MTENDAJI MKUU, MAHAKAMA YA TANZANIA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI YA UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

MTENDAJI MKUU, MAHAKAMA YA TANZANIA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI YA UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI

Share This
Hali ya jengo la Mahakama kuu kanda ya Kigoma lilipofikia
Mtendaji Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma Bw. Moses Mashaka akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi mbele ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Bw. Leonard Magacha.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw Hussein Kattanga (wa kwanza kulia) akikagua kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Wilaya Buhigwe ikiwa ni muendelezo wa kusogeza huduma kwa wananchi mkoani Kigoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Kattanga akitoa maelekezo alipotembelea ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kasulu mkoani Kigoma katika ziara yake aliyofanya Wilayani humo Agosti, 08, 2018.
Picha ya pamoja ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama , viongozi wa Mahakama Mkoa wa Kigoma na wakandarasi wa Masasi Construction wakiwa mbele ya jingo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma linaloendelea kujengwa. (Picha na Festo Sanga, Kigoma


Na Festo Sanga, Mahakama ya Mkoa- Kigoma

Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Husssein Kattanga amefanya ziara mkoani Kigoma na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu lililoanza kujengwa rasmi tarehe Oktoba 28, 2017 chini ya mkandarasi Masasi Construction Co Ltd. 

Ujenzi huo wa Jengo la Mahakama Kuu utasogeza huduma za Kimahakama karibu na wananchi wa Mkoa huo kwani wamekuwa wakisafiri kutoka Kigoma kwenda Tabora kufuata huduma za Mahakama Kuu.

Katika ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa Mahakama alipata fursa ya kutembelea mahakama ya Wilaya Kasulu na kukagua ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kasulu inayotegemewa kumalizika mwezi April 2019 chini ya Mkandarasi M/S Molad Tanzania LTD.

Ujenzi wa Mahakama mbalimbali nchini unalenga katika kusogeza huduma ya haki karibu zaidi na wananchi na vilevile ni utekelezaji dhahiri wa nguzo ya pili ya mpango mkakati wa Mahakama (2015/2016-2019/2020) ya upatikanaji wa haki kwa wakati.

Aidha ujenzi wa jingo hilo la Mahakama na unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019 utawezesha uhifadhi wa kumbukumbu na nyaraka mbalimbali na kuimarisha matumizi ya vifaa vya TEHAMA katika huduma ya utoaji haki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad