AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

AL MUNTAZIR SEMINARI YAWAKUTANISHA WANAFUNZI BARANI AFRIKA NCHINI

Share This
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SHULE ya sekondari ya Seminari ya Kiislamu Al Muntazir kwa mara nyingine tena wamewakutanisha wanafunzi wa shule za Sekondari nchini na nje ya nchi kwa lengo la kufanya mashindano ya kujadili mada mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Mjadala huo umepewa jina la "Mwalimu Nyerere Schools Invitational Debate Championships" ili kuwajenga na kuwaandaa wanafunzi hao kuwa wataalamu na wajuzi kwa miaka ijayo.Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa shule ya Al Muntazir Reuben Kimani ameeleza kuwa mashindano hayo kwa shule za Sekondari na hiyo ni mara ya tatu yamefanyika yakihusisha washiriki zaidi ya 200.

Na hiyo ni kwa lengo la kuwafanya wawe na fikra pana kwa elimu ya chuo watakayoendelea nayo, ambapo ameeleza kuna shule kutoka Zimbabwe na Kenya na wenyeji Tanzania wakiwakilishwa na shule za Tusiime, Shaaban Robert, shule ya wavulana na wasichana Feza, Aghakan na wenyeji Al Muntazir.

Aidha ameeleza kuwa mashindano hayo yatachukua siku 3 wale watakaofanya vizuri watatunukiwa vyeti na watashiriki mdahalo mkubwa utakaofanyika Desemba mwaka huu nchini Botswana. Kuhusiana na maandalizi kwa wanafunzi wao Kimani ameeleza kuwa wametoa mafunzo kwa wiki mbili yakihusisha utafiti hivyo hawana shida kwa shindano hilo na amewataka wanafunzi kuja kujishiriki kwa kutazama na kupata uzoefu kutoka kwa wanafunzi kutoka barani Afrika.

Kwa upande wa washiriki kutoka Al Muntazir Seminari Saloha Aboud wa kidato cha nne ameeleza kuwa wamejipanga kwa ajili ya mashindano licha ya kuonekana kwa magumu ila wamejipanga na watakuwa washindi.

Wameeleza kuwa waliwakilisha nchi mwaka huu katika mashindano ya kuzungumza yaliyofanyika mwezi June nchini Croatia na licha ya kutokuwa washindi ila walipata kitu cha kujifunza na wameeleza changamoto wanazokumbana nazo ni uwelewekaji wa mada hasa kwa wanafunzi wa sayansi kukutana na mada zilizo nje ya uga wao kama uchumi na sanaa.

Naye Mlezi na mwalimu wa somo la Kiingereza katika shule ya Al Muntazir bi. Getrude Mtenga amesema kuwa uzoefu walioupata katika mashindano ya kuzungumza nchini Croatia utawasaidia katika kupata ushindi mwaka huu, maandalizi waliyoyafanya kwa muda mrefu utawasaidia sana na amewashauri wanafunzi kushiriki katika midahalo hiyo na walimu kuanzisha vyama vya midahalo shuleni ili kuwajenga wanafunzi na hiyo itawasaidia wanafunzi kujijenga, kujiamini, kupanga hoja na kuchanganua masuala ya kiulimwengu.Mwalimu na mlezi wa klabu ya Lugha ya kiingereza kutoka Al Muntazir Seminari Bi. Getrude Mtenga akieleza namna shule yao ilivyojipanga katika kukabiliana na mashindano hayo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Seminari ya Al Muntazir, Reuben Kimani akitoa neno kwa washiriki kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mdahalo huo kutoka shule za sekondari nchini.
Wanafunzi kutoka Zimbabwe (wenye suti za bluu) wakisikiliza mjadala uliokuwa unaendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad