MBUNGE AWATAKA WANACCM NA WANANCHI MKOANI SINGIDA KUMPA HESHIMA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

MBUNGE AWATAKA WANACCM NA WANANCHI MKOANI SINGIDA KUMPA HESHIMA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI

Share This

Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu (kulia), ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Unyambwa Wilaya ya Singida mjini, Abdulazizi Hamisi Labu, akihutubia wananchi na wana CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika  katika Viwanja vya Kitongoji cha Unyambwa Juu mkoani humo jana.
Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu (kulia), akimnadi mgombea huyo, Abdulazizi Labu.
Naibu wa Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mheshimiwa Musa Ramadhan Sima, akihutubia kwenye mkutano huo.
Kampeni Meneja wa uchaguzi huo, Selemani Hamisi Mdulu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wakazi wa Kata ya Unyambwa Juu wakiwa kwenye mkutano huo.
Wazee wa kata hiyo wakifuatilia mkutano huo.

Muonekano wa meza kuu kwenye mkutano huo.
Naibu wa Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mheshimiwa Musa Ramadhan Sima (katikati), Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Andrew.
Mkutano ukiendelea.
Mgombea udiwani wa Kata ya Unyambwa, Abdulazizi Labu (kulia), akiwa na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida mjini katika mkutano huo.
Madiwani wa Wilaya ya Singida Mjini wakiwa wamepiga magoti kumuombea kura mgombea huyo kwa wananchi.
Vijana wa CCM wakipiga pushapu kumuombea kura mgombea huyo.
Wanawake wa CCM wakiwa wamenyoosha mikono kumuombea kura mgombea huyo.
Mkuu wa Wilaya mstaafu wa Wilaya ya Nchemba, Francis  Mtinga, akizungumza katika mkutano huo wakati akimuombea kura mgombea huyo.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Diana Mkumbo Chilolo, akimuombea kura mgombea huyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Chifu ya Aledi Sylvester akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa, akihutubia kwenye mkutano huo wakati akimuombea kura mgombea huyo.
Mhemiwa Musa Sima , akiserebuka na wanawake wa CCM wakati akienda kuhutubia.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Jimson Mhagama, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida, Aisharose Matembe, akimuombea kura mgombea huyo.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Andrew akimuombea kura mgombea.
Naibu wa Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mheshimiwa Musa Ramadhan Sima, akiteta jambo na Salum Kingi, mwenye ulemavu wa miguu ambaye alikuwa akionesha kuomba msaada fulani kutoka kwa waziri huyo.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akiongoza kutoa kiapo kwa wananchi na wana CCM cha kumchagua diwani Abdulazizi Labu.
Wananchi na wana CCM wakila kiapo hicho.
Mgombea udiwani wa Kata hiyo, Abdulazizi Labu, akiomba kura kwa wananchi.
Watoto nao walikuwepo kwenye mkutano huo.
Wabunge wakifurahi jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni  Mheshimiwa Aisharose Matembe na Mheshimiwa Elibariki Kingu.
Mheshimiwa Musa Sima na Elibariki Kingu, wakiserebuka na wanachama wenzao wa CCM na wananchi huku wakiwa wamejitwika vibuyu. 'Hakika ina pendeza sanaaaaa.'

Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu amewataka wananchi na wana CCM wa Kata ya Unyambwa Wilaya ya Singida mjini kumpa heshima Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa kumchagua mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulazizi Hamisi Labu.

Kingu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea huyo wa udiwani uliofanyika kitongoji cha Unyambwa Juu jana alisema hakuna heshima kubwa ya kumpatia Rais Magufuli zaidi ya kumchagua Labu kuwa diwani wa eneo hilo.

"Ndugu zangu wanananchi na wanaccm wenzangu hakuna heshima kubwa ya kumpa Rais wetu Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chetu Taifa kama si kumchagua Labu awe diwani wa kata hii kwani Magufuli ameonesha kutujali sana wananchi wa Singida" alisema Kingu huku akishangiliwa na wananchi ambao walisema watamchagua Labu.

Kingu alisema heshima kubwa ya kumpa Rais Dk.John Magufuli ni kuhakikisha wana mchagua Labu tena kwa kura zote ili aungane na Rais na mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na si kumchagua diwani kutoka chama kingine.

Alisema Rais Magufuli amekuwa na imani na wananchi wa Mkoa wa Singida kwani amekuwa akisaidia kupeleka miradi mikubwa kama ya maji na kuteua viongozi wa serikali hivyo hawana zawadi ya kumpa zaidi ya kumchagua Labu ili kuongeza kasi ya maendeleo katika kata hiyo.

"Msifikiri haya yote yanayofanywa na Rais yana kuja bure hapana ni imani aliyonayo kwetu wana Singida kutokana na kushika nafasi ya pili kitaifa ya kuwa na kura nyingi tulizompigia  katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2015" alisema Kingu.

Alisema Rais Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuliletea taifa maendeleo kwanza ameanza kwa kuanzisha miradi mikubwa ikiwemo kununua ndege saba za kisasa mpaka wazungu wanamshangaa kwa utendaji wake, miji karibu yote sasa imewekwa taa, kubana matumizi kwani hapo zamani viongozi mbalimbali walikuwa wakipishana angani kwenda nje ya nchi ambapo walikuwa wakitumia fedha nyingi za umma lakini leo hii safari hizo hazipo tena na hata wao wabunge wanapata mshahara na posho za kuhudhuria bunge tu na si kama ilivyokuwa zamani.

Katika mkutano huo viongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Singida wakiwepo wabunge na madiwani walipata fursa ya kuzungumza na kumuombea kura mgombea huyo ambapo wote kwa umoja wao waliomba achaguliwe Labu ili aungane na Rais na mbunge ambao ni kutoka CCM katika kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kuwapelekea miradi mbalimbali ya maendeleo badala ya kumchagua diwani wa upinzani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad