Halmashauri ya yatenga Millioni 370 kuchimba Visima katika Vijiji 16 Tarime. - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

Halmashauri ya yatenga Millioni 370 kuchimba Visima katika Vijiji 16 Tarime.

Share This
Na Frankius Cleophace Tarime.

Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini Mkoani Mara,  imeanza rasmi kazi ya kuchimba Visima Virefu Vya Maji katika Vijiji 16 kati ya Vijiji 88 vyenye thamani ya Shilingi Millini 370, kwa lengo la kupunguza adha ya upatikanaji wa Maji na akina Mama kutembea umbali mrefu ili kutafuta Maji.

Moses Misiwa Yomami ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini amesema kuwa katika Mwaka wa fedha 2016-2017 Halmashauri ilitenga kiasi cha Fedha Mill 150 lakini kwa ajili ya kuchimba Visima Vijiji vya Matongo na Kemambo lakini zoezi hilo halikufanikiwa kwa sababu ya ukosefu wa pesa zilizotengwaambapo Mwaka wa Fedha ambao unamalizika 2017-2018 wametenga Kiasi cha Shilingi Millioni 370 na Vijiji 16 kati ya 88 Vinaenda kunufaika na Mradi wa Kuchimba Visima Vya Maji.

“Tuna Mikaba Miwili hapa Kuna Mkataba wa Visima Nane Virefu vya pampu  Vyenye Thamani ya Shilingi 204 katika Vijiji Nane na Mkataba wa Pili Visima Shilingi Mill 170 ambapo jumla ya fedha tunazitoa kwa ajili ya Uchimbaji wa Visima kupitia Mapato ya ndani itakuwa Jumla ya Shilingi 370” alisema Misiwa.

Yomami ametaja kuwa Vijiji 16 katika Halmashauri hiyo vitanufaika na Mradi kuwa ni Gibaso, Kitawasi, Mutana, Surubu, Nyantira, Boga A Kwisarara na Mangucha pia katika mkataba wa Pili Vijiji Vitakavyonufaika ni Weigita, Nyamirambaro, Mutana, Kimusi, Kewanja, Mjini Kati na Nyangongo jumla Vijiji 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini.

Licha ya Serikali kuletea Maendeleo Wananchi wananchi hao wamekuwa wakidai fidia pale Miradi inapopita ambapo Mwenyekiti amessma kuwa wananachi wamekubali Miradi hiyo hivyo hakuna haja ya kuomba Fidia pale miradi inapofanyika.

Yomami ameongeza kuwa Nyuma kampuni iiyopewa kazi ilikuwa ikifanya Utafiti na kuchukua Mchanga na Kampuni nyingine inakuja kuchimba ikikosa Maji wanashindwa kuwabana kwa madai wao hawakufanya utafiti kazi yao ilikuwa ni Kuchimba Maji lakini kwa Mikaba iliyotolewa kwa sasa imeboreshwa anayechimba Visima hivyo ndiye atakayefanya Utafiti wa eneo lenye maji hiyo yakikosa lazima awajibike yeye mwenyewe na siyo mtu mwingine.

Mwenyekiti amesisitiza Wananchi kulinda Miundombinu ya Maji itakayojengwa Maeneo tofauti kwani Miradi ya Maji imekuwa ikiharibika kwa sababu ya kuaribu Miundombinu hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Moses Misiwa Yomami akiwa ofisi kwake baada ya Kuongea na Vyombo vya habari kuhusu Mradi huo wa kuchimba Visima hivyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad