WILAYA YA BUHIGWE YAANZA UGAWAJI HATIMILIKI ZA KIMILA KATIKA VIJIJI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WILAYA YA BUHIGWE YAANZA UGAWAJI HATIMILIKI ZA KIMILA KATIKA VIJIJI

Share This

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

HALMASHAURI ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imeanza mchakato wa ugawaji wa Hatimiliki za Kimila katika Vijiji vya Mugera, Kajana na Katundu katika Kata ya Mugera na Kajana katika kaya 1025 zitakazo saidia kupunguza migogoro ya ardhi Katika Wilaya na Mkoa kwa ujumla.

Akikabidhi hatimiliki hizo katika kaya 50 za mfano jana katika kijiji cha Muhegera Kata ya Mugera wilayani humo zinazotolewa na mradi wa usimamizi wa maliasili kwa ajili yq kuongeza kipato kwa mwananchi unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania na Ubelgiji chini ya shirika la ENABEL.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema katika kesi 10 zinazofika ofisini kwake kati ya hizo nane ni za migogoro ya ardhi na mbili ni za urithi.

Brigedia Jenerali Gaguti amesema mradi huo utasaidia usalama wa wananchi na kupunguza migogoro ya ardhi ambayo ilisababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kubaki wakiwa walemavu, kwakuwa wananchi wakiwa na maeneo yaliyopimwa na wakiwa na umiliki wa kisheria itasaidia kesi hizo kupungua.

"Na wananchi wataendelea kufanya shughuli zao za Maendeleo na kuachana na tabia iliyokuwepo kwa wananchi wengi kuzunguka kwenye mahakama za Ardhi, na kupeleka kesi za kuibiana maeneo na kuepuka kutumia gharama nyingi kuendesha Kesi hizo,"amesema.
Ameongeza amefurahishwa kwa mradi huo ambao ameuona maeneo mengi aliyopita kukagua mchakato huo ulivyokwenda aa ameona wananchi wengi wanauelewa na wanajua umuhimu wa hatimiliki.Ametoa mwito kwa ciongozi wa Serikali za Vijiji waendelee kuwahimiza wananchi kuja kufuatilia hatimiliki hizi kwani hati hizo nje na kupunguza migogoro ya ardhi itasaidia wananchi kutumia hati hizo kuombaea mikopo kwaajili ya kuendeleza biashara zao.

alisema Mkuu huyo."Wote wanaouelewa faida ya kwanza ni usalama mtu akimiliki hati yake anauhakika wa kumiliki eneo lake kisheria kesi nyingi zinazo pokelewa wilayani kati ya kesi 10 kesi saba ni za migogoro ya ardhi na kesi nyingine ni za mirathi imepelekea kwa kiasi kikubwa watu wengi kupoteza maisha,"amesema .

Hata hivyo amesema maeneo yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za msitu wa kupanda mti kuanza mchakato wa upandaji miti msimu wa upandaji utakapo anza na kutoa rai kwa viongozi wa vijiji kusimamia ipasavyo maeneo ya huduma za kijamii yaliyopimwa kwaajili ya shughuli za ufugaji na kilimo yatumike kwa lengo lililokusudia na wananchi waelekezwe namna bora ya kuyatumia na Kuepusha migogoro kwa wananchi.

Akitoa taarifa ya mradi Mratibu wa Mradi huo wilayani Buhigwe, William Marandu amesema mpango wa matumizo bora ya ardhi ni tokeo tarajiwa namba mbili la mradi ilipima ukubwa wa ardhi ya Kijiji cha Mugera hekta 9401.856 chenye vitongoji vinne ambavyo ni Ruyange, Mugera, Kishaha na majengo na mradi huo ulianza mwaka 2016 kwa kutenga matumizi ya ardhi ya maeneo ya kilimo kekari (6117.076) Malisho ya mifugo Hekati 1207.1, vyanzo vya maji , maeneo ya maziko , maeneo ya makazi hekari 477.78, misitu ya asili 378 na misitu ya kupandwa hekari 1097.3 kwakuwa aridhi ndio chanzo kikubwa cha Mtaji wa Wananchi.
Amesema hati miliki zilizo gawiwa Kwa kaya 50 za mfano ni kati ya hatimiliki 1025 zilizo andaliwa na mradi wa (NRMLED) Kwa vijiji vitatu vya Wilaya ya Buhigwe na hatimiliki 975 zilizobaki zitaendelea kutolewa baada ya ufunguzi wa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi wengine ambao bado hawajafanya utaratibu wa kupata hatimiliki za kimila kufanya utaratibu waweze kupata hati hizo kwa kupitia Idara ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Thadeo Bitumgwa ni mmoja kati ya wanufaika wa Mradi wa ugawaji wa hatimiliki za kimilqa amesema anashukuru kwa kufahamu mipaka ya kiwanja chake anahakika ya kuwa hata pata mgogoro na mtu yeyote na anauhakika wa Kuwarithisha watoto wake eneo ambalo ni salama na bila kuwa na ugomvi na majirani wenzake.

Nae Sospiter Sabuni mkazi wa Mugera amesema hati hiyo anaweza kunufaika nayo kwa shughuli mbali mbali wananchi wengi wamekuwa wakipoteza uhai kwaajili ya kugombea maeneo, na wengine wamepoteza haki zao za kumiliki kwakuwa hawana hati lakini baada ya Kuwa na hati wanauwezo pia wa kupata fidia pindi wanapokuwa maeneo yao yeamechukuliwa kwa shughuli zingine za maendeleo kwa kutumia hati hizo wanaweza kupata fidia.

Kwa Mujibu wa Sera ya Taifa ya Ardhi na Sheria za Ardhi Namba nne ya mwaka 1999, sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba tano ya mwaka 1999 , sheria ya mpango ya matumizi bora ya Ardhi Namba sita ya mwaka 2007 kila Kijiji hakina budi kuandaa mpango wa amatumizi bora ya ardhi kwa madhumuni ya kuwezesha usimamizi na matumizi endelevu ya ardhi na maliasili na rasilimali zake zote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad