NAIBU WAZIRI WA MIFUGO ABDALLAH ULEGA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KATI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO ABDALLAH ULEGA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KATI

Share This
Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefungua rasmi maonesho ya Nane Nane Kanda ya kati ambayo yanaenda sawa na mashindano ya Nane ya Mifugo kitaifa yanayofanyika jijini Dodoma.

Ulega amefungua mashindano ya Mifugo ambayo yalianza mwaka 2011 na huwa yanafanyika Agosti 5  ya kila mwaka mkoani Dodoma na hujumuisha ng'ombe wa maziwa na nyama walioboreshwa pamoja na Mbuzi wa asili.Akizungumza jana Ulega amesema kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kutambua umuhimu na mchango wa rasmilimali za mifugo ya asili katika kuendeleza sekta ya mifugo nchini.

Aidha amesema kuwa mchakato huo linalenga kutambua juhudi na maarifa wanayotumia wafugaji wa mifugo ili kufuga kwa tija na hatimaye kuvutia wafugaji wengi na kuiga na kuingia kwenye ufugaji wenye tija kwa taifa.Ulega amesisitaza kuwa sekta ya mifugo ni moja ya Sekta muhimu zinazochangia kupunguza umaskini wa wananchi na kukuza uchumi wa nchi kwani ni mhimili katika kuendeleza viwanda kama ilivyoainishwa katika mpango kabambe wa Mifugo Tanzania.

Hata hivyo ametoa maagizo kwa wafugaji na wadau mbalimbali kuunda na kuimarisha vikundi na vyama vya ushiriki ili kuongeza kasi ya uwekezaji katika viwanda vya kusindika mazao ya mifugo na hatimaye kufikia malengo na kauli mbiu ya Nane Nane 2018 isomekayo ''WEKEZA''.Aidha Ulega ameagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha utekelezaji wa mfumo wa utoaji kinga mbalimbali za magonjwa ya mifugo uwe ni lazima kwa wafugaji wote nchi.

Pia Ulega amesema wafugaji pamoja na wafanyabiasha  hawaruhusiwi kuhamisha au kusafirisha mifugo pamoja  mazao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali.Hivyo imesababisha maeneo ya mipakani mwa nchi yetu imeshamiri biashara haramu za mifugo na mazao yake zisizo rasmi na amewataka watendaji kusimamia sheria kwa kushirikiana na wadau ili kutatua changamoto ya utoroshaji wa rasilimali za mifugo yetu na mazao yake.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa mkoa wa mkoa Dodoma wakati wa kufungua rasmi maonesho Nane Nane kanda ya kati na mashindano ya nane ya Mifungo kitaifa yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia viatu katika banda la Magereza vinavyotegene na ngozi katika maonesho ya Nane Nane Nane katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge wakitembelea banda la wajasiria mali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia samaki aina ya kamongo alikaushwa katika banda la wajasiria mali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)


Wafugaji mbalimbali wakionesha mifungo yao katika mashindano ya nane ya mifungo yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma

Wafugaji mbalimbali wakionesha mifungo yao katika mashindano ya nane ya mifungo yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad