimwa na wakulima mkoani Manyara.

Kiwanda cha Mati Super Brand kilichopo Babati kimetoa ajira kwa vijana wa kike na wa kiume zaidi ya sitini na kusaidia kupunguza wimbi la vijana wasiokuwa na ajira.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad