TASAF YANG’ARA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU. - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

TASAF YANG’ARA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU.

Share This
NA Estom Sanga –SIMIYU 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeibuka mshindi wa pili katika kundi la Mifuko ya Jamii kwenye Maonyesho ya NANE NANE yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu kwa mwaka 2018/2019. 

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ndiye aliyemwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika sherehe hizo za NANE NANE kuwakabidhi zawadi washindi mbalimbali ukiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii katika banda lake kulikuwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao wameonyesha bidhaa mbalimbali wanazozitengeneza baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 

Miongoni mwa bidhaa zilizoonyeshwa na Walengwa hao wa TASAF ni pamoja na mkaa wa kupikia walioutengeneza kwa kutumia udongo wa Mfinyanzi na vumbi la mkaa,dagaa,vikapu mazuria ya kufutia vumbi,pochi na vikapu vilivyotengenezwa mwa shanga,nguo zilizoshonwa kwa cherehani,cheni na mapambo ya wanawake. 

Akizungumza baada ya kupokea zawadi hiyo kwenye banda la TASAF, Mtaalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mfuko huo, Bwana Fariji Mishaeli amesema ushindi huo ni kielelezo kingine tosha kinachoonyesha Mchango wa Mfuko huo katika maendeleo ya taifa. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umekuwa ukitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao mkazo wake mkuu ni pamoja na kuwahamasisha Walengwa wake kufanya kazi za kuzalisha mali huku msukumo maalum pia ukiwekwa katika sekta za Elimu ,Afya na Lishe katika ngazi ya Kaya. Zifuatazo ni picha za tukio la kukabidhiwa zawadi na Wananchi kutemmbelea banda la TASAF kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa Tathimini na Ufuatiliaji wa TASAF,Fariji Mishaeli (mbele) akitoka kukabidhiwa cheti cha Ushindi katika Maonyesho ya NANE NANE mkoani Simiyu.
Baadhi ya Watumishi wa TASAF na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Picha ya Juu na Chini ) wakifurahia ushindi walioupata kwenye Maonyesho ya NANE NANE yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Shamrashamra za Ushindi zikielea kwenye banda la TASAF baada ya Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii kuibuka Mshindi wa pili kwenye Maonyesho ya NANE NANE zilizofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Baadhi ya Wananchi (picha ya juu na chini ) wakipata maelezo kutoka kwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwenye banda la NANE NANE kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad