DC ARUMERU AUNGANA NA WAUMINI WA KANISA LA KKKT KATIKA HARAMBEE YA UCHANGIAJI FEDHA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

DC ARUMERU AUNGANA NA WAUMINI WA KANISA LA KKKT KATIKA HARAMBEE YA UCHANGIAJI FEDHA

Share This


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro jana ameungana na Waumini wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Meru kuwasilisha Salamu za Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Arumeru kwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Askofu Elias Kitoi Nasari katika Hafla ya Harambee ya Uchangiaji wa Fedha kwa ajili ya Ununuzi wa Vyombo vya Kwaya pamoja na Gari kwa ajili ya huduma za Kanisa.
Mhe Muro Amelipongeza Kanisa kwa kuendelea Kushirikiana na Serikali katika Utoaji wa Huduma za Kijamii katika Sekta Ya Afya, Elimu na Maji pamoja na Shughuli za maendeleo ya Kijamii.

Mhe Muro amesema Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea Kudumisha na kuimarisha Ushirikiano kati ya Serikali na kanisani katika kuendelea kuwahudumia Wananchi wa Arumeru na Tanzania ambapo amesisitiza kila Mdau kuendelea kusimama na kutimiza wajibu wake katika eneo lake.

Akipokea Salamu hizo, Baba askofu Elias Kitoi Nasari wa Jimbo la Meru Amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuendelea kupambana na Ufisadi pamoja na Maendeleo ambayo yameanza kuonekana katika Taifa la Tanzania.

Askofu Nasari pia Amemshukuru Mhe Rais Magufuli kwa Kumteua Mhe Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kutokana na Wilaya hiyo kukosa Mkuu wa Wilaya kwa Kipindi kirefu na Kusisitiza kuwa Kanisani litaendeea Kuungana mkono jitihada za Serikali katika Kuendelea kuwahudumia wananchi.

Katika Hafla Hiyo Mhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro amejibu baadhi ya Hoja zilizowasilisha na Baba Askofu Nasari ikiwemo ya Changamoto ya Soko la Karoti na Lumbesa ambapo Mhe Muro amefafanua tayari ameshatoa Maagizo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mbili kupitia Maafisa kilimo na biashara kuzungumza na Wafanyabiashara na madalali wanakwenda kununua bidhaa hizo nje ya nchi kwa kuwataka kwanza kununua Bidhaa zinazolimwa na Wananchi wa Arumeru ambazo ubora wake unakidhi Viwango vya kimataifa na endapo Msimu utamalizika zikiwa zimeisha watatoa fursa ya kuagiza katika maeneo mengine ya nchini Tanzania na Sio nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad