JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER

Share This

*Washauri inunuliwe na ndege ya mizigo ili kusafirisha bidhaa za Tanzania


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAFANYABIASHARA wa nchini Oman wamesema wamefurahishwa na hatua ya Rais Dk.John Magufuli kununua ndege ya Dreamliner huku wakishauri inunuliwe na ndege ya mizigo itakayotumika kusafirisha bidhaa za Tanzania na nchi yao.

Mwenyekiti wa Baraza la Biashara kati ya Tanzania na Oman Seikh Saud Al Rawadhi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa baraza ambapo wafanyabiashara wa nchi hizo mbili wamekutana kujadii fursa za kibiashara kati ya nchi hizo.

Sheikh Al Rawadhi ametumia nafasi hiyo kueleza wameona Dreamliner imetua nchini Tanzania na kwamba wafanyabiashara wa Oman wanampongeza Rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hiyo.

“Tunampongeza Rais Magufuli kwa kununuzi Dreamliner .Ni hatua nzuri katika kuimarisha sekta ya anga nchini.Wafanyabishara wa Oman tunaomba ipatikane na ndege ya mizigo itakayotumika kusafirisha bidhaa za Tanzania kwenda Oman,”amesema Sheikh Al Rawahi.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa baraza la kibiashara Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi amewataka wafanyabiashara nchini Tanzania kuchangamkia fursa ya kibiashara kwa kuuza bidhaa zao nchini Oman.

“Wafanyabiashara changamkieni fursa ya soko lililopo Oman wanahitaji bidhaa za aina mbalimbali kutoka kwetu.Wenzetu wana fedha lakini hawana aridhi, na huku kwetu tuna kila kitu hivyo tutumie nafasi hii kupeleka bidhaa huko.“Takwimu zinaonesha kuwa Oman wanauza bidhaa nyingi kwetu kuliko ambavyo sisi tunauza katika nchi yao.Hivyo ni wakati sasa wa kuhakikisha tunauza zaidi bidhaa zetu kwao kuliko ambavy wao watauza kwetu kwani tuna kila kitu,,”amesema Balozi Mwinyi.

Ameongeza jukumu la Serikali ni kuandaa mazingira mazuri ya kibiashara ambayo yatatoa nafasi kwa kupatikana kwa soko la kuuza bidhaa za Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwamo ya Oman na kwamba kumekuwa na mazungumzo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa ajili ya kuimarisha sekta ya biashara.

Wakati huo huo Balozi wa Tanzania nchini Oman Abdalah Kilima amesema kuna fursa nyingi kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuuza bidhaa zao Oman na kufafanua asilimia zaidi ya 90 wanategemea bidhaa kutoka nje ya nchi yao.Pia ametoa mfano kuwa kilo mbili za unga nchini Oman zinauzwa Sh.17,000 na hivyo wafanyabiashara wanaweza kuona namna ya mahitaji ya unga yanayohitajia.

“Watanzania wanaweza kuuza bidhaa za aina mbalimbali Oman.Kutoka Uholanzi mpaka Oman kwa usafiri wa ndege ni saa 11 na kutoka Tanzania mpaka Oman ni saa tano hivyo unaweza kuona kwamba sisi tunaweza kufika kwa haraka Zaidi kuliko nchi zilizo mbali,”amesema Balozi Kilima.
Naibu Katibu MKuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki,Balozi Ramadhani Mwinyi akizungumza mapema jana jijini Dar kwenye mkutano wa pamoja kati ya ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Oman na Wafanyabiashara wa Tanzania , wakijumuika kwa pamoja kwenye kongamano la biashara, kwa madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.

Balozi Mwinyi alisema kongamano hilo ni muhimu kwa Wafanyabiashara hasa kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawajalitumia vyema soko lililopo nchini oman, kuuza bidhaa zao kutokana na nchi hiyo kuhitaji bidhaa nyingi kutoka nje kunakosababishwa na hali yake ya uzalishaji nchini OMAN.
Mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara nchini Oman,Saud Al Rawadhi akizungumza mapema jana jijini Dar kwenye mkutano wa pamoja kati ya ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Oman na Wafanyabiashara wa Tanzania , wakijumuika kwa pamoja kwenye kongamano la biashara, kwa madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.

Mwenyekiti huyo amewataka Watanzania amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kufanyabiashara OMAN huku akisisitiza kuwa baraza lake litatowa msaada wa kila aina ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanafanya biashara na Oman bila vikwazo vyovyote. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika Mashariki na Kati-Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Suleiman Saleh akizungumza mbele ya wageni waalikwa wa Kongamano la Kibiashara kati ya Tanzania na Oman,liliofayika mapema jana jijini Dar Es Salaam.Ambapo kongamano hilo lilikuwa na madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.
Sehemu ya Meza Kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa majadiliano ya Kibiashara Baina ya Tanzania na Oman kwenye kongamano la pamoja lililofanyika jana jijini Dar
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Oman wakipeana ushauri na kubadilishana ujuzi wa kibiashara 
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao. 
Baadhi ya Wafanyabiashara wakifuatilia mada mbalimbali za fursa zilizokuwa zikiwakilishwa ukumbini humo
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao. 
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao. 
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao. 
Piicha ya Pamoja mara baada ya mkutano kuhitimishwa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad