Wanachama kuogelea wapitisha Katiba mpya - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

Wanachama kuogelea wapitisha Katiba mpya

Share This
Dar es Salaam. baada ya kusua sua kwa muda mrefu, hatimaye Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA) kimepata katiba mpya itakayo waongoza katika mchezo huo hapa nchini.

Katiba hiyo imepatikana katika mkutano mkuu uliotishwa na Kamati ya Muda ya TSA iliyoteuliwa na Baraza la Michezo nchini (BMT) hivi karibuni.
Katika Mkutano huo uliosimamiwa na BMT, wanachama kutoka klabu mbalimbali nchini walipitisha mabadiliko hayo ambayo kwa mujibu wa katiba ya sasa, Zanzibar haitashiriki katika masuala ya uchaguzi kama ilivyokuwa zamani.

Katiba ya zamani iliruhusu wanachama kutoka Zanzibar kushiriki katika uchaguzi na masuala mengine, jambo ambalo ilikuwa tofauti na michezo mingine kama mpira wa miguu, netiboli na mingineyo.

Hata hivyo, kutokana na hali ya mchezo wa kuogelea nchini kutokuwa na vyama vya mikoa na wilaya, ushiriki wa Zanzibar katika shughuli za TSA utakuwepo kupitia habibu za rejea (MoU) baina ya Kamati ya Utendaji ya TSA na Kamti ya Utendaji ya Chama Cha kuogelea cha Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Muda wa TSA, Imani Dominick amesema kuwa wamefarijika sana kukamilisha zoezi hilo lililokuwa gumu na vipingamizi vingi kutoka kwa watu ambao hawakuwa wakitaka kukamilisha zoezi hilo.

Dominick alisema kuwa baadhi ya wadau walipinga waziwazi pamoja na kusambaza ujumbe kuwa Kamati yetu siyo halali kwa lengo la kupotosha pamoja na ukweli kuwa BMT ndiyo iliyowaidhinisha kushika nyadhifa hizo baada ya wanachama kuwapitisha katika mkutano halali uliofanyika shule ya Kimataifa ya Tanganyik Upanga.

“Naomba niwapongeze kwa kazi kubwa mliyoifanya kuokoa mchezo wa kuogelea, pia nawashukuru wanachama kwa kuitikia wito wa kuijadili na kuipitisha Katiba mpya, huu ni muongozo wa kisasa na tunaamini tutafanikiwa kwa kiwango kikubwa,”alisema Dominick.Pia aliwahasa wanachama walioshindwa kuhudhuria mkutano huo kutofanya hivyo tena kwani maendeleo ya mchezo yanahitaji mchango wao kubwa kwani chama si cha watu wachache zaidi ya vilabu, waogeleaji na wanachama.

Afisa Michezo wa BMT, Benson Chacha naye aliwashukuru wanachama hao kwa kufanikisha zoezi hilo na kuwaomba kujikita zaidi katika kuuendeleza mchezo huo na kuachana na masuala ambayo yatarudisha nyuma mchezo huo.“Mmefanya kazi vizuri sana kukamilisha zoezi hili ambalo lililkuwa gumu sana, mmefanya kazi kubwa na ya kupongezwa, sasa mnatakiwa kujikita zaidi kwenye maendeleo ya mchezo, BMT itawapa ushirikiano mzuri sana,” alisema Chacha.

Baadhi wa wajumbe wa Kamati ya Muda na Wanachama wa chama cha kuogelea nchini (TSA) wakiwa katika picha ya pamoja na mjumbe wa Baraza la Mchezo nchini (BMT) mara baada ya kupitisha Katiba mpya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad