728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, June 7, 2018

  WAFANYABIASHARA KATIKA MINADA WILAYANI WATAKIWA KULIPA USHURU

  Na Shani Amanzi

  WANANCHI wa Wilaya ya Chemba wameshauriwa kutumia fursa ya minada midogo inayozunguka wilayani humo kwa lengo la kufanya shughuli za kimaendeleo ili kukuza uchumi hasa katika shughuli za kibiashara huku wakihamasishwa kulipa kodi.

  Hayo yamesemwa na Ofisa Minada wa Wilaya ya Chemba Elisante Sendato wakati alipokuwa katika mnada wa Paranga hivi ambapo amefafanua kwa upande wao watasimamia vema shughuli za mnada ili ziende sawa hasa kwa watendaji na wataalam wanaokusanya mapato kwa kutumia mashine maalum.

  Sendato amesema kuwa " pia tunaendelea kutekeleza agizo la Halmashauri kwa kila mnada lazima uwe na choo ambapo agizo hilo lilitoka Januari mwaka huu na kwa upande wa Paranga ujenzi wa vyoo upo kwenye hatua za mwisho,"

  Kuhusu mafanikio amesema ni makubwa kwani huduma ya kisoko majumbani, ajira kwa wakazi wa Paranga na kupatia mapato Halmashauri ya Chemba imeongezeka.

  Wakati huohuo Diwani wa Kata ya Paranga Hamis Ninga amewataka wafanyabiashara wawe na moyo wa kulipia ushuru wa bidhaa wanazouza na kuhakikisha .Pi wamefanya mkutano na viongozi wa minada ili kuhamisisha wenye biashara kutambua wanao wajibu wa kulipa ushuru.
   Ofisa Minada wa Wilaya ya Chemba Elisante Sendato
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAFANYABIASHARA KATIKA MINADA WILAYANI WATAKIWA KULIPA USHURU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top