ASAS DAIRIES KUTOA ZAWADI KEMKEM KWA WATEJA WAO KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YANAYOENDELEA SABASABA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

ASAS DAIRIES KUTOA ZAWADI KEMKEM KWA WATEJA WAO KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YANAYOENDELEA SABASABA

Share This


Baadhi ya wafanyakazi katika banda la maonesho la ASAS DAIRIERS LTD wakihudumia wananchi waliotembelea kwenye banda hilo katika Maonesho ya Biashara ya Sabasaba TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
Wananchi mbalimbali wakijinunulia bidhaa mbalimbali katika banda la ASAS DAIRIERS LTD kwenye Maonesho ya Biashara ya Sabasaba TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
Msanii na Mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM Ummy Wenceslaus (Dokii) akiwa na baadhi ya wafanyakazi katika banda la ASAS DAIRIERS LTD.


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Asas Dairies imesema inatarajia kuanza kutoa zawadi za aina mbalimbali katika banda lao lililopo kwenye Maonesho ya Biashara ya kimataiafa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam baada ya maonesho hayo kuzinduliwa rasmi.

Baadhi ya zawadi ambazo zitatolewa na Asas katika msimu huu wa maoneshao hayo ziko nyingi na miongoni mwa zawadi hizo ni Gym Bag , Power Bank,Peni, fulana, na kofia.Akizungumza leo kwenye banda la Asas lililopo kwenye maonesho hayo Meneja Masoko na Matukio wa kampuni hiyo Jimmy Kiwelu amesema kuwa wanatambua kuwa maziwa ya Asas yanapendwa na kukubalika na Watanzania wengi na hivyo wameamua kutoa zawadi kwa wananchi ambao watafika kwenye banda lao.

Kiwelu amesema utoaji wa zawadi hizo utaanza baada ya kufanyika kwa uzinduzi rasmi wa maonesho hayo na kueleza wamejipanga kuhakikisha kila anayefika kwenye banda lao anapata zawadi na zitatolewa kupitia mashindano mbalimbali ambayo yameandaliwa katika kipindi hiki.

Akizungumzia mahudhurio ya wananchi kwenye banda lao amesema ni mkubwa mno na hiyo inatokana na kukubalika kwa bidhaa zao na kufahamika na walio wengi.Kiwelu amesema ni jambo la faraja kwa kuona wananchi wameendelea kuwaunga mkono kwa kunununua bidhaa zao katika maonesho hayo kwa wingi ambapo pia wameamua kutenga eneo kwa ajili ya kuchezea watoto wakati wakinywa maziwa ya Asas.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad