CCM YAFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI MTWARA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

CCM YAFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI MTWARA

Share This
Joseph Mpangala -Mtwara.

Mbunge wa nanyumbu William Dua amelazimika kupiga magoti kumuombea Kura Mgombea wa Udiwani Kupitia Chama Cha mapinduzi CCM kata ya Nalingu iliyopo Mtwara Vijijini Shaibu Mtavanga katika Siku ya Mwisho ya Kufunga kwa kampeni za Uchaguzi wa Udiwani Zitakazofanyika Jumapili ya Wiki hii.

Katika Mkutano wa Hadhara Uliohudhuliwa na mamia ya wananchii wa Kijiji cha Nalingu Mbunge wa nanyumbu Seleman Dau alisema Kitendo cha Kupiga magoti kwa utamaduni wa kabila lake ni heshima kubwa hivyo Kuwaomba wakazi wa kijiji hicho Kumpigia Kura ya Ndio Diwani anayegombea kwa Tiketi ya Chama cha mapinduzi.

Awali Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia{CCM}amesema tayari anavisima 30 ambavyo vipo kwenye Mpango wa Kujengwa ili kumaliza changamoto ya maji iliyopo katika Nalingu hivyo Kuwaomba wananchii kujitokeza Kupiga Kura ili aweze kushirikiana na Diwani atakayewaletea maendeo.

“Tunauwezo wa kujenga Barabara kwa maendelao ya hapa Nalingu,Tayari ninavisima 30 Nahitaji Kujenga ili kuweza Kuondokana na Changanoto ya Maji na hili nawaambia Ukweli Nawaahidi Kuleta Zahanati itakayoweza kutatua Changamoto za Afya hasa kwa akina mama wajawazito”Amesema Hawa Ghasia.

Akimnadi Mgombea wa Udiwani Shaibu Mtavanga Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Mtwara Mohamed Saidi Sinani Amewaahakikishia wananchii wa nalingu Kuwa iwapo watamchagua Mgombea wa CCM watahakikisha matatizo ya kata hiyo yanatatuliwa kwa haraka ziadi.
 Mbunge wa Nanyumbu William Dua akipiga Magoti Kuomba Kura Kwa Wananchii ili waweze kumpigia Kura ya Ndio Mgombea Udiwani Kata ya Naingu iliyopo Mtwara Vijijini Shaibu Mtavanga.
 Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia akihutumia wakazi wa nalingu katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi wa udiwani Unaotarajia Kufanyika Jumapili ya wiki Hii.
 Mwenyekiti wa Wilaya ya Mtwara Vijijini Nashir Mfaume Mohamedi akiongea na wananchii wa Nalingu katika Mkutano wa hadhara katika kampeni za Uchaguzi wa Udiwani kata ya nalingu.
  Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara Zakaria Mwansasu akiomba Kura ya Ndio kwa Mgombea wa Udiwani kata ya nalingu Shaibu Mtavanga katika Uchaguzi Unaotarajia Kufanyika Jumapili ya Wiki Hii.
Mwenyekiti Mstaa wa CCM Mkoa wa Mtwara Mohamed Said Sinani akimnadi Mgombea wa Udiwani Kata ya Nalingu Mtwara Vijijini Shaibu Mtavanga katika Kuhitimisha Kampeni za Uchaguzi wa udiwani Mkoani Mtwara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad