Mbunge wa Bukombe azindua wodi ya kisasa ya Mama na Mtoto - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

Mbunge wa Bukombe azindua wodi ya kisasa ya Mama na Mtoto

Share This
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Mashaka Biteko (CCM) amezindua rasmi wodi ya akina mama na watoto katika Kituo cha Afya cha Charles Kulwa Memorial kilichopo Runzewe jimboni humo.

Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini amefanya uzinduzi huo jana Agosti 08, 2018 alipofika katika Kata ya Uyovu kuzungumza na wananchi wa Kata hiyo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kabulima.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Biteko aliupongeza uongozi wa kituo hicho cha binafsi kwa kujenga wodi hiyo yenye vifaa vya kisasa na kutoa rai kuwahudumia wananchi wote kwa kuzingatia taratibu zote za afya ikiwemo kutowabagua wanaotumia bima ya afya.

Mkurugenzi wa kito hicho, Dkt.Baraka Kulwa alisema kilianza kama Zahanati mwaka 1997 kabla ya kupandishwa hadhi mwaka 2015 na kuwa Kituo cha Afya ambapo kinahudumia wagonjwa kati ya 3,000 hadi 4,000 kwa mwezi huku asilimia zaidi ya 70 wakiwa ni akina mama na watoto hivyo ujenzi wa wodi hiyo iliyogarimu takribani shilingi milioni 25 utasaidia kuboresha zaidi huduma za afya kituoni hapo.

“Kwa kweli nashukuru kwa uzinduzi wa huduma hii, inatusaidia sana. Mimi natoka Kakonko lakini nimekuwa nikisikia kwamba hapa kuna huduma nzuri”. Alisema mama Winfrida John ambaye ni mkazi wa Kakonko aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya kupata huduma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad