WANAWAKE WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAUME ZAO KATIKA KUJILETEA MAENDELEO NA TAIFA KWA UJUMLA. - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WANAWAKE WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAUME ZAO KATIKA KUJILETEA MAENDELEO NA TAIFA KWA UJUMLA.

Share This

Na Frankius Cleophace Tarime

Wanawake wametakiwa kujenga Umoja na Ushirikiano na Waume zao pamoja nakuwa waaminifu katika kutunza mali zao ikiwemo fedha ili kujiinua na kuongeza Uchumi wa Nchi kwa Ujumla.

Hayo yamebainishwa na Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mara Conference George Ezekiel katika Uzinduzi wa Nyumba ya Kulala wageni iliyojengwa na Kampuni ya SOJEMA Mjini Tarime Mkoani Mara.

Askofu huyo amesema kuwa Wanawake wengi siyo waaminifu katika suala zima la fedha jambo ambalo linapelekea waume zao kushindwa kuwaamini na kuwapa Miradi Mikubwa ili waweze kusimamia hivyo amezidi kusisitiza suala la Uaminifu kwa waume zao ili waweze kupewa Mitata na kusimamia Miradi yao kwa lengo la kujikomboa Kiuchumi.

Askofu ameshukuru Kampuni ya SOJEMA kwa kushirikisha Viongozi wa Dini na Serikali katika ufunguzi wa Nyumba ya Kulala Wagenzi iliyopo Mtaa wa Mwangaza Mjini Tarime huku akisihi jamii kuiga Mfano huo wa kufanyia Maombezi Nyumba zao za biashara ili Mwenyezi Mungu azidi kuzibariki na kuepuka Majaribu.

“Wengi waliobarikiwa na Mwenyezi Mungu wamekuwa wakijenga Nyumba zaao ata za kuishi lakini hawashirikishi Mwenyezi Mungu hivyo sasa huu ni mfano mzuri wa Kuigwa” alisema Askofu.

Eziekieli amezungumzia Pia suala la Jamii kuendelea Kutumikia Mwenyezi Mungu na siyo kukumbatia Mila potofu ambzo zinanyima Mwanamke uhuru katika Jamii inayomzunguka likiwemo suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.

Angela Godfrey kutoka kampuni ya SOJEMA anazidi kusisitiza suala la Mwanamke kudhubutu na kudai kuwa wanawake wanaweza hivyo sasa wanaume waweze kuwapa Mitaji na kuwaamini ili kuendesha Biashara zao

“Mimi nimeweza kushirikiana vyema katika Ujenzi wa Nyumba hii ya kulala wageni na mme wangu ameniamini nimekuja kuifungua hayupo yote ni kwa sababu ya uaminifu” alisema Angela.Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mara Conference George Ezikiel Ojwang akikata Utepe kama ishara ya uzinduzi rasmi Nyumba ya Kulala wageni iliyojengwa na Kampuni ya SOJEMA Katika Mtaa wa Mwangaza Mjini Tarime Mkoani Mara.
 Sehemu ya jengo hilo kama lionekanavyo nje
Baadhi ya Wageni mbalimbali walioshiriki kwenye hafla hiyo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad