'UMASIKINI NI MOJA YA SABABU INAYOCHANGIA MIMBA, NDOA ZA UTOTONI' - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

'UMASIKINI NI MOJA YA SABABU INAYOCHANGIA MIMBA, NDOA ZA UTOTONI'

Share This
Na Woinde Shizza ,Mwanza

 IMEELEZWA sababu kubwa inayosababisha mabinti wadogo kujiingiza kwenye vitendo vya kujamiana na hatimaye kupata mimba na ndoa za utotoni ni umasikini katika jamii wanazotoka.

Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) ambaye pia ni Balozi wa Kampeni  ya Binti wa kitaa Angello George wakati akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya BINTI  WA KITAA iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mwanza .

Kampeni hiyo inakuja ikiwa ni siku chache toka Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsi ,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndungulile kueleza kuwa tangu Januari hadi Aprili Mkoa wa Shinyanga takribani mimba 18,000 za utotoni zimepatikana.

Hivyo amesema kampeni hiyo itahusisha mikoa yote ya Kanda ya Ziwa naitafanyika kwa muda wa zaidi ya  mwaka mmoja kwa lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba na ndoa za utotoni  nchini.
"Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazosababisha mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,"amesema.

Ameongeza Binti wa kitaa imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 18 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani.
Amesema wanatarajia kwenda kuifanya kampeni katia mikoa zaidi ya 20 nchini huku ikiwa na ajenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa kitanzania.
  
Ameongeza kuwa yeye kama mtanzania ameguswa na tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hasa katika kipindi hiki cha utandawazi, hivyo anaamini kupitia kampeni hiyo jamii itaelimika.
"Inauma kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi tano duniani  zinazotambulika kwa janga la mimba na ndoa za utotoni.

"Hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo,"amesema Angello.Sambamba na uzinduzi huo uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mwanza , Balozi Angelo ametoa mwito kwa watanzania wote kuunga mkono kampeni hiyo  ili kuwasaidia mabinti kuepukana na mimba a ndoa za utotoni.

Nao wanafunzi  kwa nyakati tofauti wamesema ili kufikia malengo yao jamii ya kitanzania iwasaidie kuwalinda na kuwajengea uwezo wa kujitambua .
 Moja ya mabinti waliohudhuria katika uzinduzi huo ni Veneranda Paul ambaye amewaomba wazazi kushiriki kikamilifu kwenye kampeni hiyo.

 Kwa upande wa Mwalimu wa Malezi katika shule hiyo Mwanambesi amesema ili Tanzania iwe salama na yenye maendeleo ni jukumu la kila mtanzania kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF) inayoendesha  kampeni ya BINTI WA KITAA   Angelo David George akiwa anazungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Mwanza,namna ya kuepuka mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni  .
Wanafuzi wa shule ya  Mwanza Sekondari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) ambaye pia ni Balozi wa kampeni ya BINTI WA KITAA  Angelo George  wa pili kushoto (Picha na Woinde Shizza,Mwanza) 
Mmoja wa Wazazi alieyehudhuria katika uzinduzi huo, Bi Carol Nzogere akizugumza na wanafunzi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad