TULIMKAMATA HALIMA MDEE KWA TUHUMA ZA KUTOA LUGHA CHAFU YA MATUSI KWA RAIS AKIWA NYUMBANI KWAKE-MRAKIBU WA POLISI URAFIKI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

TULIMKAMATA HALIMA MDEE KWA TUHUMA ZA KUTOA LUGHA CHAFU YA MATUSI KWA RAIS AKIWA NYUMBANI KWAKE-MRAKIBU WA POLISI URAFIKI

Share This

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Halima Mdee kwa tuhuma za kutoa lugha chafu ya matusi kwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli akiwa nyumbani kwa wazazi wake.

Ameeleza kuwa, walipofika nyumbani kwa wazazi wa Mdee Ubungo Kibangu, alipokelewa na mama mzazi yake zazi ambaye baada ya kujitambukisha na mahojiani mafupi aliwaeleza wamsubiri Halima anajiandaa kwa kuwa alikuwa amepumzika kidogo.

Mrakibu Kasanga ambaye ni shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka ameeleza hayo leo, Agosti 9,2018 wakati akitoa ushahidi dhidi ya kesi ya lugha ya matusi inayomkabili Mdee.Mdee anadaiwa, Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chadema,, alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.

Akiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amedai Julai 4, mwaka Jana, akiwa katika kituo cha polisi cha urafiki akiendelea na majukumu yake ya kawaida alipokea oda kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni Mark Njela akimtaka kwenda nyumbani kwa wazazi wa Mdee Ubungo Kibangu kumkamata Halima Mdee kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya rais Magufuli.

Amedai baada ya kupewa oda hiyo, walikwenda kama walivyoagiza na walipofika walipokelewa na kaka wa Halima ambaye aliwaelekeza kwa mama yao.Ameendelea kudai kuwa, mama Halima aliwapokea vizuri, akaenda kuongea na Halima na akaomba wamsubiri ajiandae kwa kuwa alikuwa amepumzika kwa kidogo.

Shahidi Kasanga amedai, baada ya hapo Halima alitoka na wakamueleza kuwa wamekwenda kumkamata na kumpeleka Osterbay Polisi na kwamba wakati huo Halima alikuwa yupo vizuri na baadhi ya ndugu zake walitoka wakaongozana nao kwenda Osterbay polisi.

Aidha shahidi huyo alidai kuwa yeye alikuwa hajawai kumuona Halima Mdee ana kwa ana alikuwa akimsikia katika vyombo vya habari ikiwamo TV na Magazeti.

Aliendelea kudai kuwa, baada ya kumkamata, alimpeleka katika kituo cha polisi Osterbay, ambapo Njela hakuwepo hivyo alimpigia simu na akamuelekeza amkabidhi Mdee kwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Ilala(RCO), Davis Msangi.

Mdee anatetewa na mawakili Peter Kibatala na Hekima Mwasipu.

Hekima alimuuliza shahidi huyo kuwa tangu tarehe aliyomkamata Halima Mdee hadi sasa,ulishawahi kuyasikia Maneno yaliyotamkwa na Halima Mdee.

Kasanga alijibu kuwa kwa kweli hakuwahi kuyafuatilia.

Kesi imeahirishwa hadi Septemba 11.2018

Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad